Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Kuna tofauti kubwa kati ya sakata la Mwigulu na lile la David Bashite. Mwigulu (kwa maelezo yaliyotolewa) alirudia darasa na kutumia jina la mtu mwingine wakati akirudia. Utaratibu kama huo huko nyuma ulikuwepo sana; yaani watu walikuwa wanafeli halafu wanaenda kurudia kwenye shule nyingine. Kuna taarifa Profesa Muhongo alirudia mara saba kabla ya kufaulu! Kujaribu kuleta issue za akina Madelu hapa ni kumpa faraja ya muda tu Bashite!

Tuhuma zinazomkabili Bashite ni kwamba alifeli kidato cha nne (alipata ziro), akachukua (kununua?) vyeti vya mtu mwingine ndio akaingilia katika chuo cha uvuvi Mwanza na kuendelea hadi kuwa bosi wa chipukizi ya chama chetu, DC Kinondoni na sasa RC Dar es Salaam! Mkuu hapa kuna kesi ya jinai ambayo mtu akipatikana na hatia, na mahakama ikafanya kazi kama JPM anavyotaka zifanye, Bashite anakula mvua saba mapema tu. Yaani kiuhalisia wakati wewe unaleta andiko lako hapa Bashite alitakiwa awe anamalizia kuandika maelezo polisi tayari kwa kufikishwa kortini kujibu jinai nyingi ambazo ziko ndani ya sakata hilo!
Nina swali hivi vyeti au hii process ya kununua majina au nafasi uwa inagharimu kiasi gani? Na je form 4 Makonda ambaye anatoka familia maskini sana aliwezaje kupata hela ya kununua hiyo nafasi/jina/cheti?
 
Mwigulu alishaeza hapa kwamba yeye alirudia shule ndo akapewa jina la mtu aliyeacha shule akafanyia mtihani na akafaulu. Tofauti na huyu Bashite anayedaiwa kufeli kisha kanunua cheti cha mtu aliyefaulu mtihani huo ulomshinda kaifanya yake. Kagushi cheti. Kugushi cheti cha mtu ni kosa la jinai. Kuhusu Kigwangala sina maelezo ya kina.

Mnaweza kuibua mambo mengine,kutumia jina lisilo lako ni kosa la jinai.Repeaters kipindi kile si kwamba sharia ilikuwa inaruhusu,hapana.Walikuwa wanawahonga walimu wakuu na maafisa elimu.Hilo lilikuwa ni kosa la jinai na bado linaendelea kuwa kosa la jinai.Kama ukitaka kurudia shule baada ya kushindwa darasa mtihani wa darasa la saba si ungeanza darasa la kwanza kwa jina lako hilo hilo?Kwanini udandie darasa la 5,6 au 7 kwa kutumia jina la mtu mwingine?Tukitaka kuhakiki majina ya repeaters kazini,si ajabu watumishi serikalini wakabaki nusu🙁
 
Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.
Mbowe anaitwa Daud au, Au ana ka certificate kake maana siyo Dr lakni ni ka kwake, Kigwangala inajurikana wazi intern hakufanya na siyo ishu sana. Lameck bado si shida, huyu sasa wa huko mjini kwenu amekuwa mdharirishaji na kuwaita wenzake ma Bashite ili hari yeye ni no moja. Asisemwe ili? Aje hadharani au aende BAKWATA akatoe clarifications tumuelewe.
 
Sasa hivi watanzania tunaugua ugpnjwa unaoitwa diploma disease ya kufikiria kwamba utendaji wa mtu unahusiana na cheti cha darasani sasa tunajikuta tunadai huyu proffesor si lolote si chochote kumbe ni proffesor wa physics au chemistry na alitakiwa afunfishe watoto wetu chuo kikuu lakini tukamuondoa kumweka kwenye siasa tukampa wizara ya wanyama pori ashindane na mbunge wa darasa la saba wa wizara ya jinsia na ushereheshaji. Nitakapokuwa Rais nitahakikisha maprof wote wanarudi kwenye fani zao kuongeza ufanisi kwenye sekta husika na siyo bla bla kwenye majukwaa
 
Mmseahau kuwa hili suala la uhakiki wa vyeti limeletwa na serikali ya awamu ya tano.

Acheni mawe yote yafunuliwe hatuwezi kuwa na RC mwenye tuhuma nzito kama hiyo
Jamaa hana aibu, anaendesha kikao kweli ofisi bila aibu mbele ya wasaidizi wake? ingekuwa mimi ningeachia ngazi.
 
Siku zote hizo jumlisha kuanzia hiyo ishu ilipoanza tayari wameshaanza kufanya yao,kama waliweza kufoji sahihi ya karume na kupeleka bungeni itakuwa huyo mwana mpendwa wa mwanasiti
 
Kwa upande mwingine tukimjibu mleta post kama anavyotaka ni kama Daudi alivyomtaja Wema akamuacha Agnes, over and out.
 
Mbowe alizungusha form 4 na sio six, aeleze na yeye aliingia vipi A level ?
Duh ,umenishangaza!
Ina maana hujawahi ona waliofeli form 4 , wakarudia mitihani na wakaendelea A level?

Mbona ni vitu vya kawaida hivi!
 
Bwana mkubwa ajipime:
Mhariri: “Mheshimiwa habari?”
RC Makonda: “Unadhani majibu ya swali hili yatamtoa Manji kwenye kesi ya dawa za kulevya?”
Mhariri: “Mheshimiwa, hilo linakujaje, sisi tunataka kujua kuhusu wewe?”
RC Makonda: “Nasema hivi, unadhani majibu ya swali hilo (kuhusu elimu yake) yatasaidia kumtoa Manji kwenye kesi ya dawa ya za kulevya? Huna akili wewe.” Alisema Makonda kisha akakata simu.

Hata hivyo, sekunde chache baadaye alipiga tena simu na Mhariri alipotaka ufafanuzi zaidi, Makonda alisema: “Na nisikie unamtisha au kumnyanyasa huyu mwandishi (Salha),” kisha akakata simu.

Mwandishi alivyouliza
Akisimulia alivyomfuata Makonda ili kumuuliza swali hilo baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari Kisarawe 11 wilayani Kigamboni, Salha alisema alimuomba pembeni Mkuu huyo wa Mkoa ili amuulize swali hilo.

Kwa mujibu wa Salha, Makonda hakuwa na shaka na alikubali ombi hilo lakini baada ya kuulizwa swali hilo, Mkuu huyo wa Mkoa aliomba nafasi ili amjibu Mhariri moja kwa moja kupitia simu yake (mwandishi) na mwandishi huyo alitii. Mahojiano ya Salma na Makonda yalikuwa kama ifuatavyo;

Mwandishi: Shikamoo.
RC Makonda: Marahaba.
Mwandishi: Kuna taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba unatumia cheti cha mtu cha sekondari, taarifa hizo ni kweli?
RC Makonda: Amekutuma nani?
Mwandishi: Nimetumwa na ofisi, bosi wanngu amenituma.
RC Makonda: Mpigie nimjibu.

Ndipo mwandishi akampigia Mhariri wa Habari naye alipokea simu hiyo na kutoa majibu aliyotoa.

Akizungumza tukio hilo, Salha alisema majibu ya Makonda yalimfanya ashangae kwa kuwa hakutegemea jibu alilosikia
 
leteni vyeti kwanza.
Sisi tunavyo vyeti vyetu vya kitaaluma sasa nyie mnao sema mnajua Makonda ana vyeti vya mtu mwingine ndiyo tunataka mtuwekee hivyo vyeti alivyonunua hapa ili tujiridhishe na haya maneno na msibadili mada
 
Nyinyi wote mnaomtetea Bashite Daudi, msaidieni basi kukanusha huo uvumi ila muwe na evidences za kutosha maana mhusika mwenyewe naona yupo kimya tu, hana la kujibu labda nyiyi mtakuwa mnajua zaidi ya mhusika mwenyewe. Kama sivyo hebu nyamazisheni hivyo vinywa vyenu. Kaeni kimya!!!!!!!
Mkuu mimi nafikiri kitu kikubwa kuliko vyote ni kuthibitisha kuwa Daudi Bashite ndio Paul Makonda, kama hakuna ushahidi sio vyema kumtuhumu mtu, hata ungekuwa wewe usingependa kufanyiwa hivyo. Usimfanyie mwingine kitu usichopenda kufanyiwa.
 
Sisi tunavyo vyeti vyetu vya kitaaluma sasa nyie mnao sema mnajua Makonda ana vyeti vya mtu mwingine ndiyo tunataka mtuwekee hivyo vyeti alivyonunua hapa ili tujiridhishe na haya maneno na msibadili mada
Nenda kwa Gwajima anavyo
 
Mbowe anaitwa Daud au, Au ana ka certificate kake maana siyo Dr lakni ni ka kwake, Kigwangala inajurikana wazi intern hakufanya na siyo ishu sana. Lameck bado si shida, huyu sasa wa huko mjini kwenu amekuwa mdharirishaji na kuwaita wenzake ma Bashite ili hari yeye ni no moja. Asisemwe ili? Aje hadharani au aende BAKWATA akatoe clarifications tumuelewe.
Mbowe alizungusha form 4 akaingia A level kwa njia za panya, napo akazungusha pia ZERO. Tangu lini form 4 failure akaingia A level, muombe Mbowe atoe vyeti vyake.
 
Mwambie ajitokeze aoneshe vyeti vyake halali.

Isije kuwa kodi zetu zinatumika kulipa mshahara mtu aliyenunua cheti.
Wewe mwenye tuhuma zake ndiyo weka ushahidi wa hizo tuhuma zake za vyeti vyake hapa.

Yeye hana shida yuko kazini toka awamu ya NNE ya uongozi wa Mzee Kikwete na hivyo vyeti vyake.

Weka ushahidi hapa kuhusu vyeti tuone which is which
 
Sisi tunavyo vyeti vyetu vya kitaaluma sasa nyie mnao sema mnajua Makonda ana vyeti vya mtu mwingine ndiyo tunataka mtuwekee hivyo vyeti alivyonunua hapa ili tujiridhishe na haya maneno na msibadili mada
vyeti vinahakikiwa....mwambie akanushe usimsemee !
 
Back
Top Bottom