Asikudanganye mtu, vitabu ni chakula muhimu sana cha akili

Naaam ni hiki hiki Ila
Topic inaitwa pleasing personality
 
Kwa mnaosoma vitabu nashauri soft copy ziwe mfumo wa epub na si pdf . EPUB inakupa option nyingi na inakuwa kitabu kabisa tofauti na hizi pdf . EPUB ni kitabu halisi ingawa inahitaji application nzuri kuweza kuifungua. Kwa wanaotumia iPhone ipo app ya books by default , Kwa android unaweza ingia play store.
 
Mkuu kama w
Mkuu kama ww umesoma vitabu huku hata kuandika kiswahili huwezi ni bora usiendelee kusoma!dhamini hapo imetumikaje?mbona sioni uhalali wa dhamini hapo!!
 
Ni browser am?
 
Mkuu kama ww umesoma vitabu huku hata kuandika kiswahili huwezi ni bora usiendelee kusoma!dhamini hapo imetumikaje?mbona sioni uhalali wa dhamini hapo!!
Mkuu, hata mimi nilihisi kuna makosa mengi sana, ila sikuwa na uhakika hasa ikizingatiwa kuwa mimi si mtaalam wa lugha. Almanusura hata niahirishe kupost humu jukwaani kwa kuhofia kuwa ujumbe niliotaka kuwasilisha usingeeleweka. Lakini nilipokumbuka kwamba anayetaka kuwa bora hapaswi kuogopa kukosea, nilijipiga moyo konde na kupost kama nilivyofanya.

Labda mkuu, unaweza ukanielekeza namna ambavyo nilipaswa kuandika?

Nashukuru kwa usaidizi wako.
 
Ni browser am?

EPUB ni format tu Kama unavyoona word pdf n.k

 
πŸ™πŸ™πŸ™ Shukran mkuu. Nimeshaipata.
 
Ili usome vitabu na uelewe unapaswa usiwe na stress.
Ili ufanye mazoezi unapaswa usiwe na stress
Ili ule na ushibe unapaswa usiwe na stress
Ili unywe na ufurahi unapaswa usiwe na stress
Unadaiwa ada za watoto, pesa ya kujikimu huo muda wa kuupa ubongo chakula unapata wapiii?
 
Ukiwa na stress ni sahihi kufa njaa?

Kama hata mtu akiwa na stress bado anahitajika kula, ndivyo ilivyo pia na usomaji.

Ukiwa na stress, unaweza usiwe na muda wa kula na kunywa kwa anasa, lakini lazima kula chakula na kunywa maji kwa ajili ya kuendelea kuishi.

Ndivyo ilivyo na vitabu. Ni sehemu ya maisha ya akili yako. Isitoshe, stress inaweza kuchangiwa na upungufu wa lishe sahihi kichwani.

Kusoma Vitabu sahihi kutakusaidia ama kuepuka stress, kuishinda, au kuimanage.
 
Ili usome vitabu na uelewe unapaswa usiwe na stress.
Stress inachangiwa na aina ya taarifa uliyoilisha ufahamu wako. Kwa kusoma vitabu sahihi, unaulisha ufahamu wako taarifa chanya chanya. Taarifa chanya zinapokuwa nyingi akilini mwako huzifisha taarifa hasi zisababishavyo stress.
 
Embu tuwe realistic. Huna hata pesa y nauli ya daladala kitabu cha 50000 utanunua ukianzia wapi?
 
Ili ule na ushibe unapaswa usiwe na stress
Ili unywe na ufurahi unapaswa usiwe na stress
Usipokula kwa sababu ya stress utakufa. Stress ikikufanya ushindwe kusoma Vitabu vizuri, itakufanya "udumae" kiakili na kuendelea kuendelea kutawaliwa na stress.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…