DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi nina mfano halisi sababu chaka langu la tonge la kila siku napatia kwenye afya za watu,kuna hizi dawa kama antibiotics ambazo sio common mtaani bei ya hasa amoxclav huwa tuchukua 4000 ila tunaipiga 12 maeneo yetu japo na mimi kuna sehem nilibamizwa kuna changamoto ya afya ilinikumba ni dawa ya kutuma muda mrefu kidogo nilitumia kidonge kimoja kila siku karibia miaka mitatu sasa nilikuwa mkoa wa katavi kidonge ilikuwa 150 sasa nikasafiri kwenda musoma huko nikiamini bei ni moja nitachukuwa huko basi kufika musoma mjini kabla ya kwenda kijijini nakuoelekea basi kupitia famacy moja nauliza wanauza mia sita kidonge kimoja na wanatoa kwa kibali cha dakitar na wanaangalia kaandika za miezi mingapi nikiangalia nimeambiwa nimeze kwa miezi mitatu kabla ya kurudi kwa tabibu kupiga hesabu ni 54000 du nilikacha na nikasema japo dawa ina withdral side effects nyingi nitakaza hadi nirudi mpanda kule pa 150 na vidonge kumi wanakupa kwa hiyo huku nako ni jipu,tangu kikwete airuhusu afya kuwa biashara huria basi ni kujipigia tu,ila wakuu sijui hii hela ni ya laaana maana ningumu kumwona jamaa kwenye afya kuwa na ukwasi wa kutisha labda wale wenye hospital zenye majina
 
Hujawaona sekta ya afya wenye hela? Nimesoma nao na nilitakiwa niende sekta hiyo, ninao wengi wenye hela ninawaona. Wamiliki wa huduma/biashara sio wafanyakazi.
 
Ujerumani hawana kabisa dawa za Malaria.

Sitasahau.
 
😅😅 Ku exaggerate Jambo mfano wewe ni observer wa Jambo / tukio Fulani
Mfano umeenda chooni ukakutana na nzi wakubwa wakubwa
Akatokea mtu akakuuliza wewe ukasema umeona NZI WAKUBWA KAMA TEMBO CHOONI
Huko ndipo ku exaggerate Jambo 😅😀😂
 
Ujerumani hawana kabisa dawa za Malaria.

Sitasahau.
Kuna nchi zimefanya eradication of malaria ukienda uko kichwakichwa utajua hujui, tupe mrejesho ilikuwaje mkuu.

Alafu afya ni biashara kama biashara nyingine, sasa wabongo ujima na ujamaa umewalemaza wao wanataka ununue dawa kwa 40,000 uuze kwa 60,000 wakati ina expire, inaweza sababisha kesi, kusoma mpaka upate kibali ni mbinde, regulations za duka la dawa ni ngumu. Wao wanataka biashara ya nihurumie.
 
Kwani wewe hujui Daslade Kila kitu Kiko Exaggerated and total manipulated? Kama tu mfano gharama ya kitu kama Cake ambayo mikoani inauzwa 20K Dar wanauza 50k ukiuliza kwa nini wanadai Decor Pumbavu Kwani watu wanaenda kula hayo Marangi rangi ya Urembo na Ukiharisha infact Dar Kila kitu Kiko
 
Sasa hapo umepigwaje na wakati wao wamekuambia wanachukua moja kwa moja BOHARI KUU
 
Mwaka 2015 nilibahatika kwenda Frankfurt bana.
Nilitoka na Malaria huku Tz, nilikuwa sijui.

Ilibaki kidogo nikate moto.

Kuna Mtumishi mmoja alijiongeza kuniagizia mseto kutoka Moshi ndio ikawa pona yangu!!

Siendi tena Ulaya bila kuwa na dawa, zile muhimu muhimu.
 
Wizi tu

Juzi nimeenda kununua vidongea vya kuzuia Allergy

Nimepigwa vibaya Sana

Nadhani hawafikirii Mbali hawa wadada wa pharmacy
 
Kama wauzaji wa Misoprostol wanapiga bei kinyama kuanzia elfu 30 hadi 60 kwa vidonge vinne wakati wao wananunua kwa 500 mpaka 1500 kidonge kimoja. Sema huku nilipo kuna duka nimeliotea wananiuzia buku 12 tu ila maduka mengine kuanzia 20 na kuendelea
 
Kuna pharmacy nilienda Sina hamu, nilinunulishwa dawa Aina 2 tofauti zote zinafanya kazi moja, nilivyotumia nikaanza kuzidiwa, nilipomuona doctor akaniambia nilipaswa kunywa Aina moja tu na sio zote kwa pamoja.
 

Nafahamu magonjwa ni faragha ya mhanga, lakini kama ulitaka kutusaidia ukataja ni vidonge vya kaswende sugu, nani jamvini angekujua Kikulachochako amepata kaswende ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…