Awamu ya Rais Samia ndiyo awamu iliyofeli kuliko awamu zote na kufanya wananchi kujutia zaidi uongozi huu

Mkuu, hawawapigii,

Ndugu yangu imhotep jaribu kuulizia kwa wananchi watakwambia


Hawawapigii ccm nakuhakikishia kuwa hawa ccm ni majambazi
Mkuu una ushahidi wowote wa hili mimi nilikuwa nategemea kura japo za hasira au wasimamizi wa ACT walihongwa?

Au Wananchi wanakisubiri CHADEMA ndio wakipigie kura?

Changamoto kwenye Chaguzi huwa hazikosekani lakini huko Mbarali ACT alikuwa ameachwa mbali sana.

Kama wangekuwa wamepishana kura 1000 au 2000 tungesema YES wamepora na hapohapo tungesema Wananchi wameonyesha hasira zao kwenye Ballot Box lakini walikuwa wamepishana mbaaali sana.

Je Mtanzania kweli yuko ready kwa Mabadiliko au ni mtu wa kulalama kutwa kuchwa?
 
Uliza na SGR ili nijibu yote kwa mpigo. Kila la heri.
 
Serikali ya Samia haiwezi enda na akili za kipumbavu kama hizi za kuua Kilimo.

Ili kuondoa maelfu ya watu kwenye umaskini uliotopea huko Vijijini,Kilimo kimefanywa biashara na juzi hapo Rais kawaambia watu huko Mtwara kwamba mbaazi sio mboga ni biashara hivyo they should think in business way likewise kwenye mazao mengine yote.

Huwezi ondoa watu kwenye umaskini Kwa kununua mazao Yao Kwa bei za kutupa ambazo haziwasaidii kutoka kwenye umaskini,huo upumbavu ni WA awamu ya 5 na watu wa Vijijini hawawezi kuendelea kuwa maskini wa kuwanugaisha nyie wa Mjini.

Ndio maana Sasa Kwa miaka 3 Sasa sekta ya Kilimo inaongoza Kwa kupokea mikopo Mingi.

View: https://twitter.com/TheCitizenTz/status/1704830802461118496?t=prLLyiPA2iAgAYvaz8JjGw&s=19
 
Kaa usitafute link utaona moto utaishia kulalamika hivyo hivyo

Ni awamu ya 6 ndio inaongoza kufanya haya
-Serikali inaajiri sana kuliko wakati mwingine wowote
-Biashara zinafunguliwa Kwa Kasi kuliko awamu yeyoey kabla
-Kilimo.kinakua kuliko wakati mwingine wowote
-Sekta ya ujenzi hasa private imeanza kukua Kwa Kasi sana
-Uwekezaji hasa wa Kilimo,viwanda na ujenzi unakua kuliko Wakati mwingine wowote
-Public expenditure ni kubwa kuliko Wakati wowote maana Kuna utitiri wa miradi sekta zote.

Sasa baba endelea kulalamika utaona moto, wakulima wa stakabadhi ghalani wanaendelea kula maisha 👇

View: https://twitter.com/thebizwiztz/status/1704149977050517902?t=hzybYpNR5HTthUdYVOSG6A&s=19
 
Umeongea vyema kwamba shida zilianza Toka zamani ila kwangu binafsi naona mwanga awamu ya 6 Kwa sababu zifuatazo.

1.Serikali inajaribu kuwa na sera zinazotabirika kwenye biashara na uwekezaji Ili kuwe na consistent ya mambo

View: https://twitter.com/dailynewstz/status/1704733721885045057?t=ehCbYaUxdFhf6Yzl-9CpoQ&s=19
2.Serikali imepunguza vikwazo vya biashara Kwa kiasi Fulani na soon watakuwa na single payment window badala ya kulipia Kila taasisi,kupunguza utitiri wa leseni nk

3.Serikali ya Sasa inasema Kilimo ni biashara hivyo imepunguza ukiriyimba huko,imeshusha riba za mikopo Kwa Kilimo ambapo ni 9% tuu na on top of that ime priotise irrigation farming na kutafuta masoko ndio sababu sekta ya Kilimo ndio inaongoza Kwa mikopo ya biashara,the so called ajenda 10/30 is real.

4.Swala la vibarua na Wafanyakazi sekta binafsi wanalipwaje Hilo hakuna Serikali itaingilia maana ni makubaliano binafsi.

Kiufupi awamu ya 6 is doing good than all other past awamu ndio sababu the so called matatizo eg umeme ni matokeo ya mafanikio na uzembe wa awamu zilizotangulia.
 
Unajitahidi kufafanua kinachofanywa na awamu ya sita lakini huwezi kuepuka kuitwa chawa wa mama.

Kwa haraka haraka ukiangalia biashara za frames za maduka mitaani utaona kuna uhai, nyingi zinafunguliwa na zile zilizoachwa magofu zinaendelea kufufuliwa. Kuna mzunguko wa pesa huko mitaani.

SSH anaendeleza kile kilichoanzishwa na marais wengine na ndio maana ya kupokezana vijiti.
 

Huna akili wewe
 
Huna akili wewe
Namba ndio zinaongea sio porojo zako.

Kabla ya kuchukua na kununa tafuta Bajeti ya Wizara yeyote unayoijua wewe mwaka 2020 harafu fananisha na Sasa then uje na majibu.

Kama hutaki huko nenda kwenye private investments report ya mwaka 2020 harafu njoo ulingamishe na ya Sasa

Broo utanuna weee na kutukana ila ukweli utabakia hivyo hivyo na endelea kukaa uache kutafuta fursa utaona moto kitaa.

Mwaka Jana kulikuwa na shida ya Maji Dar,vipi saizi Bado? Nipe jibu bwashee

View: https://youtu.be/KwM9kyXbXzg?si=O9s4mi4sul1f86bk
 
Kitaalamu tunakuita chawa promax. Uko beyond ya uchawa.
 
Mimi Huwa sijali kuitwa chawa Kwa sababu am not Chawa na Wala silipwi na yeyote hapa ,natumia mda na rasilimali zangu kama raia Mzalendo na shabiki wa Samia.

Proud of her leadership and resilience maana Kuna mambo ningekuwa Mimi nisingevumilia.

Binafsi ukitaka nigombane na Utawala basi awe na sera za Kijamaa kama za Mwendazake maana mara nyingi ni sera za Kuendeleza uvivuzulalamishi na umaskini ndio maana utakuta zinaongoza Kwa vitisho na propaganda.

Kazi nzuri kama hii ya Samia inafanywa kwenye Mikoa ya Iringa,Geita,Tanga na Lindi.

View: https://twitter.com/TaruraTz/status/1705137668500115750?t=mBHcn_E9EkrZ5_C3fkFGvg&s=19
View: https://twitter.com/TaruraTz/status/1705138930952110314?t=nVcdW414yvzhvEh7UIpWog&s=19
Hizo ni Barabara za lami Vijijini sio TanRoads Bali Tarura
 
Kitaalamu tunakuita chawa promax. Uko beyond ya uchawa.
SSH anafanya kazi nzuri na sisi tunaoishi mijini huwa hatuoni matokeo ya kazi hiyo.

Kuna vijana 270 wapo Israel wanajifunza masuala ya kilimo, watakaporudi watakuja na fikra za kimapinduzi kwenye suala zima la kilimo na hakuna mtanzania anayewazungumzia.
 
Hamuwezi kuona Kwa sababu mna alternative nyingi ila sie wa Vijijini tunaona kinachofanyika.

Hapo Mjini hata mkijengewa hospital ni kama hakuna kitu maana mna alternative za private pengine kina Mama ndio Huwa wanaona tofauti ila wanaume wa siku hizi ni hovyo kabisa kazi kulalamika tuu 😁😁

View: https://twitter.com/TaruraTz/status/1704884201378443280?t=oQojWRMPZ6rDhUsvPiKH6A&s=19
View: https://twitter.com/TaruraTz/status/1704887385438278066?t=o0LIVXIu2qiC3A_Dpm8wBQ&s=19
 
Hao vijana unajua wazazi wao ni akina nani!?. Fuatilia then niambie kama kuna mtoto wa mlala hoi hata mmoja!

Halali umsifie mama kuwa anaupiga mwingi maana upo mjini, tembelea mikoani (vijijini) uone jinsi gani wananchi wanateseka kwa sababu ya ukosefu wa maji, umeme, kodi na mfumuko wa bei za bidhaa.

Hivi can you imagine mkoa kama wa mwanza unakosa maji wiki nzima wakati ziwa victoria lipo karibu namna ile.

Gharama za matibabu zimepanda watu wa kawaida hawawezi kuaford hizo gharama.

Watu wanachangamoto za figo, figo hazifanyi kazi vizuri na hawana uwezo wa kuaford dialysis hakuna msaada wowote kutoka kwa serikali, lakini akina professa J walioharibu figo zao kutokana na life style ndo wanasaidiwa, can you imagine that huh!. Kuna wagonjwa hawawezi hata kufanya vipimo kama CT SCAN na MRI.

Halafu chawa kama wewe unaibuka from no where unasema mama anaupiga mwingi huku miradi haikamiliki ndani ya muda.

Next time kabla haujajibu swali kukuhusu kumtetea mamaako Samia inatakiwa uende vijijini ukajionee maisha ya watanzania wenye hali ya chini. Nenda hata manzese ujionee watu wanavyoishi maisha ya shida.
 
Vijana wa BBT unawajua wazazi wao?

Kama awamu zilizotangulia zilishindwa Kupeleka umeme na Barabara Vijijini ulitegemea Kwa miaka 2.5 Samia amalizie hizo shida zote? Though is doing excellent job than any other before.Kodi zimeanza awamu ya 6? Kama Kuna mfumuko wa bei Kwa nini huzungumzii mfumuko wa pesa walizopata Sasa ambazo kabla walikuwa Hawapati? Uwe unaweka ushahidi kama Mimi

View: https://www.instagram.com/p/CxWFJZ3M6QD/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
Mkoa kama wa Mwanza lini ulikuwa na uhakika wa Maji? Ni sasa ndio Samia anajenga chanzo kikubwa Cha Butimba Kumaliza shida ya Maji kama Dar.

Kwanza lazima uelewe hicho unachoita gharama za magonjwa ya figo ni zimeshuka half price,Mama alishusha kama unabisha Uliza daktari wako amkwambie bei za 2020 na Sasa.On top of that hata hizo CT Scan zilikuwa hospital kubwa Sasa ni Mikoa yote(Kazi ya Samia vinginevyo wewe ulitakiwa utoke Nanjilinji Kufuata CT Scan Dar).

Mwisho maisha ya Vijijini Kwa Sasa ni Bora zaidi kuliko miaka 2 iliyopita ndio maana hukuti watu kukimbilia Mjini , Kijijini Kuna umeme,maji,Huduma za Afya,Shule na uhakika wa usafiri.

View: https://twitter.com/ruwasatz/status/1697129408434151904?t=-Ga72_Cq00nO0Uo8etX08g&s=19
 
Tatizo lenu ni hilo hilo kukimbilia maongezi ya matumizi ya neno chawa. Hasira zenu hazina msaada wowote wa kubadili hiyo hali.

Umaskini upo na utaendelea kuwepo kwa miaka mingi. Lakini nakataa kusema kwamba awamu ya sita haifanyi lolote. Yapo mengi sana ya kiuchumi yanayoendelea kufanyika muda huu.

Kuna suala la mishahara kuongezeka huwa haliongelewi, kuna masuala ya msururu wa kodi kufutwa hata siku moja hayasemwi.

Ukiamua kuyaongelea unapachikwa jina la Chawa!, kisa unajitegemea kwenye suala la kutoa maoni.
 

Hata kwa kikwete mlisema hivi alipokuja magu napo mkasema hivi tena mkazidisha kilio saiv kwa mama wimbo wenu ule ule
 
Ongezeko la mshahara lina tija gani kwa mlala hoi!? Linaongeza mzunguko wa fedha mtaani!?.

Ongezeko lililofanywa kisiasa kwa kulenga 2025.

2025 we will murder someone, labda waweke mgombea mwingine.

You have my words.
 
Ongezeko la mshahara lina tija gani kwa mlala hoi!? Linaongeza mzunguko wa fedha mtaani!?.

Ongezeko lililofanywa kisiasa kwa kulenga 2025.

2025 we will murder someone, labda waweke mgombea mwingine.

You have my words.
Hakuna rais anayeweza kukuwekea pesa mfukoni mwako, utaendelea kulialla mpaka mwisho wa maisha yako.

JPM aliambiwa na wanyamwezi ndugu zake kwamba mzee huku kwetu kuna njaa sana!, akawaambia njaa mnataka nije niwapikie chakula nyumbani kwenu?. Hilo ndilo jibu la halali la kumpa mtu mvivu anayelialia siku nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…