Hata nami sikuona sababu ya kulalamikia hilo jambo, japo napingana na sababu alizotoa Askofu jimbo la Bukoba.
Naona angetembea na sababu za kiroho jibu lake lilikuwa jepesi sana, badala ya kuhangaika kutafuta sababu za ulimwengu mpaka akajichanganya.
Chanzo cha haya ni pale maoni yanapotolewa na mwanasiasa, kisha wafuasi wake/chama chake kuyabeba bila kujiuliza kama lililosemwa na kiongozi wao lina mantiki au hapana.
Kwanza, haya mambo ya kupigania vya ulimwengu huu yanatoka kwa mafundisho ya nani? sikumbuki wapi Yesu Kristu kwenye maandiko aliwahi kufundisha hilo jambo.
Zaidi, maandiko yanataka tuheshimu mamlaka zilizo juu yetu, sasa kama mamlaka imeamua kwenda na kiti chake kanisani, mnagoma ili iweje? kufanya hivyo sio kwenda kinyume na maandiko?
Kwa mtazamo wangu, Lema alikosea kwenye hili, nae kwa ushawishi wake, akawaponza wengi walioamua kuhukumu hili jambo bila kutumia fikra zao.