Atakayenionesha andiko linalosema mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini nampa laki 1 akale sikukuu


Sio lazima kufungisha Ndoa Kanisani.

Kufungia ndoa Kanisani ni mbinu ya kudhibiti waumini(Wateja) waendelee kusali hapo ili Watoto wakizaliwa nao wawe Wateja hapo
 

Hatuongozwi na maneno ya vijiweni.
Tupe Andiko au sheria zilizopo kwenye Biblia/Torati.
 

Hakuna ulazima wa kufungisha Ndoa Kanisani.

Ndoa ni kwenda Kwa Wazazi wa Binti ukiwa na mshenga wako au Ndugu zako, ukikubali kumchukua Binti. Imeisha hiyo. Hiyo ndoa
 
Imeandikwa alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Sasa hapo mtu asie wa dini anawezafunganisha? Na ni nani alie mkuu katika taasisi za kidini ki Mungu?
Hujajibu,mbona akili yako inakuwa biased kuwa alichounganisha Mungu wewe unajua kuwa Ni ndoa tu ndio akaunganisha ama mnakuwa manipulated na viongozi wa kusini ili muwe mateka wao mtoe hela ya kufungia ndoa kanisani kwake.

Sema Sasa alichounganisha pia jikite kabisa kujibu swali alilouliza mleta maada
 
Yaani kitu ambacho watu wengi hawajui Ni kuwa Kuna watu wanataka kuwatawala wengine kupitia nguvu ya jeshi na wengine kupitia neno kujumlisha na hofu kuwa Kuna kifo huko mbinguni,so ili wafuate matakwa yao.

Kila mtu anataka kuwa na misukule itakayofanya wao wanachotaka Ni Nani ambaye hapendi kuwa na watumwa. Huku Kuna vat unalipa kwa lazima ,huku Kuna fungu sijui zaka ulipe 1/10 na unaaahidiwa kuwa ukilipa ndio unajaziwa so hapa unapewa hope tu ndio Imani yako. Cheki mwamposa ,gwajima, mwingira ,kakobe wanavyojikusanyia utajiri kisa Cha upofu wa watu wachache wajinga.


Bana Kuna jamaa alikuwa anahubiri dini akaja kwenye blocks za hostel enzi nikisomea Moscow,Sasa jamaa akapiga neno baadaye akasema kuwa fungeni tusali. Nilimsikia yule mrusi anamuiliza "ZA CHEMU?" yaani ili iweje yule mhubiri akakosa jibu ikawa imetoka ivyo.
 
Biblia inasema tu fulani alikuwa mke wa fulani au mume wa fulani taratibu za ndoa hazipo, pia hata taratibu za kipa imara sijui komunio pia hakuna hii kitu, only Jews follow the Bible by 100%
Kipaimara huo ni utaratibu wa makanisa 2 kama sijakosea Lutheran na RC na wakati wanaanzisha huo utaratibu Biblia ilishatungwa na kukamilika kitambo,
 
Wewe kama umeamua akili yako iamini hivyo. Mimi siwezi kubadilisha. Mnajitoa ufahamu tu.
Kwani ndoa zote zinafanyikia kanisani au msikitini? Ama zinafungwa na viongozi wa dini pekee?
 
Wewe kama umeamua akili yako iamini hivyo. Mimi siwezi kubadilisha. Mnajitoa ufahamu tu.
Kwani ndoa zote zinafanyikia kanisani au msikitini? Ama zinafungwa na viongozi wa dini pekee?
Sijaamua Ila iko huru,ujibu swali la jamaa
 
Ndoa ya kiislamu hufungishwa na walii wa binti, ila kwasababu ya uchache wa elimu ndio utakuta baadhi ya vipengele kama utangulizi na nasaha baada ya ndoa vinasimamiwa na kiongozi wa dini, ila ndoa anafungisha mwenyewe mwenye binti yake au aliyekabidhiwa na wenye binti.

"...basi waoeni kwa idhini ya mawalii wao.."
Quran 4:25

Hapa utaona walii anamwambia bwana harusi nimekuozesha binti yangu fulani kwa mahari mliyokubaliana, na yule bwana harusi anajibu nimekubali kumuoa fulani binti fulani kwa mahari tuliyokubaliana..

Huu ndio utaratibu kwa mujibu wa uislamu.
 
Imeandikwa alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Sasa hapo mtu asie wa dini anawezafunganisha? Na ni nani alie mkuu katika taasisi za kidini ki Mungu?
Acha ujinga ...unataka kutuambia ndoa za wapagani siyo ndoa mbele za mungu mbona yusufu ana kataa kutembea na mke wa boss wake na kusema ni kumkosea mungu .. au amri inayo sema usimtamani hata mke wa jirani yako siyo sahihi hivyo unaweza kumtamani mke wa jirani yako ambao ni wapagani
 
Wewe ndio uache ujinga. Sticky to the post.
Kwani op kauuliza kuhusu ndoa za wapagani? Shawn.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…