Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Ubongo wa mzee sana lakini msomaji wa Vitabu huendelea kuwa active ukilinganisha na wa mzee asiye msomaji. Mfano mzuri ni Donald Trump. Kwa umri wake wa miaka 92, ilitegemewa aendelee kuwa active kwenye kazi? Vitabu vinasaidia sana.
 
Ni sahihi Mimi nilikua napendelea kusomaa vitabu magezeti hata barabarani nikiona kipande Cha karatasi lenye maandishi nasoma kwa sababu nilikua naamin mtu ambaye kaandika ana akili timamu ,,akili ilibadilika sana nilivo maliza chuo nikawa sitaki kuajiriwaa ,,kujiamin sana ,,shetani haogipwi ,,ikifika kipindi nikawa nalala mlango wazi nikiamin siwezi fanyiwa unyama na binadamu Wala shetani .
 
👏👏👏

Natamani tuanzishe club ya wasoma Vitabu! Naelewa unachosema. Naelewa mnooo!!!
 
Mimi namshukuru Mungu nimeanza kusoma vitabu nikiwa mdogo Sana, nilivyojua tu kusoma na nyumbani pia wazazi walikua wasomaji yaani nilikua nasoma vitabu,magazeti,majarida yaani nikikutana na maandishi tu Mimi nasoma hahah,nakumbuka nikiwa darasa la tatu au la nne niliishiwa vitabu nikaona nyumbani biblia kuubwaa nikaisoma lile agano la kale huwa ni Kama stori nilisoma lote nikamaliza Ila nilivyofika agano jipya nikaona sielewi nikaacha.
Pia nilipata mwalimu ambaye alielewa hobbie yangu nikiwa darasa la Kwanza akawa kila wiki ananiletea kitabu kimoja Cha hadithi nikisoma nikamaliza namrudishia ananipa kingine.Mpakq nimekua mtu mzima kwakeli nimesoma vitabu vingi Sana hadithi za watoto, novels genre nyingi nyingi, vitabu mbalimbali vya personal Growth na Non fiction nyingi sana pamoja na spiritual (Christian books) bado naendelea kusoma Kama ulivyosema vitabu ni chakula Cha akili yaani Kuna vitu vingi nimejifunza na vimenisogeza hata kwenye maisha ya kawaida kupitia vitabu.
 
hii nasadiki maana hata mm nawafundisha watoto mbinu nayoitumia nafundisha kidogo wanajisomea muda mrefu
 
Sijawahi kusoma na sina ninachokijua hivyo ninauliza na unijibu
 
Soma na vya Kiswahili pia, utajua tofauti ya 'thamini' na 'dhamini'.
 


400? Too much, vya subject hiyo hiyo
 
Usomaji ulinisaidia kushinda interview zaidi ya mara moja- interview za kazi, mbili zikiwa ni za kazi ambazo hazikuwa zikiendana moja kwa moja na taalum yangu.

Ujasiri niliokuwa nao, ambao kimsingi, ulitokana na usomaji wa Vitabu, uliwashawishi waliokuwa wakinisaili wanikubali.

Fikiria, tuliofanya interview tulikuwa zaidi ya 150, tukigombea nafasi tisa tu. Halafu Sasa, wenzangu, wengi wao walikuwa na taalum za hiyo kazi.

Niliwezaje kupenya?

Vitabu vilinisaidia kujiamini na hatimaye nikapita.
 
Kwamfano mimi sijawahi kusoma ata kitabu kimoja.

Naanzaje? Nipe tips nianze mdogo mdogo.

Je, ata kusoma vitabu vya story ni msosi wa Medulla oblongata? Au lazima viwe vitabu vya "How to become Wiseman"? "You was born to win"?
Soma hata vya hadithi, kama vimeandikwa na wabobezi, utajikuta unaboresha uelewa wa lugha inayotumika n.k.
 
Anasoma la ngapi
 
Soma hata vya hadithi, kama vimeandikwa na wabobezi, utajikuta unaboresha uelewa wa lugha inayotumika n.k.
Exactly! Muhimu tu, ahakikishe ni chakula salama.
 
Hongera sana mkuu. Ukiweza, waambukize na wengine!

Ni baraka kushea chakula kizuri na wenzako.
 
Ukisomaa sana vitabu jamii yote itakua kiganjani unawezaa fanyaa ukitakacho wakakuelewa.
Ni kweli, maana akili ni kama kiwanda.

Taarifa unazoziingiza ni raw materials. Itazichakata na kukupa product stahiki.

Ndiyo maana, kwa wasomaji wa Vitabu, ni rahisi zaidi kuibua mawazo mapya tofauti na wasiosoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…