Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Kabla hujatafuta alichosema Pengo....umesikiliza clip ya Gwajima?tuanzie hapo

Clip ya Gwajima nimeisikiliza na mi kama mkristo sidhani kama ile ilikuwa njia sahihi ya kumuongelea Mzee Pengo.
Kwanza ukiangalia suala la umri tu, Gwajima anapaswa kumuita Pengo Baba. Tofauti ya itikadi za kidini haitupi right ya kumuongelea mwingine namna ambavyo Gwaj amefanya.
Nadhani unajua fika kuwa vitabu vyote vya dini hususani Biblia nnayoisoma mimi imeainisha kinagaubaga kuwa suala la kuwaheshimu wazazi ni jukumu letu sote. Yeyote aliye umri sawa na mzazi wako naye ni sawa na mzazi wako. Hivyo ndivyo tulivyolelewa enzi zile mpaka sasa. Utandawazi umepunguza maadili sana lakini haitufanyi kukengeuka kiasi hicho.
Tunapaswa kuenenda kama maandiko yanayotuambia tusije jichumia dhambi za kukosa utiifu buuureeee.

Nadhani mpaka hapo nimeshajibu swali lako
 
Mtu yeyote akiniambia hapa gwajima alivuta bangi kabla ya kupanda madhabahuni na kutoa matusi yale. nitakubaliana naye kwa asilimia mia moja.
 
Kwa wanaomuunga mkono Gwajima kumtukana Pengo, lazima wapimwe akili zao na vyama vyao wanavyo shabikia ili kujua uwiano
 
Mtu yeyote akiniambia hapa gwajima alivuta bangi kabla ya kupanda madhabahuni na kutoa matusi yale. nitakubaliana naye kwa asilimia mia moja.

Lazima awe alivuta bangi au alitumia madawa ya kulevya wanayomtuhumu nayo au alikunywa kiroba kabla ya kuanza mahubiri.Siku hizi kuna wahubiri nimeambiwa na waimbaji wa nyimbo za injili huwa hawawezi kupanda mazabahuni bila kunywa viroba ili kupandisha munkari.

Iko haja ya makanisa kuwa na vipima ulevi kama vile vya matrafiki kabla mtu hajapanda kuhubiri au kuimba.
Nadhani uko sahihi Gwajima alihubiri akiwa kanywa pombe hasa viroba.
 
Ndugu yangu funika kombe basi mwanaharamu apite.Hili tutaonyana kanisani ila wakristo tunawasupport maaskofu wetu na waraka ule! Mi ni mprotestant nitautafuta...... umebeba maudhui mujarabu kabisa!
"nitautafuta"......kumbe ni ushabiki mbuzi unaleta hapa wala maudhui hujui....

Ipo siku Gwajima atakwambia mlambe makalio na utamlamba...ushabiki kitu kibaya sana..
 
Unafikiri hapo ulipo unaakili timamu..??

Ni wapi Pengo kasema watu wapige kura ya Ndiyo....Hii mihemko mliyokuwa nayo kurukia mambo bila kusoma na kuelewa ni hatari mno..
Hutakiwa kimtetea mpuuuzi,mnufaikaji wa peza za escrow pengo. unatakiwa kua zezeta kumtetea pengo,sitaki kuamini kama wewe pia uko hivyo.

Unamsahihisha kwa kumtukana na kutukana wakulima ambao ndo wanalisha nchi hii??

Have you contamplate your thought before posting here..??

Pathetic fool
Jifunze lugha za watu.
 
USALITI ALIOUFANYA PENGO HAUVUMILIKI.

Nilishasema tangia awali ya kuwa Pengo amekosa na tena amekosa sana sana. Yawezekana mtu mwingine wa kawaida na mdandia mada ambaye umeona tu au kusikia audio clip za viongozi hawa wawili ukasema Pengo ametukanwa. LA HASHA AMEPATA ALICHOKUA ANAKITAFUTA.

Dawa ya MSALITI na MTU MNAFIKI duniani kote ni kuambiwa ukweli wake hadharani tena mbele ya kadamnasi, na kwakua aliongea hadharani yeye mwenyewe Pengo ndio alikua wa kwanza kuvunja utaratibu kama mmoja wa viongozi na wajumbe wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Hakuna namna, PENGO NI MSALITI na ni MNAFIKI...

Pengo anasema...."NIMEKUBALIANA NA BARAZA LA MAASKOFU TAMKO LISOMWE KWENYE MAKANISA, NA PIA KWENYE MAKANISA YOTE YA JIMBO LA DAR ES SALAAM" Swali ni kwamba kama alikubaliana na hayo kwanini tena aseme kuwa ILA MIMI BINAFSI NAONA HIVI NA VILE wakati yalishapita maazimio ya pamoja ambayo naye aliyakubali?

Pili, Hoja yake binafsi ilitakiwa iwasilishwe kwa utaratibu kwa kuipeleka mbele ya Baraza la Maaskofu ili kuonyesha kutoridhika kwake na sio kuitisha vyombo vya habari na kuongea kama alivyofanya hukuakijua nafasi yake ni ipi katika jamii.

Tatu, Pengo ni lazima aambiwe hadharani na alichoambiwa na Askofu Gwajima kwanza ni kidogo kutokaa na namna ambavyo ameutangazia umma wa Watanzania ya kuwa HAKUNA KITU KINAITWA UMOJA BAINA YA WAKRISTO WA TANZANIA ila kila mtu anafuata matakwa yake mwenyewe huku ikumbukwe ya kuwa Pengo huyuhuyu ndiye aliyekuwa miongoni mwa waasisi wa awali kabisa wa Baraza hili la Maaskofu Tanzania.

Tatu, je baada ya Pengo kusema aliyoyasema amewaweka katika hali gani maaskofu wengine wote waliokubaliana na kuweka saini katika TAMKO lile? Wameonekana kana kwamba ni viongozi wanaotaka kuligawa taifa kwahiyo kwa mtu mmoja PENGO amewafanya wenzake kuwa sio kitu mbele ya jamii.

Bado, unasema huyu jamaa Pengo hajafanya makosa? PENGO ni msaliti na wasaliti wote hufa au kupotea ghafla kwa mawazo kutokana na usaliti wao. Njia ya wasaliti haijawahi kuwa ya mafanikio hata siku moja..

#PENGO THE TRAITOR
 
Kweli nimeamini humu ndani kuna watu matusi kwao ni sehemu ya chakula. Hivi unaweza kuunga mkono hayo aliyosema ngwajima? hata kama asingekuwa ni kiongozi wa dini, kwa mtu wa kawaida tu utagundua kwamba si mtu mwenye busara/hekima/ maadili hata kidogo. Mimi nimeshindwa kumwelewa kama ailpata ukichaa wa muda ama vipi, manake hayo maneno ni ya kuhuni kabisa, sijui anaimba taarabu eti ni kiongozi wa dini na kuna watu hapa wanamsifu kwa nguvu zao zote!!!? Kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
 
Unamsahihisha kwa kumtukana na kutukana wakulima ambao ndo wanalisha nchi hii??

Have you contamplate your thought before posting here..??

Pathetic fool

Mahaba yako kwa Pengo yatakuua, wewe unadhani kushabikia hiyo kura ya Ndiyo ndo sahihi? Utashinikiza kukubali kitu ambacho wananchi hawajakisoma na kutafakar? Wangapi kijijini kwenu wana nakala ya Katiba pendekezwa?
 
CAG sio kiongozi wa waislamu ni mwislamu muumini wa kawaida.Atukane Mufti au sheikh kiongozi yeyote uone mziki wake


Ishu sio kutukana hapa! Ni kusema ukweli ambao kimsingi ni mchungu baada ya watu kufanya upuuzi.
Askofu Gwajima ndio kiongozi wa kwanza wa dini kusimama na kukemea UWEPO WA MSIKITI pale uwanja wa ndege. Kwenye mahali pa public service unaweka msikiti huo si upuuzi kabisa.

Askofu Gwajima ndio kinogozi wa kwanza na wa mwisho wa kidini kukemea uongo wa serikali juu ya ugonjwa wa kutunga wa #DENGU na baada ya kukemea na audio clip zake kusambaa nani mwingine aliusikia ugonjwa wa dengu?

Askofu Gwajima ndio alimlipua huyu CAG mpya alipokua akitaka kujenga msikiti ndani ya ofisi za serikali.

UKWELI LAZIMA USEMWE. MTU YEYOTE AKIKOSEA ANASEMWA HADHARANI PASIPO KUPEPESA MACHO, NCHI HII HAITAKAA SAWA KAMA WATU WANAENDEKEZA KUFUMBIANA MACHO KWENYE UOZO ALAFU TUAMBINE KUWA WASISEMWE WALA KUKARIPIWA..
 
Kwa wanaomuunga mkono Gwajima kumtukana Pengo, lazima wapimwe akili zao na vyama vyao wanavyo shabikia ili kujua uwiano

Jengeni basi hospitals za kutupima akili badala ya kuiba fedha kwenye masandarusi na magunia! Wapuuzi, hamfai, mnanuka uovu!
 
"angebalance kidogo kwa kuionya pia serikali kuwachagulia maoni wananchi" kwa nini usingeingia kwenye kichwa chake ili atoe maoni kama unavyofikiria!? ni mawazo yake punguza munkar
 

Wale maaskofu wote wengine ndio wasaliti wa Demokrasia.Demokrasia ni uhuru wa mtu iwe wa kupiga kura apige kwa kadri ya dhamiri yake.Wale maaskofu ni maruhuni wapinga demokrasia ya uhuru wa mtu kupiga kura aitakayo kupitia tamko lao.

Pengo kakataa kukaa upande wa wachache wasiopenda demokrasia ichukue mkondo wake kaamua kukaa upande wa walio wengi wanaotaka kupiga kura yao kwa hiari bila shinikizo la yeyote liwe la kidini au chochote.Ukiwachambua matamko yao kidemokrasia lile tamko la maaskofu si la kidemokrasia na halijengi demokrasia wakati la pengo ni la kujenga demokrasia sababu linawapa uhuru watu kupiga kura watakavyo.Lile lingine la kidikteta na la kuvunja demokrasia.

NATAMKA BILA KUMEZA MANENO KUWA LILE TAMKO LA MAASKOFU SI LA KURUHUSU DEMOKRASIA ICHUKUE MKONDO WAKE NI LA KUHARIBU MFUMO WA DEMOKRASIA KATIKA NCHI.

Pengo ni Mwanademokrasia halisi kwa tamko lake na inampa heshima kubwa kwa wapenda demokrasia popote duniani.Ukichukua TAMKO LA MAASKOFU NA LA PENGO UKAWAPELEKEA WATAALAMU WA DEMOKRASIA popote duniani wafanye evaluation watakwambia lile tamko la maaskofu ni UCHAFU MTUPU.Ni aibu kwa kundi kubwa la maaskofu kukaa na kuandika tamko kama lile lisilo la kidemokrasia.nAFIKIRI UZOEFU WAO WA KUBURUZA WAUMINI MAKANISANI WANADHANI HUO HUO WAWEZA TUMIKA KWENYE KURA.

Maaskofu wale waliotoa lile tamko sisi wengine tunawaona hawana maana na ni wavunja demokrasia na wapenda kuvunja amani tu ya nchi.Lakini Pengo tunamwona yuko vizuri ni mwanademokrasia mzuri anayeitakia nchi iwe na demokrasia nzuri hivyo iwe na amani.

Maaskofu waliotoa tamko lile ndio WASALITI WAKUBWA WA DEMOKRASIA.Msaliti wa demokrasia sio Pengo ni hao wengine na huyo Gwajima.Wajifunze kupitia hili kuwa matamko mengine kwa siku zijazo wakae kwa makini kabla ya kutoa matamko kama ambavyo Pengo huwa anatulia na kufanya.Pengo ni kiongozi mwenye akili mno na katulia na kakomaa kiuongozi.
 
CAG sio kiongozi wa waislamu ni mwislamu muumini wa kawaida.Atukane Mufti au sheikh kiongozi yeyote uone mziki wake

:biggrin1: Mbona alishawahi kumshika sheikh yahya ambaye alitamka kwamba amwekea mheshimiwa mmoja ulinzi usioonekana dhidi ya maadui wake na hakuna kilichotokea.
 


UNAZUNGUMZIA DEMOKRASIA IPI?

Kwa namna yeyote ile ni ngumu sana wakristo wote Tanzania kwa idadi yao kukutana na kufanya maamuzi kuhusiana na mambo yao kama wakristo hivyo kukawa na uongozi ambao baadae ukaunda Baraza la Maaskofu Tanzania ambacho kimsingi ndio chombo cha juu kuhusiana na misimamo, maoni, matakwa na mambo yote yanayohusu maslahi ya wakristo nchini na hii inaitwa REPRESENTATIVE DEMOCRACY.

Sasa kwa suala la Pengo akiwa mmoja wa watu waliokusanyika kufanya maamuzi ya wakristo kupitia Baraza hili la Maaskofu anaowajibu wa kufuata yale ambayo kama Baraza limenuia kufanya kwa pamoja kwani maamuzi ya wengi ndani ya Baraza yanapokuwa yamefikiwa hakuna namna ila wote kufuata.

Katika hali ya kawaida ili maamuzi yapite na yawe ya wengi lazima yawe zaidi ya nusu au kwenye katiba nyingi wanasema jumla ya watoa maamuzi wawe theluthi mbili ya wajumbe wote. Pengo ama angekuwepo ama asingekuwepo kwenye kikao ila kwakua theluthi mbili imefikiwa basi anakuwa hana sababu nyingine ya kupinga maamuzi ya wenzake mbele ya umma na kujionyesha kuwa hakubalini nayo.

Alitakiwa kufuata taratibu za namna ya kupinga maamuzi ndani ya Baraza na kutoa mapendekezo yake na kama angefanya hivyo angekuwa muungwana lakini kwa njia aliyofanya yeye hakuna namna yeyote ya kumtetea PENGO ANABAKI KUWA MSALITI NA MNAFIKI.

Jiulize, ZZK aliandaa tu waraka wa mabadiliko ambao kimsingi si vibaya kuandaa waraka wa mabadiliko ndnai ya chama ili kuboresha lakini kwakua hakufuata taratibu lazima aonekane MSALITI na ndivyo kwa PENGO naye ni msaliti kama wasaliti wengine.

Pengo ameutukanisha UKRISTO mbele ya jamii nzima ya kitanzania na kuonyesha wazi kuwa kanisa au wakristo Tanzania ni watu wasio na umoja na ndumi la kuwili.
Amewaaibisha maaskofu wengine wote waliokubalina na TAMKO.
HAKUNA NJIA ILIYOBAKI YA KUMSAIDIA PENGO ILA KUMWAMBIA UKWELI KUWA YEYE NI MSALITI NA MNAFIKI.
 

Hao maaskofu wa TEC kuna muumini gani aliwahi kuwapigia kura kuwachagua hao maaskofu au kuwachagua kuwa wawakilishe kwenye hilo baraza la maaskofu? Representative Democracy inataka uchaguliwe na hao unaowawakilisha.

Hao maaskofu wa TEC hawajawahi chaguliwa na muumini yeyote wa kikatoliki kuwa awawawakilishe kwenye hilo baraza la maaskofu.Wako pale wakijiwakilisha wenyewe na nafsi zao ndio maana lile tamko halikuzingatia matakwa ya waumini ya kupiga kura kwa hiari kidemokrasia.

Tamko lao ni lao kama kikundi cha watawala wachache wa kanisani wakiwakilisha maoni yao wanavyofikiri kwenye kikao chao ambacho hawajatumwa na muumini yeyote Kwani hajawachagua wala kuwatuma wakaandike hilo tamko.

Pengo alifanya utafiti akaona kuwa watu wanahitaji uhuru katika upigaji kura ndio akatoa tamko hao wengine walikurupuka tu kwa mihemko ya ushabiki wa kisiasa badala ya kutafiti kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…