Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Nilishasema huyu ni mganga njaa. Hana ukweli wowote. Ni opportunist mtafuta uteuzi. Kila anayekuwa madarakani yeye ni wa kumsifia tu! Mnaona bandiko lake hili?
 
Pascal I agree with you,Mama anaupiga mwingi na anajitahidi sana kuweka mambo sawa anahitaji kupewa Moyo na kuungwa mkono,ila katika hii thread mimi nimependa zaidi hicho kipengele kimoja cha Kikosi kazi kuita baadhi ya watu kana kwamba wao tu ndiyo wenye haki hiyo ya kutoa maoni kwa niaba ya wengine.

Hii ni point nzito sana ambayo inahitaji thread huru kabisa kwa maslahi ya Taifa sijui kwanini umeificha humu ndani.

Unarudi vizuri kwenye Mstari kama ninavyokusifu na wewe una madhaifu yako kama mwanadamu hasa kwenye mtazamo hasi dhidi ya Chadema,jipime hapo kidogo.
 
Imefikia mahali adi mnatumia jina la MUNGU kwa uongo,

Pascal Mayalla wewe ni mkristu?
Amri ya 3 inasema " Usilitaje bure jina la MUNGU wako "

Usifikiie mahali ukamkwaza MUNGU kisa Ugali
 
Leo nilikuwa namsikiliza rais Samia akizungumza baada ya kuwaapisha majaji wapya 21, kati ya majaji 22 aliowateua hivi karibuni.

Kiukweli huyu Mama ni baraka kutoka kwa Mungu!. Amezungumzia tofauti ya utoaji haki kati ya majaji wa kike na wa kiume, kile kitu nilichokisema kuhusu majaji kuwa na jicho la haki, Rais Samia ameizungumzia kuhusu majaji wanawake kutenda haki kuliko majaji wanaume, hivyo anakwenda kuteua majaji 50/50.

Akizungumzia Kamishana Mkuu wa Magereza amewataka Magereza kuwatenda vema wafungwa kwa hoja kuwa sio wafungwa wote ni wahalifu kweli, kuna wengine wanafungwa kwa circumstantial evidence lakini sio wahalifu.

Ukimsikia Samia analiagiza nini Jeshi la Magereza kuwa treat vipi wafungwa, wale mnaomkumbuka yule alitaka wafungwa wahudumiweje, mtakubaliana na mimi , Samia na yule ni mbingu na ardhi!.
Kiukweli acheni tuu Mungu aitwe Mungu!.
Ujio wa Samia ni baraka ya aina yake kwa Tanzania.
Mungu mbariki Samia
Mungu ibariki Tanzania.
P
 
2. Heshimi Haki za binadamu ambazo zimeainishwa kwenye Katiba. Kuna uvunjifu wa haki za binadamu mdogo mdogo
Kwenye eneo hili la haki za binaadamu, Mama Samia, apewe kongole sana, huyu ni mpenda haki, muwaza haki, msema haki, mtenda haki.
Ameonyesha kwa kauli na matendo!.
Mifano iko mingi tuu ya kumwaga hapa nakupa mifano mitano tuu!, ukitaka 10, nakupa, ukitaka 20 nakupa
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Kwenye eneo la haki, so far Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendo, is the best of the best... ila sasa kwa kwa kadri siku zinavyokwenda, naona kama na yeye anaanza... itaendelea!, nitamalizia ...

P
 
P.
 
Mtu anaweza akawa na sifa zoote mbili.
Anajipendekeza halafu anasifia kiukweli!
 
huyu jamaa wakati watu wanapotea potea aliandika chochote? wakati uchaguzi unavurugwa na mwendazake aliandika chochote? kama aliandika basi atu-pastie hapa tusome.
 
Naendelea kusisitiza Kauli huumba!.
Mwaka huu twende na hili!
Mungu Mbariki Samia ayetende haya kabla ya kumaliza kipindi chake cha kwanza 2025, maana kipindi cha pili 2025 -2030, sauti zimeisha anza anza
P
 
Kwa vile leo ni birthday ya Rais Samia, nawaomba wana jf wote ambao ni well wishers, tuungane kumu wish Happy Birthday this lovely lady Rais wetu mpendwa, Rais wetu mpenzi, Rais wetu kipenzi, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, Chifu wa kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania, ambayo Kanda ya kabila hilo ndio Kanda determinant ya kura za urais wa JMT, Chifu Hangaya.
Happy Birthday.

P
 
Kama ni mtenda kweli na msema kweli,kama nimtenda haki na msema haki sawa lakini swali muhimu ni je vipi watendaji wake kwenye wizara na idara mnalimbali serikalini?

Hilo nalo naomba mkaliangalie
 
Leo ndio siku yenyewe ya wanawake duniani, hongera sana kwa wanawake wote duniani akiwemo Mwanamke huyu!.
P.
 
 

Tunapoelekea mwisho wa mwaka, huku tukielekea mwaka wa uchaguzi, nafanya tathmini ndogo ya expectations zangu na awamu hii ya Rais Samia, nili expect nini, nini kimefanyika, nini bado hakijafanyika, na nini kinaweza kufanyika kabla ya 2025 ili Watanzania tufanye Uchaguzi Mkuu huru na wa haki unaosimamiwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

Katika bandiko hili, nilikuwa na the following expectations
Kufuatia matendo haya, naamini kabisa kupitia “kikosi kazi”,
1. soon Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa,
2. ataifumua na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuifanya iwe shirikishi,
3. pia atazifumua sheria kandamizi kuzifanyia marekebisho ili kufanya uchaguzi wa haki kwenye uwanja sawa wa ushindani na sio huu uwanja tenge wa uchaguzi wetu.
4. Ombi la kufanya mabadiliko ya katiba kuondoa ubatili uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu.
Expectation number 1, imetekelezwa.
Expectation number 2 na number 3, imo on a pipeline mwezi February 2014.
Expectation number 4, ya kutuondolea ubatili kwenye katiba yetu, bado halijashughulikiwa, ila sasa tumuombe Rais Samia, hata kama muda uliobakia hauwezi kutupatia katiba mpya, muda huu unatosha kufanya mabadiliko madogo ya katiba, kuuondoa huo ubatili kwa jinsi ile ile ulivyochomekewa, na kutuwezesha tukafanya uchaguzi Mkuu huru na wa haki.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Namfanyia Rais Samia kitu kinachoitwa MTR (Mid Term Review) ya hoja za bandiko hili
Hili linakwenda kufanyika Bunge la February, ila it's very unfortunately ule ubatili bado upo!.
Uhuru huu haupo!.
  1. Katiba hiyo imetoa uhuru wa kila Mtanzania kuwa huru kushiriki uchaguzi kwa kugombea nafasi yoyote na kushiriki kuwachagua viongozi wetu, bila vikwazo vyovyote. Hili ndilo lilikuwa lengo la mtunga katiba.
Haki hii haipo!
Ubatili Huu bado upo!.
Niliyawasilisha in person
View: https://youtu.be/f5YJTJjG9rw?si=0iLEWvMHsvgSS0gY mimi ni huyo mzungumzaji wa mwisho hapo kwenye hiyo video
Ombi hili bado halijajjibiwa ila muda bado upo
Ili kuwasaidia Watanzania kuijua katiba yao,sheria zao na haki zao, nimejitolea kusaidia
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=dldJIno9G2jIxKQp
Hitimisho
Jana kwenye mitandao ya kijamii, zimesikika habari, Tundu Lissu amelipwa haki zake zote alizo dhulumiwa, hivyo hapa ni uthibitisho tuu wa matendo ya haki na sio tuu kauli za haki.
Lissu anasema aliahidiwa lakini bado hajalipwa!.
Kufuatia matendo haya, naamini kabisa kupitia “kikosi kazi”, soon Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa,
Ameruhusu!
ataifumua na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuifanya iwe shirikishi,
hili litafanyika
pia atazifumua sheria kandamizi kuzifanyia marekebisho ili kufanya uchaguzi wa haki kwenye uwanja sawa wa ushindani na sio huu uwanja tenge wa uchaguzi wetu.
hili litafanyika.
Hii mpaka sasa bado,
Kama atamaliza na hili la katiba
Nimalizie kumshukuru Mungu kwa kutuletea Samia: Ni muwaza haki, msema haki , mpenda haki na mtenda haki!. Soon ataruhusu mikutano ya siasa na kuiunda NEC Shirikishi, jee vipi kuhusu ubatili huu ndani ya Katiba yetu?
Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kutuletea Samia
Asante Mungu kwa Rais Samia, ni Baraka kwa nchi yetu!, naomba lile jicho, liuone na ubatili huu ndani ya katiba yetu, lituondoshee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025!.
Jicho lione
Mungu Mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
Mungu Mbariki Rais Samia,

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Kuna muda Pascal Mayalla anarudi na kujiteka mwenyewe. Niseme pia maisha ni bahati unaweza ukasifia sana na usibahatike kamweee

Unaweza ukatumia akili mno na usipate kitu, unaweza kuwa mropokaji na ukapata kila kitu mpaka usivyokua ukihitaji.

Kuwa huru ukihitajika utatafutwa, mkuu Pascal Mayalla angeendelea kuwa machachari au huru leo hii angekuwa mbali sana, teuzi angepata kwa kuwa ni mtu huru kama walivyopata wakina Hussein Bashe, Makonda, Sulemani Jafo, PolePole, Msigwa, Msando, Jokate.......

Fungu alilochagua jamaa ni fungu la wote, ata asiye na akili anaweza kusifu na watu wanaosifu hawana adhari sasa kwa nini tuwape teuzi ili kuwafunga midomo wakati walishaamua kuifunga wenyewe.
Pascal Mayalla hapendwi na upinzani wala chama tawala, kwa sasa siyo karata yenye mashiko tena! Sio mtii, sio muoga tatizo hana misimamo. Muda aliopigwa vita na awamu ya tano ndio ulikuwa wakati wake sahihi wa kuchanua kwa kutunisha misuli ya kichwa na kumwaga sumu zaidi ikiwezekana kukimbia nchi leo hii angekuwa nguli kwenye medani za siasa za Tanzania na angetafutwa akapewa majukumu.

Kwenye ulimwengu wa bahati sioni kesho yake iliyobora zaidi naona balaa na ajali za kisiasa zikimsogelea kwa kificho. Naomba Mola amuepushe kwa hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…