Azzan Zungu ataka mazungumzo Bandari ya Bagamoyo kunusuru tatizo la ajira

Bandari ya Mtwara ina kina kirefu sana.kuliko bandari zote ukanda huu wa A. mashariki .Kama swala nikuwezesha meli kubwa kupakia na kushusha mizigo pale Bagamoyo Nivema zadi ingeboreshwa bandari ya Mtwara kwa gharama nafuu. ambayo ina kinakirefu sana asilia cha maji kuwezesha meli yenye ukubwa wowote duniani kuweza kutia nanga pale
 
Mkuu, siupingi mradi wa Bagamoyo, siupendi kwa ninayosikia yakisemwa kwamba yamo ndani ya mkataba wa ujenzi huo. Kama ni kweli, nitaendelea kuupinga sana.

Nimenukuu hayo maneno yako hapo juu kuhusu manufaa yatakayotokana na mradi huo.
Hivi Tanga na Mtwara haiwezekani nako tukahimiza manufaa haya yawepo? Kuna vizuizi gani!
 

Itakuwa makosa makubwa sana kuwapa China bandari hii watu hawajui haitakuwa bandari yetu itakuwa ya china. Kama kweli tuna nia tukope tujenge parks wenyewe
 
Mhh!! kushindikana au kusitishwa kwa mkataba wa bandari maelezo yalikuwa ni mkataba usio na maslahi kwa wananchi na serikali ya tanzania je sasa hivi unatija?

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Suala la kujenga bandari sio baya, ila waweke mkataba hadharani watu wote wausome kama alivosema Prof Assad.
Hakuna Jambo limetokea likakubaliwa na wote au kukataliwa na wote,hata ukioneshwa huo mkataba unaweza ukaukubali Mimi nikaukataa

Sio kila Jambo liwekwe hadharani,Kuna vitu vingine vinahitaji usiri kidogo ili Mambo yaendelee, serikali tumeichagua wenyewe kwa mujibu wa katiba tuiache halafu baada ya miaka 5 ijipime Kama inatufaa au la.

Kutokujua kwako ndio furaha yako!
 
Kama mradi wa Trilioni 20 utashindwa kufikisha maximum capacity kwa miaka 33 basi unapaswa kukimbiwa kama ukiwa. Dar port na madhaifu yake ukiangalia record zake imeweza kufikisha zaidi ya Trilioni 20 miaka 15 tu iliyopita, sasa kwa vipi Bandari ya Bagamoyo ihitaji zaidi ya miaka 33? Tena kwa sifa yake kedekede ya kuingiza mimeli mikubwa ya mizigo!!

Kalagabaho
 
Tanga na Mtwara mbona zinapanuliwa kitambo tu lakini ujenzi unaenda taratibu sana sababu bajeti ipo stretched sana.

Sababu kubwa ya Bagamoyo ni muwekezaji ndio ameonyesha opportunity hapo sio kwamba pesa ni yetu tunaweza amua wapi iwekwe. But maadam ni Tanzania hakuna hasara yoyote hta Gesi ipo mtwara but inachakatwa Dar!!

Bagamoyo kwa maoni yangu ipo karibu na social amenities nyingi kwa uwepo wa Dar tu mfano SGR, Airport kubwa, service sector karibu yote imejikita Dar (Bima,logistics etc) so Bagamoyo itakua kma extension tu ya jiji la Dar but kwa Mtwara inabidi mpka lami zijengwe, Airport zitanuliwe, mfumo wa Reli na vitu kibao vianze kujengwa upya so inakuwa disadvantage kwa uwekezaji mkubwa kama huo.
 
Angalau jana niliona Wakenya wanaandamana kutaka mikataba ya ujenzi wa SGR iwekwe wazi...japo wameishachelewa,
" ...akili zangu ndogo huwa zinajikita kwenye uadirifu wa hawa wanaochombeza kuhusu huu mradi, kwanini wote ni watu wenye rekodi zenye utata kwenye utumishi wao?..."
 
Mtaji wa Trillion 20 sio mapato usichanganye.... Yaani unasema bandari ya Dar imewekeza mtaji wa trillion 20 ndani ya miaka 15??? Unaweza nipa source ya hiki?

Wakati bado unatafuta source.... Sheria ndio inaruhusu mpaka miaka 99 na kuna wawekezaji wengi tu wanapewa hivyo sasa sielewi kwanini inageuzwa kma ni mara ya kwanza. Nmekueleza hapa hta wakatoliki wame lease ardhi kibao kwa hati za 99 years! Ila sioni mapovu kwamba nchi imeuzwa Vatican? It's really weird.
 

Mkuu zitto ulikuwa wapi muda wote huo!! Big up sana!
 
No to Bagamoyo Port. Big NO! Bado hamjaweza kueleza kwanini mnafikiri bandari zetu 3 hazifai hivyo tuingie mkataba wa kuwapa watu wajenge bandari mpya ambayo siyo yetu. Magufuli alikuwa na mapungufu mengi sana lakini kwenye hili la bandari alikuwa sahihi mno. Huwezi kuipa nchi ya kigeni lango la kuingia kwenye nchi yako walimiliki. Ni hatari sana. Bandari tulizo nazo zikiboreshwa zitakuwa na manufaa mara milioni moja kuliko hili wazo la kuuza nchi.
 
Mbona hili rahisi kueleweka, kama Trilioni 20 ni uwekezaji mwekezaji anategemea kuzirudisha na hazirudi kama mana toka juu, ni mapato. Sasa unampaje mwekezaji miaka 99 kuendesha mradi wa Bandari kwa kuzingatia mantiki hiyo hapo juu!

Mfano wako na ardhi inayohodhiwa na Wakatoliki ni kama mwanga na giza. Wakatoliki kama taasisi nyingine binafsi wamepewa ardhi kuendesha miradi yao kwa sababu huwezi kuendesha mradi bila ardhi. Kwa Bandari tunazungumzia sekta binafsi kuwekeza kwenye taasisi za uma mahali ambapo Serikali haina uwezo wa kuwekeza, hapa Bandari tunazungumzia maslahi ya Nchi moja kwa moja.

Hapa tayari tuna Bandari na mamlaka kamili ya usimamizi. Ndiyo sisi akina Yakhe tunauliza je, kuwekeza Trilioni 20 unategemea kurudisha pesa yako na faida kwa miaka mingapi? 99!!!?

Iweke akilini kwako, mradi wa Bandari si kama uwekezaji wa kiwanda. Kwa lugha rahisi ni kama atokee mwekezaji ajenge barabara ya Morogoro to Songea. Hii tutaita PPP na kwamba atapewa timeframe ya kurudisha chake. Ikiwa ni kiwanda tutampa lease ya miaka hata 99 na akishindwa biashara anaweza kuuza mitambo kama chuma chakavu ila kwa habari ya barabara hawezi kuondoa chuma cha madaraja wala kuzuia magari kupita.
 
Uchumi wa Singapore na Malaysia wanategemea bandari mkuu,kwa hiyo bandari ni mojawapo ya vyanzo vya mapato kwa asilimia kubwa vyenye uhakika kwa mwaka
Je, tulizonazo za mtwara, dar na tanga tumezu-utilize to the max mpk tuanze kuhangaika na bwagamoyo?
 
Sasa hapo upigaji wake uko wapi?

Umasikini ni mbaya sana
 
Haina haja ya kuwepo. Ziendelee kupanuliwa za Dar, Tanga na Mtwara.
Wanatumwa?????
 

Mkuu hiyo bandari ya Bagamoyo, hizo meli kubwa mnazosema hazitoenda Mombasa zitakuja Bagamoyo port ni Container Vessel tu. Kiuhalisia mpaka sasa Mombasa meli za container za mita 300+ wanapokea kwa nadra Sana inaweza ikawa kwa miezi 3 ikawa moja.

Ukanda wetu huu meli ya kontena yenye urefu wa Mita 300+ (Megamax) si Mara kwa mara maana idadi ya kontena zinazoshuka ni chini ya 2000.

Ukifatilia Kenya Shipping List ya 14 days hutoona meli za Mita 300+.


Bagamoyo port ikijengwa basi bandari tulizonazo zitabidi zifanyiwe Specialization ya meli na mizigo itayohudumiwa. Maana kwenye Dar/Tanga/Mtwara tuna terminal za aina zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…