Askofu wa Katoliki Jimbo la Bukoba atetea uwepo wa kiti cha Rais Kanisani

Baba Askofu shukuru tu Wakatoliki hatuna utamaduni wa kubishana vinginevyo tungempopoa!
 
Shida ya viongozi wetu WA dini huwa hawasimamii wanachokiamini Bali wanazungumza Kwa woga, Rais anapokuwa kwenye ibada anakuwa chin ya kiongozi WA ibada na anafuata masharti ndio maana hata akienda msikitin lazma avue viatu,hawez kusali na viatu Kwa kuwa ni Rais,
 
Wewe Bavicha hovyo kabisa!
Nikuambie mara ngapi kuwa mimi sio Bavicha?
Nimejiunga na Chadema 1997 na kushiriki mkutano mkuu wa kumchagua Bob Makani kuwa mwenyekiti leo nitakuwaje Bavicha?
Ninauhakika mwaka huo lazima utakuwa hata mjini hujafika maana pengine unachunga mbuzi huko Nanjilinji kwenu.
🤣🤣
 
Kilaini anajulikana kwa kuegemea kwa watawala hadi kuna kipindi alidai mtu fulani alikuwa chaguo la Mungu, kwa hiyo siwezi kumshangaa kutetea jambo kama hilo. Mwenye mamlaka ndani ya hekalu ambaye anamwakilisha Mungu ni Kuhani Mkuu ambaye mbali na kukalia kiti maalumu, pia hata mavazi yake ni maalumu, halafu wanafuata makuhani wengine, watumishi hadi waumini wa kawaida. Atuwekee maandiko hapa kama ndani ya hekalu lililojengwa na mfalme Suleiman, mfalme alikuwa na kiti chake juu ya kiti cha Kuhani Mkuu ili aweze kutuaminisha kwamba ilikuwa sahihi rais kuingia na kiti chake kanisani.​
 
Huu mjadala hauna afya tangu lini walatoliki wakazuia mtu kwenda na kiti chake kama anataka, tumeona wengi tu wamaenda na viti vyao husisani watu wenye umri mkubwa.
 
Watanzania wengi ni watu wanaoweza kukubali kuibiwa kura mtu akachukua urais isivyo halali, halafu akachukua mic altare kanisani na kujiweka juu katika mimbari ya kanisa.

Akazuia mikutano ya kisiasa inayokubalika kikatiba. Akapiga risasi wapinzani.

Halafu wakakataa rais kuingia na kiti chake kanisani.

A very peculiar bunch.

Mkuu Kiranga hakuna mtu anayekubali kuibiwa kura, labda uweke sentensi yako vyema. Huyo mwizi wa kura huko altareni haingii kwa ridhaa ya aliowabia kura, bali madaraka yake yanaweza kumuingiza humo.

Anaweza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa maana anaagiza vyombo vya dola kuzuia hiyo mikutano, na hakuna mahakama zenye nguvu unazoweza kupeleka shtaka likaenda kinyume na utashi wa mwenye madaraka. Wapinzani wanaweza kupigwa risasi maana wapinzani hawana silaha, hivyo hawana la kufanya labda wajaribu kuingia msituni.

Hawakatai rais kuingia na kiti kanisani, bali wanakosoa rais kujipa utukufu usio na sababu yoyote, huku wakiwa wameingia madarakani kwa njia za wizi. Ingekuwa wamezuia rais kuingia na kiti kanisani wangeenda nje ya hilo kanisa na kuzuia.
 
Kilaini anajulikana kwa kuegemea kwa watawala hadi kuna kipindi alidai mtu fulani alikuwa chaguo la Mungu, kwa hiyo siwezi kumshangaa kutetea jambo kama hilo. Mwenye mamlaka ndani ya hekalu ambaye anamwakilisha Mungu ni Kuhani Mkuu ambaye mbali na kukalia kiti maalumu, pia hata mavazi yake ni maalumu, halafu wanafuata makuhani wengine, watumishi hadi waumini wa kawaida. Atuwekee maandiko hapa kama ndani ya hekalu lililojengwa na mfalme Suleiman, mfalme alikuwa na kiti chake juu ya kiti cha Kuhani Mkuu ili aweze kutuaminisha kwamba ilikuwa sahihi rais kuingia na kiti chake kanisani.​

Sikutegemea Kilaini kuongea tofauti na alichoongea.
 
Huu mjadala hauna afya tangu lini walatoliki wakazuia mtu kwenda na kiti chake kama anataka, tumeona wengi tu wamaenda na viti vyao husisani watu wenye umri mkubwa.
Usifananishe mtu wa kawaida anayebeba kiti kutoka nyumbani kwake na rais ambaye kiti chake kinabeba mamlaka......hii kwa maana nyingine ni kwamba rais anapeleka mamlaka yake hekaluni.
 
Narudia tena, kupeleka kiti ndani ya nyumba ya ibada ni ulimbukeni.

Mbona hakubeba hicho kiti kule kwenye basi la london?
 
Labda tungemuuliza huyo Baba Askofu ni lini alimchagua huyo Kiongozi anayemsema? Nijuavyo mimi Viongozi wa watu huchaguliwa hata Papa mwenyewe hupigiwa kura!
We kweli kijakazi, hujui kabisa km ulimchagua Samia? Tuna safari ndefu.
 
Nikuambie mara ngapi kuwa mimi sio Bavicha?
Nimejiunga na Chadema 1997 na kushiriki mkutano mkuu wa kumchagua Bob Makani kuwa mwenyekiti leo nitakuwaje Bavicha?
Ninauhakika mwaka huo lazima utakuwa hata mjini hujafika maana pengine unachunga mbuzi huko Nanjilinji kwenu.
🤣🤣
Wakati naogelea pale Kilimanjaro hotel Swimming pool Mwenyekiti wako Mbowe alikuwa Mlinzi pale BOT

Alikuwa anafungua mlango wa gari ya Gavana na wakati mwingine alitumwa kuwaleta Akina naniliu pale Swimming pool kiulinzi zaidi lakini baadae alivutiwa na kuvuta jiko kabisa

Hapo Ufipa st naweza kuongea na Mrangi tu ndio aliwahi kuja mjini akitokea Kondoa na basi la Siri Yako!
 
Labda tungemuuliza huyo Baba Askofu ni lini alimchagua huyo Kiongozi anayemsema? Nijuavyo mimi Viongozi wa watu huchaguliwa hata Papa mwenyewe hupigiwa kura!

mradi kaapishwa ndio anakuwa kiongozi
 
Wapendwa, nimeona mjadala juu ya kiti cha Rais na nikaonelea nitoe maelezo kidogo. Kanisa katika protocol zake inatambua na kuwaheshimu viongozi katika hadhi zao mbali mbali.

Hii protocol siyo ya sasa au jana ni ya miaka mingi. Rais ni kiongozi wa nchi hivyo hadhi yake ni hadhi ya nchi siyo yake binafsi.

Kwa sababu ya unyenyekevu wa viongozi wetu, kiti cha Rais kilikuwa kumebanwa kati ya mabenchi amezungukwa na masista na watu wengine. Kikawaida ingebidi sehemu moja ya kanisa benchi ziondolewe na kipangwe kiti chake rasmi na wapambe wake.

Hiyo ndiyo protocol halisi ya Mkuu wa Nchi anayekuja rasmi kwa dhifa ya kitaifa kama Rais wetu alivyokuja kwa kumbukumbu ya kitaifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hiyo si heshima kwake bali kwa nchi. Hewala si utumwa, tukikosa heshima kwa viongozi wetu tutakosa heshima hata nyumbani mwetu.

Tunatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa Taifa kuungana nasi katika ibada ya kumwombea Baba wa Taifa. Ni jambo jema sana.

Hata kanisani tunaheshimu siyo mtu binafsi lakini nafasi yake anayoishika. Kwa mfano Kardinali akiwa yeye haongozi ibada hakai pembeni na maaskofu wengine bali anapewa kiti maalumu kwa heshima yake. Unashukuru wat wa Itifaki ya Ikulu waliotuazima viti walau tukatoa heshima hiyo ndogo kwa mgeni wetu maalumu wa siku hiyo.

Ndugu zangu nimeona nitoe maelezo hayo kwa sababu niliona hoja inakua bila kutazama protocol za kanisa na heshima zake. Vile vile hakuna katazo kiti Fulani kisiingie kanisani ndiyo sababu unaona hata viti vya plastic vinavyotumika sehemu nyingine vinawekwa kanisani watu wakiwa wengi.

Nachukua fursa hii kuwashukuru waamini wa Bukoba Kanisa Kuu na parokia Jirani kwa kuungana nasi kwa wingi kumwombea Baba wa taifa. Mungu awabariki.

Askofu Method Kilaini
Baba Askofu umejichanganya.
Ile 80 milioni ulishairudisha?
 
Ulishatwambia kwamba Kikwete alikuwa chaguo la Mungu.Kwenye mgao wa ESCROW napo ukapiga.
 
Back
Top Bottom