Uchaguzi 2020 Arusha: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia

Uchaguzi 2020 Arusha: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Arusha. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.


Mkoa wa Arusha una jumla ya majimbo ya uchaguzi 7 ambayo ni;

Arusha Mjini:
Mrisho Gambo (CCM) - Kura 82,480
Godbless Lema (CHADEMA) - Kura 46,489

Karatu:
Daniel Awaki (CCM) - Kura 49,042
Cecilia Pareso (CHADEMA) - Kura 31,150

Arumeru Magharibi:
Noah Lembrus Mollel (CCM) - Kura 72,160
Gibson Blasus (CHADEMA) - Kura 22,743

Arumeru Mashariki:
John Daniel Pallangyo (CCM) - Kura 84,858
Rebecca Michael Mgondo (CHADEMA) - Kura 14,688

Longido:
Dkt.Steven Kiruswa (CCM) - Kura 61,885
Pauline Laizer (CHADEMA) - Kura 1,037

Monduli: Fredrick Lowassa(CCM) - Kura 72,502
Cessilia Ndossi(CHADEMA) - Kura 4,637

Ngorongoro:
William Ole Nasha (CCM) - Kura 63,536
Jaqueline Swai (CHADEMA) - Kura 7,983.

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Kituo nilichopo wameweka wazee, wapo slow mno. Wanashindwa hata kuangalia jina la mtu kwenye daftari. Mtu mmoja anatumia dakika saba hadi kumi. Ni upotevu wa muda.
 
Hujuma zozote dhidi ya uchaguzi Arusha hazitavumuliwa Watanzania waachwe wachague viongozi wanaowataka.
 
Big up kwa kutupa habari za yule mpepeta mchele anavyoanguka.
 
Leo nimeamka saa 11:40 asubuhi kuwahi kituoni kwenda kufanya jambo la muhimu kwangu.

Haiwezekani hadi mitandao ya kijamii tunafungiwa?

Tumekosa nini? Hawajui maelfu ya watanzania wamejiajiri kupitia mitandao ya kijamii na mawasiliano ya internet kwa ujumla?

Mimi nimewakataa mazima hadi mwisho wa maisha yangu.
 
Back
Top Bottom