Mpuuzi ni mtu anayepuuzia mambo ya muhimu! Mjinga ni mtu asiyejua! Mpumbavu ni mtu asiyejua ila akifundishwa anajua/anaelewa...Tusi liko wapi hapo?
Halafu hivi Pengo alishindwa kuitaadharisha na serikali isiwaambie wananchi waipigie katiba kura ya Ndio?
Hivi kweli kosa la Kardinali Pengo mpaka Gwajima amtukane kiasi hicho nini hasa?!!!
Pengo alitoa maoni yake kwamba waumini wapewe elimu kuhusu yaliyomo kwenye mapendekezo ya katiba mpya, halafu waamue wenyewe bila kushurutishwa kuipigia katiba kura ya ndio au ya hapana.
Msimamo ya CCT ambao unaongozwa na Askofu Malasusa ambaye ni KKKT, uliwataka waumini waisome katiba inayopendekezwa kisha waipigie kura ya hapana. Kimsingi hii siyo demokrasia. Nyie maaskofu mnaowataka watu watumie demokrasia yao kama mnavyotaka ninyi mmepata wapi mamlaka hayo??? Hilo ndilo swali la msingi la Kardinali, hakuna jingine!
Sikiliza vizuri alichosema Kardinali:https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=237215&d=1427127373
Kweli nyie wenye akili mnaona kwamba Kardinali amekosea hapa? Mlitaka awe dikteta kama alivyo Gwajima ndio mfurahi?
Gwajima amenishtua kabisa, huu ndio mwanya kwa wale wanaotaka kupima roho na kujua mtumishi gani ni wa kweli na yupi ni wababaishaji. Au mnasubiri mwone Yesu akishuka kutoka Mbinguni kuwaambia huyu ndiye na huyu siye?
Huwezi kuniambia hata kidogo kwamba alivyofanya Gwajima kumtukana Kardinali aliyetoa maoni yake ameongozwa na Roho Mtakatifu, nafikiri anaongozwa na roho mtaka "tifu".
Watanzania jifunzeni kufikiri la sivyo mtaendeshwa kama baiskeli na hawa wahuni wanaojiita watumishi wa Mungu.
Mnaonaje kama Kardinali naye angekuwa mwendawazimu kama Gwajima na kujibu matusi aliyotukanwa?
Pengo amevuna alichopanda. Wakatoliki wengi wamechelewa kumjua mnafiki mkubwa huyu.
MABAGHEE;
Ni kweli ngwajima alitumia maneno makali sana lakini contents ya alichokizungumza kina mashiko na Pengo amevuna alichopanda.
.....Pengo ni mnafki sana, kama analijua hili kwanini asingegoma kusign ktk huo mkataba baada yake akasign kisha akaja kusema pembeni mambo ambayo no tofauti na mkataba.
.....Viongozi wa kiroho (Maaskofu) siku zotr huwa wanatutakia mema, mimi binafsi kwa taifa letu lilipofikia naona ni vema kwa wao kuungana na kupiga kura ya HAPANA.
.....Na ifahamike kwamba, Wakristo wengi au Watanzania wengi hawajaisoma Katiba Ipasavyo, kama wao wameiosoma na wameona haitafaa kwa Maslahi ya Watanzania ila ni kwa maslahi ya CCM ni vema wakatuambia ukweli na tuikatae.
.....Pengo najua ameona madhaifu ya KATIBA na yeye kama kiongozi alipaswa kusimama wima na kupinga vikali juu ya hiyo katiba, sio kuanza kuwa na maamuzi mepesi mepesi wakati ikipita Maisha ya Watanzania yatakuwa mabaya zaidi.
.....Asilimia kubwa ya maoni ya Watanzania yametupwa nje, sasa hiyo ndo Katiba ambayo tunaitaka? Mimi nasema kwamba Hakuna Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake ambae ataikubali hii Katiba, hata mimi ninhekuwa na uwezo wa kupita kila mahali na kusema watu waikatae katiba mpya basi ningefanya hivyo.
.....Pia tutambue kuwa waliomuona Pengo ni mpuuzi sio Gwajima tuu, Chama cha Maaskofu Tanzania kipo na watu wengi, nadhank wote wamemshangaa Pengo na wakaamua kuwa na maneno ya pembeni, heri Gwajima katoa yake ya Moyoni.
.....Naungana na Gwajima kuwa Pengo ni mbweha tuu.
Halafu hivi Pengo alishindwa kuitaadharisha na serikali isiwaambie wananchi waipigie katiba kura ya Ndio?
Pengo na Gwajima woote wana makosa ya kipi cha kusema na wapi pa kusemea na ni lipi kulisema au kutolisema! wajifunze kuwa wao ni viongozi katika jamii!
Kard.Pengo - Ameruhusu barua isomwe na halafu anaiponda! Yeye siyo msemaji wa TEC!
Gwajima - Matusi siyo kitu chema na katika kadhia kama aliyoianzisha Kard.Pengo kunahitajika uvumilivu!
Pengo hahitaji kuwa mnafiki kwa lolote, maaskofu wa kanisa Katoliki sio maaskofu uchwara wanaotafuta umaarufu ili wapate waumini wengi kwenye mikutano ya Injili. Waangalie maaskofu hao wa makanisa binafsi akina Kakobe, Mzee wa upako, Mwingira na Gwajima, hawa ni watu wanaocheza na akili za watu kwa ajili ya ufahari wa maisha yao tu na wala hawatoi chochote kusaidia jamii isipokuwa kujenga majumba ya kifahari na kununua magari na ndege za mabilioni huku makanisa yao yakichangia nothing kulinganisha Kanisa Katoliki; mashule, hosptali, vyou vikuu, nyumba za yatima na wakoma kila mahali, tembea uone!
Yaani nyie mnaoabudu vinyago na yule mke wa Yusufu (Mariam) ndo muwe sauti ya ukristo!!???
Nyie msioweza hata kukemea kajini kadogo kamaimua nyie ndo muwe kabisa sauti ya ukristo!!???
Nyie kabisa nyie????
Kwa lipi hasa muwe sauti ya ukristo??? Kwa idadi ya mahekalu makubwa yaliyojazwa sanamu na vinyago!!??
YESU KRISTO NA AKUKEMEE.
Mtafungua thread kibao kuhusu Gwajima. Watu wameshaonge kwenye threads zingine hujapitia hoja au umepata chochote kufungua yako.
Awali ulikua hujauliza swali, jibu ni kwamba alichokisema BABA MTUKUFU DOKTA NABII GWAJIMA kuhusu Kardinali Pengo ni kweli kabisa.
Uliza swali lingine mdogo wangu.
kwa jinsi ulivyojaa majivuno,kiburi na kudharau wengine,utaishia kukemea mapepo tu,lakini mbinguni uwezekano wa wewe kuingia ni mdogo sana Mathayo 7:22
Kwa hiyo mwisho wa siku tukiambiwa na TEC kwamba lazima tumchague fulani kua Rais tukubali kwani sisi ni Punda