KERO Askari wa Barabarani Arusha wanatunyanyasa sisi madereva Bajaj

KERO Askari wa Barabarani Arusha wanatunyanyasa sisi madereva Bajaj

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Arusha. Kero yangu inahusu baadhi ya askari wa usalama barabarani (trafiki) ambao wanatunyanyasa sisi madereva wa bajaji. Kuna maeneo ya Arusha mjini ambayo haturuhusiwi kuingia, licha ya kuwa maeneo hayo ndiyo yenye fursa nyingi za kupata riziki.

Tukiingia maeneo hayo na kukamatwa, tunapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) na kutozwa faini zisizo na viwango maalumu, ambazo wakati mwingine hufikia hadi Shilingi 120,000, ilhali kwa mujibu wa tunavyofahamu, faini inayotakiwa ni Shilingi 10,000. Wakati mwingine tunazuiliwa kituoni hadi saa mbili usiku, kisha tunalazimika kutoa Shilingi 20,000 ili tuachiliwe.

Kwa kweli, hali hii imekuwa kero kubwa kwetu. Baadhi ya askari hao, pamoja na watu wanaoshirikiana nao, wanatufanya tushindwe kufanya kazi zetu kwa uhuru na kwa amani. Tunaona kana kwamba tumegeuzwa chanzo cha mapato yao badala ya kutendewa kwa mujibu wa sheria.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie malalamiko haya, zichunguze mwenendo wa askari wanaohusika na kuhakikisha kuwa tunatendewa kwa haki. Sisi ni madereva tunaotegemea kazi hii kujipatia kipato na kuhudumia familia zetu, hivyo tunaomba hatua zichukuliwe ili tuweze kufanya kazi zetu bila vitisho, usumbufu au madai ya fedha yasiyoeleweka.
 
Bajaji mjitathmini. Mnakera sana barabarani.
 
Makonda analijua hilo?
1915.jpg
 
Back
Top Bottom