Askofu wa Katoliki Jimbo la Bukoba atetea uwepo wa kiti cha Rais Kanisani

Sawa. Lakini sehemu zote walizofanya mabadiliko kwani waliofanya mabadiliko walikuwa na dola?

Uko sahihi, hata huko haikuwa usiku mmoja, ni baada ya kufanyiwa uhuni kwa muda mrefu ndio wakafikia hatua ya machafuko. Hatuko mbali na huko kaka.
 
Bora hata mamlaka ya Samia imebeba kiti tu. JPM alifikia hatua ya kuwakejeli maaskofu akiwa amesimama pale pale wanapoendeshea misa zao!!.

Bora Samia hajasikika akijibishana na mamlaka za kidini, JPM alijiandaa akaenda na vifungu vya Biblia vya kuwashambulia maaskofu akiwa amesimama katika altare wanazotumia kuongozea misa kila Jumapili!;

Hali kwa ujumla haikuwa nzuri.
 
Chuki inaondoa uwezo wa kufikiri.

Unacho kiona wewe, hawawezi kuiona kwasababu wamejitia upofu
Wheelchail na hata viti vya kawaida vimeruhusiwa hata misikitini kwa watu wenye uremavu na kwa wazee wenye matatizo ya viungo.

Lakini kwajinsi wananzengo walivyo komalia kiti, hata angekua na jipu kwenye Tako, akamua kwenda na mto Ili iwe nafuu kwake kukalia benchi, Bado ingekua nongwa TU.
 
Kilaini alikula Mlungula, 40M za Tegeta Escrow, Askofu Mpigaji
 
Labda tungemuuliza huyo Baba Askofu ni lini alimchagua huyo Kiongozi anayemsema? Nijuavyo mimi Viongozi wa watu huchaguliwa hata Papa mwenyewe hupigiwa kura!
Kwani 2020 kuna rais alichaguliwa na Wananchi?
 
Na tusio na masista na tunatumia mikeka tutauweka kati ya nini?
 
Kwani 2020 hukupiga kura au kusoma hujui je hata picha hukuiona?
Hizo kura ulizihesabu wewe! Tatizo nchi hii si kupiga kura tatizo ni kuziheshimu kura hizo kwa kuzihesabu na kuzitangaza inavyotakiwa kisheria.
 
Mimi nasikitika watu wanaposhindwa kukomalia vitu vya msingi, wakaenda kukomalia nani anaingia na kiti kanisani.

Huko kanisani kwenye Biblia si wameambiwa watii mamlaka maana zimewekwa na Mungu?

Sasa wanaopinga rais kuingia na kiti kanisani walitaka maaskofu wapingane na Biblia kwenye jambo la rais kutaka kuingia na kiti chake kanisani?

Magufuli kaenda mpaka kuchukua mic kanisani na kumzodoa Jaji Thomas Mihayo kwa kuvaa barakoa, that was a more serious issue kwa sababu rais aliingia kanisani akatoa speech kutoka mimbarini, lakini hawa wanaopinga rais kuingia na kiti kanisani walikuwa wapi?

Kanisa lenyewe ni sehemu ya maigizo, mwanzo mpaka mwisho, sasa rais akishiriki maigizo kwa kuingiza drama zake wanashangaa nini?
 
Kiti cha urais hakipashwi kuletwa kanisani!
Unatetea "utukufu" wa Rais /mwanadamu mbele ya utukufu wa Mungu! Hapa umepotoka kiasi kikubwa. mambo mengine jinyamazie! Umekengeuka!
Kiti cha Raisi kuingia kanisani ni Amri.ipi ya Mungu au ya kanisa imevunjwa? Acha porojo

Hakuna amri iliyovunjwa.Chadema mna ujinga sana
 
Ndo huyu Askofu wa ESCROW au sio yeye?
 
Katoliki ndio wanasimika watawala nchi ya Tanzania. Ukatoliki ulianzia Zanzibar kabla ya kuvuka maji hadi Bagamoyo kisha nchi nzima. Maeneo ulikoanzia ndio imekuwa ngome ya kinyume chake ila wanatambua fika bila sauti ya wakatoliki hapatikani kiongozi sijui kuna maagano gani ambayo ni hatari sana. Katoliki mpaka ina balozi wake akimwakilisha Papa hapo Tanzania.
 

Sisi viongozi wa kanisa ni muhimu na lazima tutende mambo yetu kwa mujibu wa maandiko (Biblia - Neno la Mungu)

Ni andiko gani katika Biblia linalo back up utetezi huu...? Ni wazi Askofu Kilaini anasema kwa hisia zake, yaani kwa anavyofikiri yeye...

Anasema "ni vyema kuheshimu viongozi wa nchi". Lakini mimi nasema, kilichofanyika si heshima bali kumkweza na kuabudu binadamu mwenzao kwa sababu ya cheo chake cha kidunia...!

Kuheshimiwa au kutoheshimiwa kuko ndani ya mtu mwenyewe anayetendewa...

Na sidhani kama angeenda kwenye ibada hiyo yeye na watu wake na wakakalia viti ambavyo kila mtu amekalia angejiona hajaheshimiwa...

Kama angekujawa na hisia hizo, basi hilo ni tatizo lake kubwa sana na ni kasoro kwa kiongozi wa watu...!!!
 
Askofu anataka kusema kuwa huyu ni Rais wa kwanza kuingia kanisani. Mwalimu alikuwa anasali Saint Peters lakini hata siku moja hatukusikia kuwa amepelekewq kiti anachokalia Ikulu. Ki ukweli, wakati wake hicho kiti kilikuwa hakionekani nje ya Ikulu. Mpaka alikuwa nae anasali sana lakini hata alikuwa hapelekewi kiti chake cha Ikulu kanisani kwake. Hata wakati wa JPM, sidhani kama alikuwa anaenda na kiti chake kanisani.
Askofu anajichanganya zaidi anapotaka kutuaminisha kuwa ule ulikuwa ni uamuzi wa Kanisa. Kanisa kingetoa wapi kiti cha Ikulu? Au kanisa ndio kiliomba aletewe kiti chake?
Kadinali na maaskofu wanapewa upendeleo kwa sababu ya nafasi zao katika Kanisa. Hawa ni tofauti na wale wote wanaoingia kanisani kushiriki ibada inayoongozwa na watumishi wa Mungu. Hivi anataka kutuambia kuwa viongozi wote wa kisiasa wanapotembelea Vatican wanaenda na viti vyao?
Mimi naamini huu haukuwa uamuzi wa Rais bali ya wapambe ikiwa pamoja na viongozi wa Kanisa maana anaonekana anapokuwa msikitini huwa anakataa upendeleo. Wanaofanya hivi wanamuharibia.

Amandla...
 
Kwani JPM hakuwa rais au alikuwa rais wa daraja la chini kuliko Samia? Mbona amewahi kusali kanisa hilo hilo na kilaini akiwa askofu jimbo hilo hilo lakini kiti cha ikulu hakikuingizwa kanisani hata siku moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…