Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Labda alikuwa anaondoa uchovu....dereva ukihisi uchovu/usingizi Park gari nenda kalale/kapumzike ukiwa fredh safar iendelee..Acha umbea mkuu
 
Yes, nami nahisi hivyo hivyo. Walipaki sehemu kupata huduma fulani kisha safari iendelee.

Hii taarifa ina harufu ya majungu na unaa dhidi ya dereva husika.

"Dereva alipaki Sakina Bar, akawashusha waombolezaji, yeye akaingia Bar kunywa na kucheki mechi ya EPL" ...

halafu eti ushahidi wa shutuma hii ni hizo picha mbili !!!

Kwa picha hizo, nani aweza thibitisha hapo ni Sakina Bar?

-Kaveli-
Nadhani huo unaweza kuwa unatoa walau mwanga fulani katika kuupata ukweli wa tukio hilo.

Sijaamini kwamba dereva wa Serikali anaweza kujisahau kiasi hicho na akawa bado yupo katika ajira yake.

Mtoa Taarifa naye naona hayupo makini na Taarifa hiyo kwani sijaona ni tukio la tarehe gani na huyo aliyehojiwa ni nani katika waombolezaji/familia husika.
 
Sisi tutajua kama kweli ni bar hapo !!??

Hata kama ni baa, huko ndani ya jeneza muhusika yumo tayari ndani????

Sisi tutakuamini vp, je labda unavisa na dereva wa gari ONESHWA hapo juu???

: MKAZANE MAISHA MAGUMU 😆
Maswali ya kishetani na ya kuzimu..hapo unajiona na wewe una akili..subiri yakukute
 
malisa aache unafki sisi wachaga mbona tunakaaga bar na maiti sasa mmeingia njia panda saa tisa usiku na mtapeleka mwili saa 9 usiku,

huyoo dereva kapiga hesabu zake kaona akifikisha mwili saa saba usiku then what.
 
Maeneo ya njia panda Himo, kukuta gari za maiti zimepark watu wanakula/kumwagilia moyo baada ya safari ndefu kutoka Dar kuja Kaskazini ni kawaida.

Inawezekana wahusika walipita hapo sakina Bar kupata chochote kitu ili waendelee na safari

Mleta mada: hiyo maiti ilitokea wapi na inapelekwa wapi?

Hii inaweza saidia kujua kweli dereva alipaki hapo kwa lengo baya au nzuri
si ndio maana nasema malisa mnafki njia panda ya moshi pale hajawai kukaa na maiti bar. akipata supu na vinywaji kusubiri papambazuke.
 
Labda alikuwa anaondoa uchovu....dereva ukihisi uchovu/usingizi Park gari nenda kalale/kapumzike ukiwa fredh safar iendelee..Acha umbea mkuu
Huwa naona wana-park na kulala kwa kuegemea usukani au kulegeza kiti chake kwenye gari kama hana msaidizi. Bado ninahisi kama ni tukio la kweli, basi dereva kwa makubaliano na wahusika wote walikwenda kupata huduma muhimu na baadaye safari iendelee.
Ni kwa nini Mtoa taarifa anatumia neno "Bar" ilhali zipo hoteli nyingi kando ya barabara zina huduma ya chakula pia?
Nakubaliana na ww huo unaweza kuwa ni uchonganishi au umbea kwani angeonesha basi walau picha ya dereva akiwa kwenye ukumbi akiangalia mpira kuthibitisha hoja yake.
 
Yawezekana wamekubaliana hivyo na wengine ndugu wa marehemu wameshuka na wameenda kuhemea.
 
Na Malisa GJ

Habari kaka.

Kuna tukio limetokea hapa Arusha usiku huu limenisikitisha sana. Kuna Familia imepata msiba, wanatakiwa kusafirisha kwenda wilayani kuzika lakini hawana uwezo. Hivyo wameomba msaada wa gari ya serikali kusafirisha maiti. Gari hiyo imebeba maiti na ndugu wachache wa marehemu.

Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.

Binadamu wote wana haki ya kulindiwa utu wao. Umaskini usiwe sababu ya kudhalilisha wengine. Huyu dereva angekua amefiwa na baba yake mzazi, angediriki kwenda kumuanika bar halafu aangalie mpira? Namba za gari ni STM 3708. Tunaomba serikali ichukue hatua kali kwa dereva na wote waliohusika. Huu ni udhalilishaji mkubwa wa utu.

View attachment 2788969View attachment 2788971
Je wafiwa aliwatelekeza wapi au alikuwa nao bar?
 
Huwa naona wana-park na kulala kwa kuegemea usukani au kulegeza kiti chake kwenye gari kama hana msaidizi. Bado ninahisi kama ni tukio la kweli, basi dereva kwa makubaliano na wahusika wote walikwenda kupata huduma muhimu na baadaye safari iendelee.
Ni kwa nini Mtoa taarifa anatumia neno "Bar" ilhali zipo hoteli nyingi kando ya barabara zina huduma ya chakula pia?
Nakubaliana na ww huo unaweza kuwa ni uchonganishi au umbea kwani angeonesha basi walau picha ya dereva akiwa kwenye ukumbi akiangalia mpira kuthibitisha hoja yake.
Huyo jamaa ni mwongo, sijui alitaka aungane nao kulia
 
Maswali ya kishetani na ya kuzimu..hapo unajiona na wewe una akili..subiri yakukute
Hapana mkuu. Ni maswali ya msingi sana hayo ukizingatia kwamba baadhi ya watu wana mizengwe sana na hapo inawezekana hata pia picha hizo zikawa ni "edited" aka photoshopping. Tutajuaje kama jamaa amehitilafiana na dereva katika kitu kingine tofauti lakini kwa lengo la kumkomoa mtoa Taarifa anatumia picha hiyo?? au mtoa taarifa amenunuliwa?
 
Kwani akiwa mama kitu gani?
Tunapenda sana kukuza mambo.
Ni misiba mingapi watu tunapaki mahotelini na mabar tunakunywa mpaka pakuchwe na tunaelekea majumbani? Siwapendi watanzania wenzangu kwa unafiki na uchonganishi. Hapo njia panda ile bar ya did watu wanapanda mpaka juu ha meza na misiba yao wanacheza mziki. Kwahiyo kisa imaskini wao ndo utumike kumkaanga jamaa? Akishafukuzwa kazi ndo marehemu atafufuka? Hao wamama wanaoangua kilio wako wapi? Jamaa akiangalia EPL yuko wapi? Na wanaelekea wilayani sehemu gani? Na hao waliotoa gari kwanini waliwapa ya wazi na vumbi lote hilo? Je mvua ingenyesha je?

Mambo mengine tujifunze kuwa positive tu. What if lilikua litokee jambo baya hapo endapo wangeondoka?
Siupendi umaskini na maskini wenyewe. Tuna roho mbaya sana.
After all kama ni kufiwa na hawakua wakimudu kwanini hawakuzikia sehemu aliyofia?

Kinachotutesa Watanzania ni kusahau kuwa nchi hii ni kubwa na ina tamaduni tofauti nyingi katika mambo mbalimbali!!

Unavyouchukulia msiba wewe Mchaga ni tofauti na Mmakonde anavyouchukulia! Mfano: unaweza kutega barabara ya kusini usione msiba unasafirishwa kwenda kusini bali kutoka kusini kwenda Kaskazini!!

So, ukimwambia mtu kama huyo kwamba tunasafirisha msiba na tukakaa mahali tukala na kunywa kusubiri kukuche, anakushangaa hizo nguvu unapata wapi?? You see??

Wao wakifiwa hakuna linalowezekana tena mpaka marehemu azikwe kwanza!! Na obvious huzikwa siku hiyo hiyo au labda kama kafa jioni basi kesho yake!! Wakati wa kusubiri maziko kila kitu husimama!!

Nimeshangaa kwa sababu aliyeanzisha mjadala ni Malisa atakuwa anajua mambo za kusafirisha maiti! Ila wanaokomaa kuhusu gari ya maiti kupaki bar hao ni tamaduni nyingine ambazo hayo mambo kwao hayapo
 
Cha kushangaza dereva amekuja na maiti hapa Sakina bar, amepaki gari, akawashusha ndugu wa marehemu kisha akaingia ndani kutizama EPL. Nimeumia sana kuona wamama wako nje wanalia, jamaa yuko ndani anakunywa na kuangalia game. Hakika umaskini ni mbaya sana. Naomba upaze sauti ili serikali iweze kuchukua hatua kwa kitendo hiki cha kinyama na kisicho cha utu.
Lakini hata ninyi wanaume wa Arusha mnastahili lawama, mlishindwaje kumuonya au kumvutia nje na kumlamba bakora?
 
Je wafiwa aliwatelekeza wapi au alikuwa nao bar?
Hawajatelekezwa mkuu. Inaonekana wazi kwamba aliingia nao humo ndani kwani hapa nje hawaonekani/hawapo ila yupo mtu mmoja anaongea na simu na pengine habari za maiti/marehemu hazimhusu.
 
Hawajatelekezwa mkuu. Inaonekana wazi kwamba aliingia nao humo ndani kwani hapa nje hawaonekani/hawapo ila yupo mtu mmoja anaongea na simu na pengine habari za maiti/marehemu hazimhusu.
Sad
 
Nakazia akapimwe akili na mkojo
Kwani imethibitika ni mvutaji wa bangi? Hivi kumbe wavuta bangi huwa wanatakiwa wakapimwe akili na mkojo!!!.
Inashauriwa Tusihukumu kabla hatujaupata ukweli.
 
Back
Top Bottom