PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
mambo ya ajabu haya unayoandika hapa.
Kwani Gwajima kaeleza nini, au hukumsikiliza kwenye habari yake ya mwanzo?
Sasa unaweka 'spin' gani tena hapa!
 
Useless!
Hata Pascal ni mtu wa kurejeshea hapa?
Kama ni uchambuzi ulionuia kuufanya ni wa hovyo!
Utamwondoa vipi Rais, ambaye ndiye anateua watu anaoona wanafaa kuongoza vyombo hivyo unavyo vipa uhusika wa matendo ya hovyo, bila ya uhusika wake mwenyewe?

Hukuelewa alichozungumza Gwajima katika 'press conference' yake?
 
Yale maneno 'no reform no election' yanasahaulika taratibu.
Hilo lisikupe faraja.
Endelea kuwa na matumaini hayo, hata kama hayana msaada wowote kwenu.

Haya yote mmeyatengeneza wenyewe; kwa bahati mbaya sasa hamna uwezo wa kuyazuia yasiwafyekelee mbali.
 
Sidhani kama hoja ni useless;

Ila nadhani umejibu kwa haraka sana bila kufanya tafakuri.

Gwajima alimuunganisha wazi Rais na Utekaji - tena katika utaratibu ulio nje ya vyombo vya ulinzi ma usalama (yaani kuna kikundi "fulani" kinachopokea maelekezo moja kwa moja kutoka "juu" ambacho kinafanya kazi kwa utaratibu ulio nje ya vyombo vyetu"

Hoja ya namna hii inamaanisha Rais yeye mwenyewe kwanza ana kundi la utekaji nje ya mifumo ilopitishwa na Bunge na ametoa order ya kumteka mtu kama Soka, Kumshambulia Kitima Nk... kufikiri hivi itakuwa ni kumfault Rais kusiko na maana. Hatuwezi kujenga nchi kwa namna hii. Askofu Gwajima anajua hii hoja sio sahihi hata kidogo.... yaweza kuwa alikuwa na hoja nyingine lakini aliwasilisha kitu kingine... nadhani hoja ingekuwa ni Accountability ya Rais kwa wananchi kuhusu yanayoendelea?? Ni hatua ganinanachukua?? Hii ni hoja ya msingi zaidi kuliko kuja na hoja zisizoweza kuthibitika. Na ambazo tu zitasababisha watu wakupelekee moto bila sababu.
 
Ukisoma comments za wanaompinga gwajiboy unagundua kuwa nchi hii ina tabaka bovu sana lililo katika mamlaka ya nchi.


Mungu aionee huruma nchi yetu.
Ni tabaka lilojengwa khasa kati ya 2005 na 2015.

Miaka 10 kujenga nchi ya wapigaji si midogo.

Ndo tabaka lilounda mfumo wa Kleptokrasia na limejiaminisha kuwa na nguvu.

Lakini sio kweli hizo ni ndoto zao tu.

Huu ndo wakati wa watanzania wenye uzalendo kujitokeza kulishinda hili tabaka lenye nia ovu kwa Tanzania, maana huko mbele kuna hatari inokuja tukaongozwa na wahuni watupu.

Mchungaji Gwajima aungwe mkono kwa nguvu zote.
 
Huwa sibahatishi, kwa sababu maswala ya namna hii siyo ya utani utani.
Nilicho andika hapo juu kinabaki kama kilivyo wasilishwa. Wewe weka tafsiri inayokufaa, mimi siioni hivyo.
 
Mwenye akili kashaelewa
 
Tuongee na m23 watusaidie kwa kweli. Ile top cream ya administrators ni wahuni watupu, wasioamini katika falsafa yoyote ya kulikwamua taifa zaidi ya kuogofya wananchi ili wao waneemeke.

Akili ya ku-utilize resources hakuna kabisa. Hii nchi sio masikini.
 
Njia hii yatosha kwa kuanzia.

Tumefungua njia kwa maombi ya siku 7.
 
Kwahiyo ww unaona hilo haliwezekani au sio
 
Hivi ni kwamba unadhani tunaona Gwajima anakosea? Gwajima ameenda moja kwa moja kwenye mzizi wa tatizo. Huenda hutaki rais ahusishwe kwa mantiki ya kwamba ni mtakatifu wakati uhalisia unakataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…