Arusha: Jeshi la Polisi lasema linafuatilia tukio la msanii Dogo Janja kumjeruhi Mtu kwa kumpiga risasi

Arusha: Jeshi la Polisi lasema linafuatilia tukio la msanii Dogo Janja kumjeruhi Mtu kwa kumpiga risasi

Self-defense must be proportional, meaning the force used in defense must be reasonable and not excessive given the threat faced. For a self-defense claim to be valid, the degree of force used must be equal to the degree of force or harm being threatened; you cannot use deadly force to respond to a minor threat⚖️
 
Uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi kuhusu tukio la Mgombea Udiwani kata ya Ngarenaro (CCM) Abdulaziz Abubakari Chande "Dogo Janja" kumshambulia kwa risasi Bakari Halifa Daudi (18) huko sombetini jijini Arusha umebaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akijihami.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo zimesema kuwa tukio hilo lililotokea Agosti 23 majira ya saa 5:30 usiku lilihusisha bakari kujeruhiwa kwa risasi mguuni.

"Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, wakati Abdulaziz, mkazi wa Levolosi, alipokuwa akishuka kwenye gari, alidai kutaka kuvamiwa na Bakari akiwa na mwenzake wakiwa na silaha ya jadi. Hali hiyo ilisababisha mtuhumiwa huyo kutumia silaha aliyokuwa nayo na kumpiga risasi Bakari," imesema taarifa ya polisi.

Hata hivyo, polisi mkoani Arusha wamewakamata watu wawili kuhusiana na tukio hilo na wamesema uchunguzi zaidi unaendelea.

=======

Kwa hiyo mpaka hapo ni self defence

Ova
 
Police wamekiri kwamba mtu aliyepiga risasi ni dogo janja lakini inawashikilia watu 2 kutokana na tukio hilo .😀😀😀😀.
... typing
 
Polisi wafanya Uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja kujeruhiwa na risasi.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aitwaye Bakari Halifa Daud (18) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

Akitoa taarifa hiyo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2025 muda wa saa 5:30 usiku huko katika maeneo ya Sombetini Jijini Arusha.
Kamanda Masejo ameendelea kufafanua kuwa wakati Abdulaziz Abubakari (30) mkazi wa Levolosi Jijini Arusha akiwa anashuka kwenye gari alidai kutaka kuvamiwa na Bakari Halifa akiwa na mwenzake kwa kutumia silaha ya jadi hali iliyopelekea kutumia silaha aliyokuwa nayo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo ambapo limesema bado linaendelea na uchunguzi.
Yupo saw dogo janja asingekuwa na chuma mida hii angekuwa maiti kijana nunua bastola
 
Hivi hii inshu ya bwanamdogo (DogoJanja) kumpiga risasi ya mguu jamaa mmoja aitwaye Bakar imekaaje?
Kuna baadhi ya majibu ya Jeshi la Polisi yanasema eti Dogo Janja alikuwa anajihami baada ya kuvamiwa.
Screenshot_20250825-135028_1.jpg
 
Polisi wafanya Uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja kujeruhiwa na risasi.

Jeshi la Polisi mkoani Arusha linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aitwaye Bakari Halifa Daud (18) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

Akitoa taarifa hiyo leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2025 muda wa saa 5:30 usiku huko katika maeneo ya Sombetini Jijini Arusha.
Kamanda Masejo ameendelea kufafanua kuwa wakati Abdulaziz Abubakari (30) mkazi wa Levolosi Jijini Arusha akiwa anashuka kwenye gari alidai kutaka kuvamiwa na Bakari Halifa akiwa na mwenzake kwa kutumia silaha ya jadi hali iliyopelekea kutumia silaha aliyokuwa nayo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo ambapo limesema bado linaendelea na uchunguzi.
Noma sana
 
Sasa nawe huu ni uzi? Hii si yafaa tu kuwa comments huko kwa wenzako.. kaa hapo subiri mods wakuunge.

Back to topic, kwa hii miaka niliyoishi huku sishangai kilichotokea as wanasema kimetokea Sombetini kule si uswahilini pro!! Lolote laweza kuwa limetokea
 
Dogo Ganja asingemsambaza miguu huyo kibaka leo mngekuwa mnawatuhumu wasiojulikana na kuwashanhilia CCM kutafunana wenyewe kwa wenyewe.

Kibaka lazima atawanywe fuvu na utumbo.
 
Kama kweli alitaka kuvamiwa ni sawa kabisa moja ya mguu inatosha. Mheshimiwa Diwani mtarajiwa hana kesi ya kujibu kwani silaha ni ya kujilinda na siyo kupigia picha.
 
Wameeleza kisa chote halafu wanasema wanachunguza. Wanachunguza kipi sasa
Hasa si lazima wachunguze kujuwa kama ushahidi aliotoa Dogo Janja ni wa kweli ama ni wa kutunga.Na uchunguzi ukikamilika kama amedanganya sheria itafuata mkondo wake.
 
Back
Top Bottom