Arusha: Dereva wa Serikali aenda na maiti bar

Labda alikuwa anaondoa uchovu....dereva ukihisi uchovu/usingizi Park gari nenda kalale/kapumzike ukiwa fredh safar iendelee..Acha umbea mkuu
 
Nadhani huo unaweza kuwa unatoa walau mwanga fulani katika kuupata ukweli wa tukio hilo.

Sijaamini kwamba dereva wa Serikali anaweza kujisahau kiasi hicho na akawa bado yupo katika ajira yake.

Mtoa Taarifa naye naona hayupo makini na Taarifa hiyo kwani sijaona ni tukio la tarehe gani na huyo aliyehojiwa ni nani katika waombolezaji/familia husika.
 
Sisi tutajua kama kweli ni bar hapo !!??

Hata kama ni baa, huko ndani ya jeneza muhusika yumo tayari ndani????

Sisi tutakuamini vp, je labda unavisa na dereva wa gari ONESHWA hapo juu???

: MKAZANE MAISHA MAGUMU 😆
Maswali ya kishetani na ya kuzimu..hapo unajiona na wewe una akili..subiri yakukute
 
malisa aache unafki sisi wachaga mbona tunakaaga bar na maiti sasa mmeingia njia panda saa tisa usiku na mtapeleka mwili saa 9 usiku,

huyoo dereva kapiga hesabu zake kaona akifikisha mwili saa saba usiku then what.
 
si ndio maana nasema malisa mnafki njia panda ya moshi pale hajawai kukaa na maiti bar. akipata supu na vinywaji kusubiri papambazuke.
 
Labda alikuwa anaondoa uchovu....dereva ukihisi uchovu/usingizi Park gari nenda kalale/kapumzike ukiwa fredh safar iendelee..Acha umbea mkuu
Huwa naona wana-park na kulala kwa kuegemea usukani au kulegeza kiti chake kwenye gari kama hana msaidizi. Bado ninahisi kama ni tukio la kweli, basi dereva kwa makubaliano na wahusika wote walikwenda kupata huduma muhimu na baadaye safari iendelee.
Ni kwa nini Mtoa taarifa anatumia neno "Bar" ilhali zipo hoteli nyingi kando ya barabara zina huduma ya chakula pia?
Nakubaliana na ww huo unaweza kuwa ni uchonganishi au umbea kwani angeonesha basi walau picha ya dereva akiwa kwenye ukumbi akiangalia mpira kuthibitisha hoja yake.
 
Yawezekana wamekubaliana hivyo na wengine ndugu wa marehemu wameshuka na wameenda kuhemea.
 
Je wafiwa aliwatelekeza wapi au alikuwa nao bar?
 
Huyo jamaa ni mwongo, sijui alitaka aungane nao kulia
 
Maswali ya kishetani na ya kuzimu..hapo unajiona na wewe una akili..subiri yakukute
Hapana mkuu. Ni maswali ya msingi sana hayo ukizingatia kwamba baadhi ya watu wana mizengwe sana na hapo inawezekana hata pia picha hizo zikawa ni "edited" aka photoshopping. Tutajuaje kama jamaa amehitilafiana na dereva katika kitu kingine tofauti lakini kwa lengo la kumkomoa mtoa Taarifa anatumia picha hiyo?? au mtoa taarifa amenunuliwa?
 

Kinachotutesa Watanzania ni kusahau kuwa nchi hii ni kubwa na ina tamaduni tofauti nyingi katika mambo mbalimbali!!

Unavyouchukulia msiba wewe Mchaga ni tofauti na Mmakonde anavyouchukulia! Mfano: unaweza kutega barabara ya kusini usione msiba unasafirishwa kwenda kusini bali kutoka kusini kwenda Kaskazini!!

So, ukimwambia mtu kama huyo kwamba tunasafirisha msiba na tukakaa mahali tukala na kunywa kusubiri kukuche, anakushangaa hizo nguvu unapata wapi?? You see??

Wao wakifiwa hakuna linalowezekana tena mpaka marehemu azikwe kwanza!! Na obvious huzikwa siku hiyo hiyo au labda kama kafa jioni basi kesho yake!! Wakati wa kusubiri maziko kila kitu husimama!!

Nimeshangaa kwa sababu aliyeanzisha mjadala ni Malisa atakuwa anajua mambo za kusafirisha maiti! Ila wanaokomaa kuhusu gari ya maiti kupaki bar hao ni tamaduni nyingine ambazo hayo mambo kwao hayapo
 
Lakini hata ninyi wanaume wa Arusha mnastahili lawama, mlishindwaje kumuonya au kumvutia nje na kumlamba bakora?
 
Je wafiwa aliwatelekeza wapi au alikuwa nao bar?
Hawajatelekezwa mkuu. Inaonekana wazi kwamba aliingia nao humo ndani kwani hapa nje hawaonekani/hawapo ila yupo mtu mmoja anaongea na simu na pengine habari za maiti/marehemu hazimhusu.
 
Hawajatelekezwa mkuu. Inaonekana wazi kwamba aliingia nao humo ndani kwani hapa nje hawaonekani/hawapo ila yupo mtu mmoja anaongea na simu na pengine habari za maiti/marehemu hazimhusu.
Sad
 
Nakazia akapimwe akili na mkojo
Kwani imethibitika ni mvutaji wa bangi? Hivi kumbe wavuta bangi huwa wanatakiwa wakapimwe akili na mkojo!!!.
Inashauriwa Tusihukumu kabla hatujaupata ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…