Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Hawezi shindwa, Kimaro yuko stage ya juu, so akipitisha michango, within a month anajenga kanisa kubwa na waamini kibao wataenda na tatizo la watanzania wengi ni uoga, jua uoga wako ndio adui wako mkubwa kuliko chochote..

Ingekuwa mm, hapo hapo Kanisani, ningemwambia Malasusa, mmenionea sana sana na kuanzia leo hii, mm sio mchungaji wa KKKT, naomba nieleweke hivyo, na sitakubali mateso haya mnanifanyia, hii ingempa heshima kubwa sana Kimaro..

Binadamu mwenzako anakusulubu kisa anaonekana anawazidi umaarufu? Mm ningewapiga chini hao akina Malasusa hapo hapo na kuwageuka na kuachana na KKKT nasema ukweli kwa 100%.. Huu upuuzi kabisa

Kimaro ajenge kanisa lake, anaweza kwa 100%, narudia uoga wako ndio adui yako mkubwa wa maendeleo yako, sio wala watu, ni ww mwenyewe, ukijua unarudishwa nyuma na kunyanyaswa, piga moyo konde, achana nao, songa mbele, uoga ukatae kabisa, ni adui namba moja ya kila jambo duniani.
Naamini Kimaro siyo mjinga!
 
Kanisa limesoma upepo ndani ya siku hizo 60 likaona show iishe namna hiyo
 
Kwani alipoomba msamaha ..alisema anaomba tu msamaha bila ya kutaka kosa lake??

Basi huk sio msamaha .. .. Safi ..chinyango tu!
 
Mkuu, kwanza barua za makaripio ya kichungaji ni za siri zote, wao huonyana kwa siri.

Pili, Ibada ya leo Mchungaji Kimaro alifika kama muumini, hili nimelisema sijui ni kwanini imekuwa gumu wewe kuelewa na kukubali.

Ndio,nimesema ameomba radhi na yeye mwenyewe Mchungaji ndio anajua kwanini ameomba radhi kwa unyenyekevu.

Kuomba radhi ni hiyari yake, angeweza kutumia hiyo likizo yake na kisha kuripoti alipotakiwa kuripoti. Kuomba radhi huku akiendelea na likizo, hiyo ni busara yake yeye.

Unasema aliwakosea waumini wa kijitonyama? Mchungaji Kimaro ni mchungaji wa Lutheran, anaweza kutumwa popote kuhubiri injili. Yeye hakuwa mchungaji wa Kijitonyama pekee. Akikosea anakosea KKKT nzima.
Pamojaamkuu tumalizanee naamzembee kwanza
Maombiyakooo
 
Kwani alipoomba msamaha ..alisema anaomba tu msamaha bila ya kutaka kosa lake??

Basi huk sio msamaha .. .. Safi ..chinyango tu!
Amesema aliposema Vijana wa kiislamu ni waaminifu baadhi ya Watu walimtafsiri vibaya!
 
Kwa hiyo mmeligeuza kanisa la Kabila la wanyakyusa?
Ulijifunza historia wapi wewe. Uliwahi kuwasikia Rebman na Krapf, ambao ndiyo walilileta kanisa KKKT. Rudi darasani ujifunze tena historia ya makanisa (RC, KKKT, Anglican, SDA, n.k. ili ujuwe hayo makanisa walianzia na kushamiri wapi. Utashangaa kusikia Bagamoyo ndiyo kitovu cha Ukristu Afrika Mashariki na siyo Mwakaleli wala Unyayusani kama unavyotudanganya. Ndiyo maana kila Mnyakyusa anadanganya kuwa Mbeya ni Unyakyusani kumbe ni Usafwani!
 
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama ameomba msamaha kwa Kanisa zima la KKKT, Maaskofu, Wachungaji na Waumini wote

Askofu Malasusa amemtangazia msamaha

Askofu awataka Waumini waache Ushabiki kwa sababu wanaligawa Kanisa na huo siyo Ukristo

Tukio lilikuwa mubashara KKKT Kinyerezi

Chanzo: Upendo TV

View attachment 2522599


=====

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt Alex Gehaz Malasusa leo kupitia Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi ametangaza msamaha kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama Dr. Eliona Kimaro ambaye January 16, 2023 Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ilimpa likizo ya miezi miwili bila kuweka wazi sababu za likizo hiyo.

Licha ya kupewa likizo ya miezi miwili, Kimaro alitakiwa kuripoti Makao Makuu pindi likizo yake itakapomalizika, jambo ambalo liliibua taharuki kwa Waumini wa Kanisa hilo na hata baadhi ya Waumini wa KKKT Kijitonyama wakaandamana wakiomba Uongozi wa Kanisa hilo umrudishe Kimaro.

Askofu Malasusa leo amenukuliwa akisema “Sote ni Wakristo lakini wengine tumeitwa ili tuwaongoze katika kazi ya Mungu na hawa ni Wachungaji, tuwatunze, tuwasaidie, tuwaombee na tuwapende, Mchungaji Kimaro, Ndugu yangu kama ulivyoomba na Mimi nasema kwa niaba ya Washarika umesamehewa”

Kuhusu kusimamishwa kwake, soma: Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
Huyu alimkosea mtu au kanisa? Hadi huyu malasusa ajitokeze au kwa niaba yy huyu malasusa alichemka mangapi akavumiliwa?
 
Vyeti feki vimetokea wapi? Au ndio yale ya mtu ana PhD lakini hawezi kuongea au kuandika sentensi ya kiingereza, na maprofesa waliomsaidia kuandika thesis wote akawapa byeo?
Kuwa na Ph.D. siyo lazima ujue kuandika na kunyoosha sentesi ya Kiingereza. Inategemea hiyo Ph.D. iliandikwa katika lugha gani! Unaweza kuandika Ph.D. kwa lugha zaidi ya 30. Ni sisi tu hapa Afrika ndiyo tunaandika Ph.D. zetu kwa lugha za kigeni..Kiirussi, Kireno, Kiingereza, Kichina, Kifaransa, Kipolandi, Kiholanzi, Kidenishi, Kikikuyu, na Kikurya.
 
Angalia kwanza object ninayoitumia kupost humu JF ndio utajua hatufanani wala kulingana!

Mimi sitafuti pesa ya kula,natafuta maisha yenye upendo na amani kwa mke wangu na wanangu!
Ndio maana nawachukia wezi,wala rushwa,wabadhirifu na wakabila kama wewe chiembe !

Mnamchukia Dk Malasusa!

Kisa tu,alimuwajibisha Kimaro! mmachame mwenzenu toka Hai!

Ndio maana watanzania wamewakataa sababu ya Ukabila wenu na kuligawa taifa.
Chagga Dem***** Manifesto!

Tunawaona na tunawajua na tunawadhibiti na mnadhibitika!

Wewe sasa ndiyo unadhihirisha ukabila. siyo kila anayeonekana kuwa upande wa Kimaro ni Mchagga na wa upande wa Mwakjafyale ni Mnyakyusa. Watu wanaandika jinsi wanavyoliona hili jambo. Wewe unaweza kuwa sahihi au mimi ninaweza kuwa sahihi. Yule atayekuwa sahihi hatakuwa sahihi kwa sababu ya kiukabila.
 
Angalia kwanza object ninayoitumia kupost humu JF ndio utajua hatufanani wala kulingana!

Mimi sitafuti pesa ya kula,natafuta maisha yenye upendo na amani kwa mke wangu na wanangu!
Ndio maana nawachukia wezi,wala rushwa,wabadhirifu na wakabila kama wewe chiembe !

Mnamchukia Dk Malasusa!

Kisa tu,alimuwajibisha Kimaro! mmachame mwenzenu toka Hai!

Ndio maana watanzania wamewakataa sababu ya Ukabila wenu na kuligawa taifa.
Chagga Dem***** Manifesto!

Tunawaona na tunawajua na tunawadhibiti na mnadhibitika!

Sasa mkuu, hapa wewe na huyu Chiembe ni nani amedhihirisha kwamba yeye ni mkabila?

Nini kinafanya wewe uone kuna mtu anamchukia Dr Malasusa? Kinachokufanya uone kuna jambo la kikabila hapa ni nini?

Baadhi ya watanzania ni wajinga sana, yani sisi tunaona katika misingi na taratibu za kinadhamu za Kanisa lakini kuna wengine mnaona kwenye Ukabila?

Hivi mkuu ukisoma tena ulichoandika huoni hata aibu? Tumia hicho kichwa kufikiri na uache ukabila.
 
Back
Top Bottom