Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Mabadiliko pekee ya katiba wanayotaka CCM ni kumfanya Magu atawale mileleUnajua maana ya upinzani wa kisiasa!!?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mabadiliko pekee ya katiba wanayotaka CCM ni kumfanya Magu atawale mileleUnajua maana ya upinzani wa kisiasa!!?
Lissu katumia Akili ya kawaida,hujamuelewaKumbe Askofu ni mpinzani wa kisiasa....
Huyu siyo mtumishi ni mhuni fulani tu. Hakuna askofu wa sampuli hiyo.tatizo lako mtumishi ni moja tu, husifu & kuabudu mungu wa Chato!.
Atawachungia wapi hao kondoo na kanisa lilimfukuza?Huyu Askofu ndiyo ali organize matembezi ya hiyari kudai Katiba mpya?
Nadhani angejikita kwenye kuchunga kondoo wa bwana tu, utawala uliopo huwa haupendi kufosiwa kufanya mambo. Mambo yanafanyika pale mwenye nyumba atakapoamua.
Hata kama aliwahaidi Katiba mpya -mpaka apende mwenyewe
Milioni 50 kila Kijiji - mpaka apende
Nyongeza ya mishahara - mpaka apende
You mention...
Kumbe jiwe anakubaliana na akina Ngamia, Kessy, Msukuma....?
View attachment 1703071
View attachment 1703070
View attachment 1703379
====
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.
Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.
Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.
LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021
Zaidi, soma:
Askofu Mwamakula azungumzia "matembezi ya hiyari"!
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA "MATEMBEZI YA HIYARI" Baada ya Askofu Mwamakula kutangaza kuwa 'ataingia barabarani' kuongoza "Matembezi ya Hiyari" kwa nchi nzima ili kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya, watu wengi wametaka kujua zaidi kuhusiana...www.jamiiforums.com
Ndio anajiita kwa kuwa hana kanisa, alitimuliwa MoravianEti "Anayejiita Askofu" , Mambosasa kiburi cha uzima na madaraka kitakupeleka pabaya sana
Hata kama ndiyo tumeharibikiwa ila huyo jamaa hapana kwa hiyo nafasiMambosasa katika uzuzu wake wa kuusaka uIGP
Yamefanikiwaje wakati alie yaanzisha yuko nyuma ya nondo na nyie mliopaswa kumuunga mkono barabarani mko nyuma ya keyboardMpaka muda huu maandamano ya Askofu Mwamakula yamefanikiwa
Hapa ndo makamanda wa malalamiko hua siwaelewi. Mi nadhani wawe wanawaweka wazi hawa waanzisha maandamano kwamba tutakupa support ila ya mitandaoni tu, barabarani hatuingii. Huenda itawafanya hawa waanzisha maandamano watuluze vichwaSasa kama amekamatwa si muandamane mwende mkamtowe.
Si mlimuahidi kwamba mko nae bega kwa bega.
Nacho fTafadhari naombeni CV yake. Kazaliwa wapi, kasoma wapi na ana elimu kiasi gani. Naona mtandaoni siioni CV iliyoshiba ila atakuwa ana akili sio kama kina Askofu Rashid
Nachofahamu Askofu Mwamakulah alisoma Azania High school. Na alikuwa mchapuo wa PCM.Tafadhari naombeni CV yake. Kazaliwa wapi, kasoma wapi na ana elimu kiasi gani. Naona mtandaoni siioni CV iliyoshiba ila atakuwa ana akili sio kama kina Askofu Rashid
Mkuu Watanzania nawajua, ni waoga kupitiliza. Kile kizazi cha akina Samwel Sitta hakipo, fikiria mtu anahamasisha mgomo hadi kufikia Mwl Nyerere kutoka Ikulu kwenda Chuo Kikuu na Kumchapa viboko.Watu wenye mawazo kama yako ndo wamefanya watanzania kuchezewa kama watoto wadogo nasi kukubali kufyata mkia! Kazi ya mchungaji ni pamoja na kulinda usalama wa kondoo wake! Watanzania wameuawa, wamepigwa, wamebambikiwa kesi za uongo, nasi tuko kimya tunaendelea kutoa macho tu na kuandika kama uliyoandika hapa!