Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Mkuu, mshaurini Lissu kwamba aache vituko na maigizo!

Hivi si ni Lissu huyu huyu wakati wa kampeni akikuwa anashuka kwenye gari na kutunishiana misuli na Polisi huku akiwaambia nifanyeni chochote mnachotaka?

Si ni Lissu huyu huyu alipowasili toka Ubelgiji alisema haogopi chochote maana hana cha kupoteza? Au alifikir ameshakuwa Rais?

Mwambieni jamaa yenu aache woga na vituko, arudi nyumbani akakae na mkewe, hapo Ubalozini atamnyima hata mkewe haki yake ya ndoa.

Au kama amezoea maisha ya Ulaya mwambieni aombe vibali akaishi huko, aombe vibali kwa kufuata sheria siyo kwa hivyo vituko vyake.
Nasikia we we ni mmoja wa wauaji
 
AMEANDIKA:

BABA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA.

USALAMA WA MAISHA YA LISSU UKO HATARINI, AKIMBILIA KUPATA HIFADHI KATIKA UBALOZI WA UJERUMANI JIJINI DAR ES SALAAM!

Jana tarehe 5 Novemba 2020 nilizungumza na aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye anaishi Uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam. Tulikubaliana kuwa mimi kama Askofu na Mshauri wake katika Masuala ya Kiroho, niwajulishe Umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla kuhusu hali ya Usalama ya Mheshimiwa Lissu.

Kupitia mazungumzo yale, Mheshimiwa Lissu alieleza kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, alianza kutishiwa maisha yake. Baada ya vitisho kuzidi kuongezeka, Mheshimiwa Lissu alipokea pia taarifa kutoka kwa 'wasamalia wema' waliomtahadharisha kuwa kulikuwa na 'maelekezo maalum' ya kutaka 'vijana wamalizane kabisa na Lissu' safari hii!

Baada ya kutafakari kwa kina taarifa za vitisho hivyo pamoja na taarifa kutoka kwa 'wasamalia wema', Mheshimiwa Lissu aliamua kwenda kutafuta hifadhi ya muda sehemu nyingine tofauti na nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hatua ambayo ilionekana kama ni kuhatarisha usalama wa maisha ya watu wengine. Ndipo alipoamua kutafuta hifadhi katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam siku chache. Siku alipokwenda Ubalozini, alipowasili na akiwa nje ya Ubalozi akisubiri taratibu za Ubalozi pale Umoja House, Polisi waliokuwa katika magari mawili walifika pale Ubalozini na kumkamata na kwenda naye Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam. Ndipo Maafisa wa Ubalozi waliamua kumfuatilia Mheshimiwa Lissu kwa nyuma na kusubiria pale Central, jambo ambalo liliwafanya Polisi waamue kumuachia kwa kuogopa kelele zaidi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

Mheshimiwa Lissu alinieleza kuwa Maafisa wa Ubalozi wameendelea kuwasiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Mheshimiwa Palamagamba Kabudi kuhusu hifadhi yake, lakini Serikali hadi kufikia jana tarehe 5 Novemba 2020, Serikali ya Tanzania ilikuwa inasita kutoa kibali kwa Ubalozi unaoshughulikia masuala ya Lissu kwa kisingizio kuwa Lissu aombe ruhusa ya Kimahakama kwa kuwa anazo kesi Mahakamani. Hoja ya Serikali ilionekana kutokuzingatia au kutokujali tishio dhidi ya uhai wa Mheshimiwa Lissu.

Katika mazingira yaliyopo, tunaiomba na kuishauri Serikali itoe kauli kuhusu kumhakikishia usalama Mheshimiwa Lissu. Kukaa kimya kwa Serikali pasipo kutoa hakikisho lo lote la usalama kwa Mheshimiwa Lissu kutapelekea watu kufikiri na kuamini kuwa Serikali inahusika au iko nyuma ya vitisho dhidi ya maisha ya Lissu.

Ikumbukwe kuwa miaka mitatu iliyopita, Mheshimiwa Lissu aliwahi kulalamika mara kadhaa kuwa kuna watu walikuwa wakimfuatilia na kuwa maisha yake yalikuwa hatarini na haikupita muda mrefu akashambuliwa na risasi mchana jijini Dodoma na hadi sasa hakuna taarifa za kukamatwa kwa mtu ye yote kutokana na tukio lile.

Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu hali halisi ya usalama wa Mheshimiwa Lissu katika mazingira ya sasa na baada ya kushauriana na wadau mbalimbali, imeonekana ni vema na ni hekima na usalama kwa Mheshimiwa Lissu kuendelea kuishi Uhamishoni katika Ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam hadi pale itakapoamriwa tena hapo baadaye. Kwa sasa Mheshimiwa Lissu pamoja na baadhi ya Wasaidizi wake wapo katika Ubalozi wa Ujerumani ambapo wanaendelea kupata hifadhi.

Ninaandika haya kama Askofu Mshauri wa Mheshimiwa Lissu ili Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa wapate ufahamu kuhusu yanayoendelewa kwa Mheshimiwa Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunatoa wito kwa wote walio nyuma ya mpango wa kutishia usalama wa maisha ya Mheshimiwa Lissu kwa kuelekeza, kufadhili, kutuma au kutekeleza mpango huo kuacha mara moja kwa kuwa mkono wa Mungu na ulinzi wake upo pamoja na watu wasiokuwa na hatia (Zaburi 35 na Zaburi 121). Tunasisitiza kuwa mpango wa kutaka kumdhuru Lissu ni uovu hivyo waache mara moja (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
kamanda Lisu tunakuombea mungu yupo pamoja na ww hao watakutisha lkn hawatashinda
 
Wakati anafanya kampeni kwa matusi na kejeli hakujua kuwa mwisho wake ni rais akiapishwa.Simuonei huruma na hana adabu.
 
Ila hili ni baya sana litakuwa na impact mbaya sana mbele ya jumuia za kimataifa na katika maswala ya kidplomasia,
Haya mambo wangekaa wakayamaliza humu humu ndani wenyewe kwa wenyewe kuliko hivi sasa kuexpose kila kitu kwa wakubwa wa dunia
 
Mbona swali na jibu tofauti kabisa?

Halafu mimi nimefurahi mno Biden kushinda kwasababu alikuwa mpinzani na inaonesha jinsi gani nchi za wenzetu zinavyojali democrasia.

Trump ni Rais aliyepo madarakani lakini hakutegemea jeshi, polisi, usalama wa taifa wala wakurugenzi ili wampitishe kwa njia haramu kama ilivyo huku kwetu.

Kazi ya polisi na vyombo vya dola sio kuhakikisha utawala uliopo kubaki madarakani bali wenzetu wanajitenga kabisa na siasa wao anayeshinda ndo boss wao.
Tanzania jwtzccm Polisiccm Uhamiajiccm magerezaccm mahakamaccm Msajiliccm NECCCM Tumeccm tbcccm ni vyombo binafsi vya CCM ndivyo huhakikisha CCM unatawala zaidi ya miaka 1000
 
Mkuu Lissu kwa sasa ni raia Kama raia wengine anapoona anatishiwa Kuna mamlaka zipo,,,,aende police aripoti na sio ubalozini ....
Polisiccm mahakamaccm ni mali binafsi za CCM kuna haki huko?
 
Ila hili ni baya sana litakuwa na impact mbaya sana mbele ya jumuia za kimataifa na katika maswala ya kidplomasia,
Haya mambo wangekaa wakayamaliza humu humu ndani wenyewe kwa wenyewe kuliko hivi sasa kuexpose kila kitu kwa wakubwa wa dunia
Mwambie polepole aache kuchua ushauri wa kishetani toka kwa akina cyprian Musiba na kuupeleka kwa mtukufu wanafanya vioja
 
Mkuu umesema mengi lakini mengine umeyaacha ambayo ni. Lisu huyu huyu ambae Mwenyezi Mungu amemnusuru kifo baada ya kupigwa risasi lukuki na watu wasiojulikana lakini wanaeleweka.

Na ni Lisu huyu huyu ambae serekali ilikataa kugharamia matibabu yake alipokuwa akitibiwa nnje ya nchi. Ni lisu huyu huyu ambae spika aliamua avuliwe ubunge kwa vile alikuwa yeye spika hafahamu Lisu aliko japo alikuwa kwenye tiba. Ni Lisu huyu huyu ambae alinyimwa mshahara wake wakati akitibiwa nnje ya nchi.

Ni lisu huyu huyu ambae amewafanya ccm na washirika wake wafanye dhambi kubwa ya uharamia wa kughushi matokeo ya uchaguzi kwa kuogopa mteule wao wa kiti cha uraisi kushindwa vibaya kwenye uchaguzi.
Lisu hakushindwa vibaya kwenye uchaguzi acha kupotosha hapo, lisu kapata kura nyingi mno lakini NECCCM Tumeccm na Polisiccm wakaunajisi kuubaka na kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani
 
Unaamini kwenye uchaguzi huu vibaraka na wanaowatuma wamepikea message clear bila chenga kutoka kwa umma wa watanzania?
Uchaguzi upi? Hakuna uchaguzi Tanzania umefanyika zaidi ya CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani
 
Arudi tu huko apewe asylum status aishi,atapewa flat ya kawaida tu na benefit za kumtosha na familia badae watamwambia jiongeze.tuliwai kukutana na waziri mkuu wa Lebanon enzi zake tukipiga box kawaida tu na story kibao akitupa itakua Lissu.huko Belgium ni kwa wale wasiojua tu ni kanchi masikini Europe wamejaa wanasiasa nguli toka DRC,Rwanda na vi nchi kibao vya Africa magharibi na ni wasomi wanagonga kifaransa kama kimakua itakua yeye,ana kazi nzito kwanza kujifunza lugha hiyo kabla kuanza ku-practise uwakili kule.
Yaani huyu ni utopolo kweli kweli,wako huku wanasiasa manguli hasa wapinzani toka Kenya,Uganda na mataifa kibao wanazurura tu hadithi zao ni hizo hizo kuonewa na watawala.lakini angalia maisha wanayoishi.
Hata akipata asylum baado ndio kwaanza km kaanza vidudu ana safari ndefu sana huko.
Umepatia, na huko ujerumani itabidi kwanza ajifunze kijerumani. Asifikiri wazungu wa mataifa mengine wote wanashobokea Kiingereza anachoringia kwa wabongo.
 
Tundu anatafuta kusikika tu wala hana la maana lolote, kama ni adui labda jamii yake inayo mzunguka yeye mwenyewe kwenye chama chake au amewahi kupindisha sheria kwa mtu kwenye makesi yao huko..nje na hivyo siamini serikali kuhangaika na mtu mdogo huyo,pia hua anapenda sifa tu kwenye mazungumzo yake mengi ambayo mala nyingi hayana lolote la maana
Wewe mwenyewe ni mbumbumbu juha zuzu kilaza mchawi mwenye roho mbaya unawezaje kujua mazungumzo ya maana wakati huna Ubongo umejaa chuki za kichawi tupu, huamini kuwa Serikali inahangaika na mtu Mdogo Mbona wewe mtu mkubwa upo busy kumuombea dua za kishetani?
 
Anaogopa sana maana anajua project yake ya kuleta fujo imekufa kifo cha mende. Waliokuwa wanamdanganya ndio Rais wamemuacha aandamane mwenyewe.
Anaanza kuleta hadithi za kusadikika. Akapambane mahakamani ili awe free bila kuwa na shida yoyote. Siamini kabisa kama kuna mtu anahangaika naye
Fujo zipi? Mahakamaccm kuna haki huko? Acheni roho mbaya za kuwabambikia kesi kesi wapinzani kwa njia haramu za kishetani
 
Lissu ameshaamua liwalo na liwe, yuko tayari kuiona Tanzania inateketea ili matakwa yake ya kisiasa yatimie. Too bad!
Amemaliza awamu yake ya kugombea, ana wafadhili tayari, ajiendee zake Belgium akaishi kwa amani.
 
Yan muuaji anataka kukuua anakupigia na sim kabisa kama point ilio fanya uo ubaloz wa ujeruman umpe hifadh ni huu basi Hao wazungu huenda ni wazungu Rangi tu ila akil ni gongowazi
 
Anakimbia kesi zake, amegundua sasa atabaki gerezani muda si mrefu,
Hakuna mtu wa kumuua mtu aliyekosa ushawishi kwa wananchi, alikuja kugombea akijua atalindwa na jamii za kimataifa kwa ajiri ya kisiasa, sasa siasa zimeisha na kubaki kama raia ameanaza kutimka.
Alifikiri ataokota bingo hapa TZ 😁😁😁😁
Hajakosa ushawishi kama angekuwa raia wa kawaida usingecheka kichawi kupanga mipango haramu ya kishetani dhidi yake, ungeamuacha Aishi kwa uhuru wake, hizo kesi za kuwabambikia watu imekuwa rungu lenu la uonevu, malipo ni hapa hapa Duniani mwisho wa ubaya ni Aibu
 
Lissu ameshaamua liwalo na liwe, yuko tayari kuiona Tanzania inateketea ili matakwa yake ya kisiasa yatimie. Too bad!
Amemaliza awamu yake ya kugombea, ana wafadhili tayari, ajiendee zake Belgium akaishi kwa amani.
Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi angefikaje Belgium?
 
Yan muuaji anataka kukuua anakupigia na sim kabisa kama point ilio fanya uo ubaloz wa ujeruman umpe hifadh ni huu basi Hao wazungu huenda ni wazungu Rangi tu ila akil ni gongowazi
Muuaji akiwatuma wauaji wakiona ni uonevu wapo wenye huruma watakupa taarifa tu , si kila wanaotumwa kuua wana roho mbaya na wapumbavu kama wewe
 
Muuaji akiwatuma wauaji wakiona ni uonevu wapo wenye huruma watakupa taarifa tu , si kila wanaotumwa kuua wana roho mbaya na wapumbavu kama wewe
Yan kumuua Tundulisu serikal ndio iangaike kiasa icho Tundulisu Ana Nini cha kumlinda
 
Back
Top Bottom