Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Hao CCM siyo wazanzibar?


Ccm si wazanzibari. Ni mabolozi wa Tanganyika ndani ya Zanzibar. Hawana uwezo hata wakushinda majimbo ma 10 bila ya nguvu ya dola. Na maeneo yenye nguvu ya CCm nimeonea ya wahamiaji kutoka bara.
Hebu zitizame izo sherehe uwanjani kuna wananchi waliohudhuria? majukwaani mumejazwa JKU na KVZ. Watumishi wa serekali na wanafunzi wa skuli za serekali hulizimishwa kwa nguvu kuhudhuria. Mapambo ya sherehe utayakuta kwenye maskani za CCm na ofisi za serekali tu. Bado Picha hupati. Nenda mwenyewe ukajionee alafu ndo uzungumze.
 
Wewe pia unaonekana ni mvivu wa kusoma au wa kutafuta habari. umekurupuka ulipotoka kwasababu tu hukupendezwa na ukweli mchungu alioambiwa Yerricko Nyerere. Ungepata nafasi ya kusoma kitabu cha KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU kilichoandikwa na Dr.Harith Ghassany ungeelewa vizuri alichokua anamaanisha Mohammed Said kwasababu ndo rejea aliyoifanya kuhusu uandishi makini wa historia, sasa sijui unataka akusanye kitu gani tena au aandike nini. Hivyo hivyo, ukisoma hata kitabu alichokiandika yeye mwenyewe cha MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHID SYKES utaona utafiti wa kina uliofanyika katika uandishi wa kitabu hicho. Kwahiyo,anachojaribu kutuelewesha Sheikh Mohammed, kwamba unapoandika kitabu (hasa vinavyohusu historia siyo riwaya) ni lazima ufanye utafiti tena ikiwezekana kufanya mahojiano na wahusika wenyewe waliokuapo kwa wakati huo ili kupata uhalisia wa mambo na hicho ndicho alichofanya Dr.Ghassany. Sasa Yerricko anavyoandika upupu wake anakua amemhoji nani au amefanya utafiti gani? hivyo ni haki kabisa mtu mwingine kusema anafanya ' Plagiarism'.
 
Kwanza nakushukuru kwa kujibu kwa ADABU tofauti na maandishi yaliyomo kwenye uzi wako namba moja...

Umeonesha kujutia vizuri kile ulichokiandika awali, huu ni uungwana mkubwa...


Lakini nikusihi tena na tena, kitabu changu kina rejea (reference's) zote, na zaidi nyaraka muhimu zote...

Ninaamini kabisa kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi wewe mzee hujakiona hata kwa macho ya karibu tu, achilia mbalikukisoma.. Maana ungekuwa umesoma bila shaka kila rejea ungeona... Kwa kukusaidia tu rejea zote zipo mwishoni mwa kitabu achilia mbali zilizowekwa ndani ya maandishi.......

 
Yericko,
Vizuri ujifunze lugha za kistaarabu.

Unaposema, "wewe mzee," ni tofauti na "mzee wangu."

Mfano wa kwanza ni kukosa adabu na wa pili ni staha ingawa maana ni moja.
 
Yericko,
Waamuzi wa hadhi ya kitabu kwanza huwa "reviewers," hawa ni wataalamu wa somo lililoandikiwa kitabu na hawa ndiyo huwafanya watu wakakisoma kitabu.

Kama ipo "review," yoyote tuwekee hapa tuwasikie nini maoni yao kuhusu kitabu chako.
 
Nilimwambia yeriko hakuna cha maana alichoandika ila ukiandika wewe wanasema ni muongo,mdini,mkabila ila wao ni kukopi tu ndo wanachoweza
 
Na ni yapi maoni yako juu ya huyo anaelalamikiwa?
 
BB,
Nina uzoefu mkubwa katika haya.
Naingia Maktaba In Shaa Allah nitakuwekea hapa stori ina zaidi ya miaka 30.
 
BB
Ofisi za Africa Events Banner Street, London alikuwapo Mohamed Mlamali Adam, Ahmed Saleh Yahya, Ahmed Rajab na Mlamali Adam. Alikuwapo na Abdullatif Abdallah huyu kutoka Mombasa. Waliobakia wote Wazanzibari. Hili gazeti lilifanya makubwa na Babu akiandika sana mle. Ikafikia serikali ikawa inalipiga vita chini chini kwa BoT kukataa kuwapa fedha za mauzo ya gazeti hadi yalipofanyika makubaliano maalum nayo ni kumtoa Mlamali kama Mhariri mkuu na kuzuia makala za Mohamed Said. Haya yalifanyika lakini baada ya miaka 3 Ahmed Saleh Yahya akanipa assignment juu ya Rais Mwinyi lakini by line jina langu halikuwekwa nikawa sasa ni Special Correspondent na malipo yakawa ki James Bond napigiwa simu nakutana na mtu ananikabidhi bahasha. Lakini tulimsaidia Mzee Mwinyi na yeye akaeleweka shida anazokutananazo kama Rais kutokea Zanzibar...
 
Hakika wewe ni MAHIRI katika UANDISHI .. Big up .. but nimevutika na title moja isemayo .... "THE MERMAIDS OF MSAMBWENI AND OTHER STORIES" .... hapoooooo penye MERMAIDS hapo ... yaani kila siku iitwapo leo niko CURIOUS kufahamu juu ya hao VIUMBE ... are they REAL or just IMAGINARY creatures ...?
 
BB,
Hiyo hapo juu ni stori ya 1988.

Chukua muda usome ujue tatizo la kuandika historia ya kweli katika nchi za Kiafrika.
 
kwa nini rubawa unaamini kuwa mzee said tu ndo anapaswa kumkosoa au kuwa ndo mwalimu wa yericko?unadhani umri ni kigezo cha kusema yeye yericko akubaliane na hata kile asichokiamini? si sawa. tukiamini hivi tutapelekana shimoni maana kipofu hawezi mwongoz akipofu mwenzie. simshauri yericko akubaliane na mzee said. namshauri apingane naye kwa hoja. hakuna mwenye hati miliki ya elimu au ufahamu.na hili halihusiani na dini wala mtizamo. nadhani ukaribu na imani uliyo nayo kwa mzee said kama unavyosema kuwa ulimpigia simu vinakufanya pengine utiwe upofu wa kufikiria kinyume na yeye...hivyo ukajikuta kila alisemalo wewe waitikia "hewalaah" au tawile. ashakum si matusi.sisi wazee wa siku hizi tunakataza sana ufuasi.
 
nimemsoma rubawa anaonekana kuwa ni mfuasi mtiifu wa said mohamed kiasi kwamba kwa yeye haoni hata sababu ya kutafakari yale yanayosemwa na ustaadhi mzee wetu said mohamed. kitu ambacho naona ni kibaya sana kwa ustawi wa akili. yeye anachosisitiza ni kuwa fuata kile kinachosemwa na mzee said naye atafurahishwa nawe.

Unataka ushahidi wa kipi ikiwa kitabu hujakisoma?

Nimekufafanulia hapo kwamba marejeo yote yamewekwa wazi, au hujui maana ya marejeo?
 
Msamehe huyo mzee ni rafiki yangu yupo Buguruni Malapa ni mfuasi mtiifu wa Mohamed Said....

Hawa wazee wote ni watu ninaowamudu vizuri, niliwahi kubishana nao hapa miaka miwili mfululizo usiku na mchana, wana chuki sumu ya koboko inasubiri...wadini hasaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…