Ndiho
JF-Expert Member
- Feb 23, 2013
- 2,306
- 1,536
Ninaamini wewe kama ni unyumbu ndiyo "Linyumbu lililokubuhu",Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.
(1) Tuhuma ya Waziri Mwigulu alijitokeza, akafafanua na kuonyesha uma kitu kilichotokea.
--- Makonda kimyaaa, huu ukimya maana yake nini?
(2) Tuhuma ya Mbowe ni tofauti kabisa na ya Mwigulu na Makonda.
Mbowe alifeli F6 na iko wazi kama wengine walivyofeli. Lakini Mbowe hakuridhika na matokeo yale, akarudia mitihani na kuendelea hadi kupata elimu ya juu ya pale alipofeli. Unalinganishaje na aliefeli na kuchukua cheti cha mtu mwingine?
Kama umekuja kumtetea Makonda ulipaswa uonyeshe namna ambavyo alisoma kwa utaratibu na hakutumia vyeti vya mtu mwingine. Kuita watu nyumbu inaweza kuonyesha hata wewe hukufaulu na pengine kama umepata elimu unaweza kuwa umetumia vyeti vya mtu mwingine