Askari polisi adaiwa kufia gesti akimtoroka mwanamke, Polisi Watoa tamko

Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.
Huyu alichapwa risasi tuache kuvungavunga
 
Askari Polisi jijini Arusha mwenye namba Pf 18530, Stewart Saiba(40) amefariki dunia katika mazingira ya utata katika nyumba ya kulala wageni ya Mrina shine iliyopo makao mapya jijini hapa.

Taarifa za awali kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina Lake lihifadhiwe zimedai kuwa, Saiba aliingia katika nyumba hiyo majira ya saa sita usiku akiwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake hakufahamka mara moja .

Aliieleza kuwa marehemu aliandikisha katika kitabu cha wageni na kupewa chumba namba tano na kisha kuingia katika chumba hicho akiwa na mwanamke huyo, kibegi kidogo cha mgongoni na radio ya mawasiliano aliyokuwa ameshika mkononi.

Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.

Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa ,Justin Masejo ili kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba mara baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kutopokelewa.

Mwili wa marehemu Stewart unatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao Bukoba kwa ajili ya maziko, baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Mwenyezi mungu alilaze mahala pema peponi roho ya marehemu Stewart, Amen!
Watu wengine hawaibiwi kizembezembe
 
Kaiba simu ya mwanamke, manjagu wenzie waitwa saa tisa usiku ila wakafika baadaye sana na mwisho alikuwa anatoroka na chips🤣
Kuna kitu.Wamerahisisha hadithi mnoo!Kachukua simu bila ruhusa(wizi),kaangukia kichwa(wrecklessness).Katoroka eneo la tukio hatarishi(kagomea ukamatwaji halali).Lakini hilo la kupata jeraha na kuvuja damu(?) lichunguzwe.Hakukuwa na mob-justice kweli(kujichukulia sheria mikononi)?
 
Kama alinunua chips kwann hawakuila mpaka anarudi nayo?

Kama bia aliingia nayo kwann hakuinywa au kumpa mwenzie mpaka anaamua kurudi nayo?

Kama mchezo umepewa mpaka mtu kalala fofo na wakati umeingia wahudumu walijua lazima utakuwa n Askari sababu ya rediokol sasa kulikuwa na ulazima gani aruke ukuta?

Kwa mazingira yale Kama alifanikiwa kumwacha Mwanamke akiwa amelala fofofo na kumchukulia simu yake huku chakula na bia akiwa navyo mkononi pamona na kutambulika kuwa n Askari sidhan Kama alishindwa kupitia njia ya mlangoni.

Hapa kuna shida nyingine zaidi ya hili mnalojadili humu.

Nataka hilo faili litoke polisi walikete ofisini kwangu kwa uchunguzi zaid
Angetoka mlangoni, lazima mhudumu wa gesti angekwenda kumwamsha yule demu, ili ahakiki kama yuko salama (watu huwa wanaua wenzao "gesti" nakukimbia). Sasa hapo Mbinu ya askari kutoroka na Chips, Bia na simu ya demu si ingejulikana??? Ndio maana askari aliamua kutumia mbinu za "MEDANI" - kuruka ukuta na kuwakimbia wote - mhudumu wa "gesti", Mlinzi wa "gesti" na Malaya.
 
CCM bila polisi ni wepesi kama kalatasi
 
Angetoka mlangoni, lazima mhudumu wa gesti angekwenda kumwamsha yule demu, ili ahakiki kama yuko salama (watu huwa wanaua wenzao "gesti" nakukimbia). Sasa hapo Mbinu ya askari kutoroka na Chips, Bia na simu ya demu si ingejulikana??? Ndio maana askari aliamua kutumia mbinu za "MEDANI" - kuruka ukuta na kuwakimbia wote - mhudumu wa "gesti", Mlinzi wa "gesti" na Malaya.
Wewe umemaliza kesi
 
Duh mungu nijalie mwisho mwema.vifo vingine ni aibu kubwa unaenda motoni direct
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu so kama huendi directly unapitia wapi kwanza kabla ya kwenda huko motoni? Au kumwagilia moyo kwanza?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kama alinunua chips kwann hawakuila mpaka anarudi nayo?

Kama bia aliingia nayo kwann hakuinywa au kumpa mwenzie mpaka anaamua kurudi nayo?

Kama mchezo umepewa mpaka mtu kalala fofo na wakati umeingia wahudumu walijua lazima utakuwa n Askari sababu ya rediokol sasa kulikuwa na ulazima gani aruke ukuta?

Kwa mazingira yale Kama alifanikiwa kumwacha Mwanamke akiwa amelala fofofo na kumchukulia simu yake huku chakula na bia akiwa navyo mkononi pamona na kutambulika kuwa n Askari sidhan Kama alishindwa kupitia njia ya mlangoni.

Hapa kuna shida nyingine zaidi ya hili mnalojadili humu.

Nataka hilo faili litoke polisi walikete ofisini kwangu kwa uchunguzi zaid
Kama alisema pesa ya lodge atalipa kesho ili hali hana kitu?
 
Najiuliza wamejuaje kwamba alikuwa anamtoroka mwanamke!??

Je huyu marehemu alimwambia mtu kuwa nipo na demu nakula show, ila nikimalizana nae nitamtoroka!??

Pia kwa maaskari wetu walivyo wababe sidhani kama angehitajika kuruka geti, pale ilikuwa anakwenda kumface mlinzi na kumuamuru amfungulie hata ikibidi angejitambulisha,, mlinzi asingegoma asilani

Kuna utata ktk hili
tyc walijuaje kwamba alikua anatoroka. Jibu.
Walimuuliza huyo mwanamke maana hiyo alfajiri alikua hajatoka room, halafu alikua na uchovu wa kushughulikiwa na poti na chips alizoahidiwa atawapelekea watoto wake zillibwa pamoja na simu yake.
 
Back
Top Bottom