Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Nina amini scenario kubwa tatu

1.Kuwa ni kweli anatishiwa maisha kwa sasa au bado ana hofu sababu hana ulinzi tena kama mgombea na waliofanya jaribio la kumuua bado hawajulikani walipo na hali hiyo pia inahatarisha maisha yake...

2. Kutokana na kampeni inawezekana katumia saving zake zote na Chama kina hali mbaya...kwa sasa Lissu sio Mbunge na CDM haina ruzuku kulipa gharama za case zinazomkabili lkn pia kuendesha chama...hivyo anatafuta namna ya kupata uhamisho kwenda Nje ili aweze kusustain maisha yake na familia yake.

3.Ni njia anayotumia kuendelea kuweka msisitizo kwa mataifa ya Ulaya kufuatilia mwenendo wa siasa Nchini na ikiwezekana kuwawajibisha watu wanaotuhumiwa kukiuka haki za binadamu na kumpora ushindi na hivyo anatumia hicho kigezo kuspeed up process.

Ni mawazo yangu
 
Hukuamini hivyo hivyo aliposema anafuatiliwa na watu wasiojulikana,akanusurika kifo!
Hukuamini pia pale Ben saanane aliposema anatishwa!Kweli kapotezwa!

Hawa ni watanzania!
 
Lissu akiguswa hata na unyoya safari hii! , tusije kulaumiana huko mbele ya Safari maana maandiko ya Mungu yanasema Kisasi ni haki, Kisasi kitalipwa tu!

Ila KATIKA WATU WAPUUZI HUMU WEWE NI NAMBA MBOJA. SIJUI BANGI. NI NINI HASA kinakusibu mana Kama Siasa huna lolote. Nini hasa tatizo lako. Mana umeamua kuaachana kabisa na reasoning Sasa unaamua kuonyesha ujinga wako na hamu za kumwaga damu. Jitokeze tu Jinga wewe.
 
Kweli mkuu ukiangalia mtu anafurahi kabisa huku ata net kafungiwa anatumia VPN
 
Hukuamini hivyo hivyo aliposema anafuatiliwa na watu wasiojulikana,akanusurika kifo!
Hukuamini pia pale Ben saanane aliposema anatishwa!Kweli kapotezwa!

Hawa ni watanzania!

What made him came back after all? He knew his safety is in jeopardy!
Mmemuangusha sana kwa kutoandamana. Alitegemea ndio pakutokeaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
What made him came back after all? He knew his safety is in jeopardy!
Mmemuangusha sana kwa kutoandamana. Alitegemea ndio pakutokeaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Aliomba ulinzi kwa jeshi la polisi na ni wajibu wa jeshi la polisi kumlinda!Kweli amelindwa wakati wote wa kampeni,sasa mnaona haitoshi mtu huyo aishi!Mmeanza kumtisha tena kwasababu mnajua amebaki raia wa kawaida na si mgombea tena!
Haya mnayofanya mnazidi kubomoa umoja wa kitaifa!
Mimi leo nikimuta kada wa CCM anakaribia kukata roho na anahitaji msaada,wallah namuacha na kuendelea na mambo yangu!Naanzaje kumsaidia wakati yawezekana ndio wewe au yule anayekejeli maisha ya mtanzania mwenzake hapa jukwaani?
 

..uchaguzi umekwisha, hivyo TL hana ulinzi wa Polisi tena.

..usalama wa TL uko mashakani kwasababu waliomshambulia Sept 7 2017 bado hawajakamatwa.
 
Baada ya Tundu Lissu Kuukosa 'Urais' ambao unajulikana alikuwa akipewa Ushirikiano wote na nchi baadhi ya Ulaya ( zenye Uwezo na Nguvu ) leo hii anataka kuubadili Upepo wa Kushindwa Kwake kwa kusema kuwa anataka 'Kudhuriwa' na wale wanaoitwa 'Maadui' zake wa Kisisasa hapa nchini Tanzania.

Kuna 'Hoja' zingine ukizisikia tena kutoka kwa Watu wenye 'dhamana' ya 'Kiimani' kwa Wanakondoo wa Mwenyezi Mungu unaanza kuamini kuwa huenda Viongozi wa Imani ( Dini ) nchini Tanzania wameisha na sasa wamebaki Makasisi Wanafiki pekee. Hivi kwa akili ya kawaida tu 'timing' nzuri ya 'Kudhuriwa' kwa Mtani wangu kutoka Singida Tundu Lissu ilikuwa ni kabla ya Kampeni alipokuja au wakati wa Kampeni au hivi baada ya Uchaguzi Mkuu?

Hivi wale mnaomuamini huyu Askofu na 'Kumtetea' Tundu Lissu leo hii mmesahau kuwa Kuna 'Kesi' zake kadhaa Mahakamani ambazo Kisheria anatakiwa Kuzikabili? Ni 'Mpumbavu' tu pekee ndiyo hatojua kuwa huu ni 'Ujanja' tu wa Tundu Lissu kutaka 'Kukimbia' nchi hadi tena mwaka 2025 na pia 'Kuzikwepa' hizi 'Kesi' zake huko Mahakamani.

Nakumbuka hapa hapa JF zaidi ya mara Saba (7) nilishauri Tundu Lissu 'asirejee' Kwanza nchini kutokana na kwamba bado 'upepo' wa Kisiasa na Kiusalama haukuwa mzuri Kwake ila kuna 'Wapuuzi' kadhaa hawakunielewa na kunipinga ila leo ( kwa sasa ) nadhani mtaanza Kunielewa na hata Kuwaelewa wale wengine ambao nao walishauri kama Mimi.

GENTAMYCINE bado nasisitiza nitakuwa wa mwisho 'Kuamini' kuwa 'Maadui' wa Mtani wangu Tundu Lissu ni Serikali, CCM na Watu wa 'System' tu.
 
..uchaguzi umekwisha, hivyo TL hana ulinzi wa Polisi tena.

..usalama wa TL uko mashakani kwasababu waliomshambulia Sept 7 2017 bado hawajakamatwa.
Kama haamini kuwa Tanzania ni nchi salama kwa yeye kuishi, hakuwa na sababu ya kurudi. Vilevile hakuwa na sababu ya kuamasisha watu kuandamana. Anavyojali usalama wake anatakiwa kujali pia usalama wa wale anaowahamasisha kuandamana.
 
Uncle aende tu...
Kila anayosema huwa anajiongezea potential lawsuits. (kumbuka hata akizishinda, kesi ni mizigo. Na bado anazo kama nne hivi).
Hili sasa litageuzwa Defamation kwa jeshi la polisi na watu wengine 'maarufu', including maneno mengine aliyosema kwenye kampeni na enzi za misele yake kipindi kile cha matibabu. Hao waliomtonya hawatathubutu ku-testify, af itaonekana nia yake mbaya.
As long as waliopo madarakani wapo, Wana sehemu nyingi za kupita naye.
Mjomba ana akili sana ila, mchezo wa siasa unahitaji atleast boderline narcissism; bahati mbaya yeye hana.
Maana, hawajaanza na familia yake...
Wanaomsapoti watabaki JF na twitter wakilalamika, af Yeye akichakaa kwa ajili ya wabongo ambao wameamua kuweka moyoni walivyotapeliwa, na kupotezea.
 
Kama haamini kuwa Tanzania ni nchi salama kwa yeye kuishi, hakuwa na sababu ya kurudi. Vilevile hakuwa na sababu ya kuamasisha watu kuandamana. Anavyojali usalama wake anatakiwa kujali pia usalama wa wale anaowahamasisha kuandamana.

..alirudi muda muda mchache kabla ya uchaguzi kwasababu sheria inalazimisha wagombea Uraisi wapewe ulinzi.

..pia aliamini angeshinda uchaguzi, na kama ndoto yake ya kushinda Uraisi ingetimia basi angekuwa na ulinzi maisha yake yote.

..alihamasisha maandamano ya AMANI, hivyo alijali na alizingatia usalama wa aliowahamasisha kuandamana.

vilevile wakati wa kampeni alikuwa akiviasa vyombo vya ulinzi kutokutumia silaha zao dhdi ya wananchi pale watakapoamua kuandamana kwa AMANI.
 
Wamtumainio bwana ni kama mlima sayuni hautatikisa kamwe, maadui wa lissu watakuwa Madui wa Mungu
 
Tatizo sio kuogopa. Ujinga nikumtishia uhai wake bila ya sababu kwahiyo mimi kukutishia kifo kwanjia ninayoijua mimi inamaana hutaogopa wakati ninanguvu zakukushinda kwa njia yoyote?
kwan kauli zake zake alikuwa akisemaje ,yupo tayari kwa lolote. Sasa lolote Lina kuja anakimbia, mimi sio mfuasi wa chama chochote. hunikut naongelea siasa. Ila huu upumbavu wa kuwapeleka kingi raia haraf wew una lala mbele siupendi.

kama yeye anaogop, inakuwaje ana shawish raia wakaandaman kinyum na taratib huku akijua juna nguvu itatumika kuwatawanya , matokeo ya nguvu hizo zinajilukan Yeye anakuwa wapi muda huo, ubalozin.
 
Anakimbia kesi zake, amegundua sasa atabaki gerezani muda si mrefu,
Hakuna mtu wa kumuua mtu aliyekosa ushawishi kwa wananchi, alikuja kugombea akijua atalindwa na jamii za kimataifa kwa ajiri ya kisiasa, sasa siasa zimeisha na kubaki kama raia ameanaza kutimka.
Alifikiri ataokota bingo hapa TZ 😁😁😁😁
 

Tundu Lissu aongea live toka ndani ya ubalozi wa Ujerumani ktk makazi ya balozi, jijini Dar es Salaam Tanzania
 
Kama hayo ni ya kweli basi washukuriwe hao wajerumani kwa kumpa hifadhi maana kwa kupuuza taarifa kama hizi kipindi cha nyuma alichakazwa na maharamia mvua ya risasi 32.

Kwa hakika ni heri ya beberu mthamini roho za watu lakini si mkoloni mweusi na vikundi vyake vya kishetani vyenye kiu isiyomithilika ya damu za binadamu wasiokuwa hata na hatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…