Askari polisi adaiwa kufia gesti akimtoroka mwanamke, Polisi Watoa tamko

Askari polisi adaiwa kufia gesti akimtoroka mwanamke, Polisi Watoa tamko

Yaani mafunzo yote ya medani anakimbia mwanamke? Angetumia zile mbinu wanazitumia kuwadunda Chadema na vibaka.

Yaani huyu alikula ugali wa chuo Cha polisi bure
Hii mkuu aingii akilini nini kilichomfanya ashindwe kuondoka kwa kupitia mlangoni tena Askari? Ikiwa makahaba wanakuibia na kupita mlangoni bila tatizo lolote?
 
ndo aina ya askari wetu nchini

1--- ulalaji fofofo wa changudoa wake (kunamashaka kumbukeni chupa ya bia kwenye begi lazima huyo dada aliwekewa madawa kufanikisha utoro wake)

2---hakua na lengo lakutia lengo wizi wa cm mungu kajibu maombi
 
Najiuliza wamejuaje kwamba alikuwa anamtoroka mwanamke!??

Je huyu marehemu alimwambia mtu kuwa nipo na demu nakula show, ila nikimalizana nae nitamtoroka!??

Pia kwa maaskari wetu walivyo wababe sidhani kama angehitajika kuruka geti, pale ilikuwa anakwenda kumface mlinzi na kumuamuru amfungulie hata ikibidi angejitambulisha,, mlinzi asingegoma asilani

Kuna utata ktk hili
Kwani alikuwa kavaa uniform?
 
Angetoka mlangoni, lazima mhudumu wa gesti angekwenda kumwamsha yule demu, ili ahakiki kama yuko salama (watu huwa wanaua wenzao "gesti" nakukimbia). Sasa hapo Mbinu ya askari kutoroka na Chips, Bia na simu ya demu si ingejulikana??? Ndio maana askari aliamua kutumia mbinu za "MEDANI" - kuruka ukuta na kuwakimbia wote - mhudumu wa "gesti", Mlinzi wa "gesti" na Malaya.
Toka lini gest aliepanga chumba akiondoka anaulizwa aliekuja nae kama vitu vyake vimetimia? Walau ingeingia akili kama huyo mwanamke anaondoka ndio aamshwe mwenyeji wake aulizwe swali kama hilo
 
Hii mkuu aingii akilini nini kilichomfanya ashindwe kuondoka kwa kupitia mlangoni tena Askari? Ikiwa makahaba wanakuibia na kupita mlangoni bila tatizo lolote?
Yaani utoroke Nia yako usitambulike ni wa wapi? Asa halafu ukajitambulishe Kwa mlinzi mie ni Askari si tayari ushauza ramani ya wapi unapatikana.
 
Toka lini gest aliepanga chumba akiondoka anaulizwa aliekuja nae kama vitu vyake vimetimia? Walau ingeingia akili kama huyo mwanamke anaondoka ndio aamshwe mwenyeji wake aulizwe swali kama hilo
Utoke sa2 asubuh mhudumu aanze kuangaika na wewe? Kajaribu Leo uchukue chumba halafu kurupuka sa9 za usiku kama utatoka kiurahisi.
 
Askari Polisi jijini Arusha amefariki dunia katika mazingira ya utata katika nyumba ya kulala wageni ya Mrina shine iliyopo makao mapya jijini hapa.

Taarifa za awali kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye aliomba jina Lake lihifadhiwe zimedai kuwa, Saiba aliingia katika nyumba hiyo majira ya saa sita usiku akiwa na mwanamke mmoja ambaye jina lake hakufahamka mara moja .

Aliieleza kuwa marehemu aliandikisha katika kitabu cha wageni na kupewa chumba namba tano na kisha kuingia katika chumba hicho akiwa na mwanamke huyo, kibegi kidogo cha mgongoni na radio ya mawasiliano aliyokuwa ameshika mkononi.

Alisema majira ya saa 9 usiku askari huyo alitoka ndani ya chumba hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa amelala fofofo. Aliendelea kudai kuwa marehemu alikwenda nyuma ya nyumba hiyo na kuruka geti la nyumba hiyo akiwa na lengo la kumtoroka mwanamke huyo, ndipo alipoangukia kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.

Hata hivyo baada ya askari polisi kufika walipekua begi la marehemu na kukuta chupa ya bia moja,chips ,radio ya mawasiliano simu mbili ikiwemo ya huyo mwanamke pamoja na vitu vingine.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani hapa ,Justin Masejo ili kuzungumzia tukio hilo ziligonga mwamba mara baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kutopokelewa.

Mwili wa marehemu Stewart unatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao Bukoba kwa ajili ya maziko, baada ya kufanyiwa uchunguzi.

Mwenyezi mungu alilaze mahala pema peponi roho ya marehemu Stewart, Amen!
Kwa hiyo Mr. Afwande alikuwa kapita na simu ya huyo dada halafu akawa anamtoroka kukwepa "tozo" ya mbususu?
 
Yaani utoroke Nia yako usitambulike ni wa wapi? Asa halafu ukajitambulishe Kwa mlinzi mie ni Askari si tayari ushauza ramani ya wapi unapatikana.
Kwanini asitambulike wakati amepanga chumba na jina ameandikisha? Kumbuka aliepanga chumba ni Mwanaume na sio Mwanamke hata kama aliongopa jina wahudumu waliona Askari polisi ameingia na Mwanamke
 
Taarifa zinadai kwamba baada ya mlinzi kusikia kishindo alienda katika geti hilo na kumkuta askari huyo akiwa ameanguka chini akivuja damu nyingi kwenye paji la uso na kutoa taarifa polisi ambapo majira ya alfajiri polisi wenzake walifika na kukuta amepotez maisha.
Huyo ni askari mwenzao wameitikia wito alfajiri, je raia hoehae
 
Utoke sa2 asubuh mhudumu aanze kuangaika na wewe? Kajaribu Leo uchukue chumba halafu kurupuka sa9 za usiku kama utatoka kiurahisi.
Mkuu unatoka tu kwani unafikiri hao Malaya uwa wanatoka muda gani? Tena kwa yeye Askari polisi ndio akuna hata shida ya kujieleza
Wangesema amefumaniwa katika harakati za kutoroka hiyo ingeingia akilini lakini kwa maelezo hayo Kuna utata na Kuna watu itabidi wawajibike kwa kifo hicho
 
Back
Top Bottom