Auz
JF-Expert Member
- Apr 6, 2016
- 13,539
- 11,419
WaTz tuache ulimbukeni wa madaraka, hali nzuri tulizonazo. Vyote hivyo ni kwa huduma kwa WaTz wenzetu. Tufuate sheria, tufuate katiba!Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dares Salaam lilipokea taarifa kuwa tarehe 29/11/2023, Saa sita usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni askari wawili walimjeruhi kwa risasi mu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 mlinzi binafsi wa Bar itwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.
Jeshi la Polisi tayari limewakamata askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka Kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria kiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi.
View attachment 2828811
View attachment 2828814
Video hizi zifuatazo chini zinaonesha namna hali ilivyokuwa kabla ya tukio la Askari kufyatua risasi
View attachment 2828866
View attachment 2828868
View attachment 2828869
Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app