Maneno mazito yenye busara kwa awamu ya sita wayasome na kuelewa kuhusu uongozi wa nchi kwa kufuata katiba.
Mazingira ya kusitisha kufuata Katiba na taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kusitisha kufuata Katiba ni kama ifuatavyo ilivyotamkwa ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni :
_________________________________________________________________
26
Madaraka ya
kutangaza hali
ya hatari
Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
32.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali ya hatari katika
Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.
(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo.
(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita;
au
(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri ya Muungano
inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita;
au
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii au kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama;
au
(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee;
au
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au la baa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemu ya jamii katika Jamhuri ya Muungano;
au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio kwa nchi.
(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania bara nzima au Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa Bunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais.
(4) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti kuhusu nyakati na utaratibu ambao utawawezesha watu fulani wenye kusimamia utekelezaji wa mamlaka ya Serikali katika sehemu mahususi za Jamhuri ya Muungano kumuomba Rais kutumia
madaraka aliyopewa na ibara hii kuhusiana na yoyote kati ya sehemu hizo endapo katika sehemu hizi kunatokea yoyote kati
ya hali zilizotajwa katika aya ya (c), (d) na
(e) za ibara ndogo ya
(2) na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemu hizo, na pia kwa ajili
ya kufafanua utekelezaji wa mamlaka ya Serikali wakati wa hali
ya hatari.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
27
(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais kwa mujibu wa ibara hii litakoma kutumika-
(a) iwapo litafutwa na Rais;
(b) endapo zitapita siku kumi na nne tangu tangazo
lilipotolewa kabla ya kupitishwa azimio lililotajwa
katika ibara ndogo ya (3);
(c) baada ya kupita muda wa miezi sita tangu tangazo hilo lilipotolewa; isipokuwa kwamba kikao cha Bunge cha weza, kabla ya muda wa miezi sita kupita, kuongeza mara kwa mara muda wa tangazo hilo kutumika kwa vipindi vya miezi mingine sita kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wa kikao hicho wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote;
(d) wakati wowote ambapo mkutano wa Bunge utalitengua tangazo hilo kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za wajumbe waiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote.
(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashaka juu ya ufafanuzi au utekelezaji wa masharti ya ibara hii, masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge na ya sheria nyingine yoyote, inayohusu utangazaji wa hali ya hatari kama ilivyotajwa katika ibara hii, yatatumika tu katika sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambapo hali hiyo ya hatari imetangazwa.