Askari polisi adaiwa kufia gesti akimtoroka mwanamke, Polisi Watoa tamko

Daaah niabu aisee imagine ni ndugu yako wa damu [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Bora ingekuwa fresh kiporo 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Dah! Huo msiba ufanyikie hapo hapo gest, nyumbani unapelekaje msiba kama huo
 
Intelejensia inaonyesha huyu polisi
1. Ni mzinzi
2. Ni mwizi
3. Ni mlevi
4. Ni mzembe
Watu wenye sifa hizi wanaruhusiwa kuwepo jeshini.
Hivi polisi hawana intelejensia Kama Ile ya geshi. (Military intelligence)?
 
Watasema akiwa katika harakati za kutimiza majukumu yake aliangukia kitu chenye ncha kali
 
Baada ya kuona hili jambo la kwanza kujiuliza ni vipi yote yametokea ? Ni kachero je kuruka ukuta ndiyo ukachero ?

Kukimbia na simu ya kimada je ? Hii yaweza kuwa ni mbinu ya kikachero kwenda kufuatilia taarifa zake au sio jamani ?

Je hili la kubeba na chipsi kunako begi ?

Finally nimekaa na makachero wabobezi wa mambo haya na wamehitimisha hivi .

Ni likibaka limoja ndani ya jeshi kwanza lililewa na pia halikuwa na hela ya kulipa likaona bora litoroke ila haikuwa rahisi kihivyo likaishia kupoteza maisha .

Sasa wito wa makachero wabobezi ni upi ?
Litangulie mbele ya haki sisi ni wapitaji hapa duniani .
 
Dah apumzike kwa amani kamanda wetu. Alipata huduma na hakutaka kulipia. Mazoea mabaya sana
 
Hakuna utata wowote!, Ni pombe zake tu ndio zilikuwa zimemtuma kutoroka kwa kuruka ukuta!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
The whole thing looks framed up, there are signs of personal vendetta. Ila kwa haya ma-idiot litapita tu.
 
Dah. Yani kala mzigo bure, kaiba na simu, akaangalia mezani akakuta kiepe, na chenyewe akapita nacho. Si angemwachia huyo mwanamke ale angalau apooze hasira za kudhulumiwa? daah, watu wengine hawana huruma kabisa.

Sasa kaenda kuruka geti, kafa. Kiepe hajala, simu hajauza, hela hajapata, na dhambi katenda, tena katenda dhambi siku ya kufa!

Mwenyezi mungu amsamehe dhambi zake, ampunguzie na adhabu ya kaburi, aipumzishe roho yake mahala pema peponi, amen [emoji1488]

Jamani, tuacheni roho mbayaa, hatujui siku wala saa.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…