Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Tofauti ya Mwigulu na Daudi Bashite ni kwamba mwigulu ni mstaarabu Daudi ana kiherehere cha hatari na mlevi wa madaraka na ndio maana tunamuandama. Daudi akipewa cheo cha mwigulu watanzania uwe ccm au upinzani tutakoma.
 
Mkuu mimi nainunua amani Kwa namna yeyote,nikuulize wewe hili neno chakaza katika kiswahili fasaha umekusudia nini???na kwa mantiki gani haya uniulize suala Hilo,unakusudia nini?
Huoni kuwa unaweza kumpandisha mtu hasira hapo mwisho naye afanye press conference
 
Na hawa wanaotetea huyu RC hembu tuwe wakweli hivi huyu RC na kile kiherehere chake ingekuwa anayetuhumiwa na hili sakata la ununuzi wa vyeti angekuwa yupo pale ofisi ya mkuu wa Mkoa mtumishi mweye issue kama kwa hurka za Daudi Albert Bashite si tayari angekuwa central ana siku kadhaa hata bila ya mahakamani.
Mtumishi anaajiriwa kwa kutumia vyeti vyake, Je mkuu wa mkoa unahitaji cheti ?
Vipi kuhusu suala la Mbowe kuingia A level huku amezungusha form 4 na A level penyewe si haba akazungusha tena ZERO. Je tangu form 4 failure anaruhusiwa kuingia A level ?
 
Na hawa wanaotetea huyu RC hembu tuwe wakweli hivi huyu RC na kile kiherehere chake ingekuwa anayetuhumiwa na hili sakata la ununuzi wa vyeti angekuwa yupo pale ofisi ya mkuu wa Mkoa mtumishi mweye issue kama kwa hurka za Daudi Albert Bashite si tayari angekuwa central ana siku kadhaa hata bila ya mahakamani.
Angekoma.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya sakata la Mwigulu na lile la David Bashite. Mwigulu (kwa maelezo yaliyotolewa) alirudia darasa na kutumia jina la mtu mwingine wakati akirudia. Utaratibu kama huo huko nyuma ulikuwepo sana; yaani watu walikuwa wanafeli halafu wanaenda kurudia kwenye shule nyingine. Kuna taarifa Profesa Muhongo alirudia mara saba kabla ya kufaulu! Kujaribu kuleta issue za akina Madelu hapa ni kumpa faraja ya muda tu Bashite!

Tuhuma zinazomkabili Bashite ni kwamba alifeli kidato cha nne (alipata ziro), akachukua (kununua?) vyeti vya mtu mwingine ndio akaingilia katika chuo cha uvuvi Mwanza na kuendelea hadi kuwa bosi wa chipukizi ya chama chetu, DC Kinondoni na sasa RC Dar es Salaam! Mkuu hapa kuna kesi ya jinai ambayo mtu akipatikana na hatia, na mahakama ikafanya kazi kama JPM anavyotaka zifanye, Bashite anakula mvua saba mapema tu. Yaani kiuhalisia wakati wewe unaleta andiko lako hapa Bashite alitakiwa awe anamalizia kuandika maelezo polisi tayari kwa kufikishwa kortini kujibu jinai nyingi ambazo ziko ndani ya sakata hilo!
Peleka ushahidi ili afungwe
 
Mbona unakuwa mzito kuelewa.

Unataka tuweke cheti gani?

Unaambiwa Hana cheti cha form four kwani alipata ZERO.

Ila cha ajabu ana degree kwahiyo tunataka atuoneshe cheti cha form four kilichompa sifa za kuendelea na masomo baada ya kupata ile zero.


Wewe mwenye tuhuma zake ndiyo weka ushahidi wa hizo tuhuma zake za vyeti vyake hapa.

Yeye hana shida yuko kazini toka awamu ya NNE ya uongozi wa Mzee Kikwete na hivyo vyeti vyake.

Weka ushahidi hapa kuhusu vyeti tuone which is which
 
Mwigulu alishaeza hapa kwamba yeye alirudia shule ndo akapewa jina la mtu aliyeacha shule akafanyia mtihani na akafaulu. Tofauti na huyu Bashite anayedaiwa kufeli kisha kanunua cheti cha mtu aliyefaulu mtihani huo ulomshinda kaifanya yake. Kagushi cheti. Kugushi cheti cha mtu ni kosa la jinai. Kuhusu Kigwangala sina maelezo ya kina.
Kaghushi una ushahidi?
 
Si ndio,dhambi zote zisingekuja kama sio kupindua madaraka ya meya kuongoza jiji la Dar,ambaye amechaguliwa na baraka za wabunge waliochaguliwa na wananchi wa jiji la Dar,Huyu hafai anarekodi mbaya huko nyuma,Kodak lake hata angeweza kufungwa,Kwa vile alivyomvamia Mzee Warioba,amekosa heshima huyu,hafai kuongoza.
Abuha una uhusiano gani na Meya, mbona unalia lia tu ? Meya ana kazi zake, RC ana kazi zake na Mbowe ana kazi zake, kama inshu kuhusu vyeti vya Meya ilete hapa, vinginevyo hapa tunahoji kuhusu vyeti vya RC na Ndugu Mbowe, Waziri Mkuu kivuli, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
 
Huoni kuwa unaweza kumpandisha mtu hasira hapo mwisho naye afanye press conference
Huko ndio uungwana,Mimi ndio ninavyotaka,ili ukweli ujulikane,Ile Miaka ya kuwadumaza wananchi imepitwa na wakati,maendeleo haya hayatoweza kuja bila ya ukweli na haki kwa wananchi,
 
wewe umetumwa kumsafisha cha msingi mwambie atoe vyeti vyake hadharani ili kuua maneno ambayo aidha ya wabaya wake au wasema kweli,binafsi hata ikiwa ni kweli mteuzi wake au wanyumbani hawezi kumtumbua kwani ni mtu ambaye amekuwa akimpa sifa kupitiliza na itaonekana uteuzi wake alikosea lakini kuzuri msg sent & delivery,nchi hii hakuna msafi hasa ccm!
Hana shida ya kuonyesha vyeti hadharani ataionyesha mahakamani akitakiwa kufanya hivyo. Anayejua nani msafi nani mchafu ni mungu pekee kwani matendo mengi machafu hufanywa kwa siri.
 
Ngoja nichukue nafasi nisubiri 30 days
 
Mbowe ana tuhuma ya kugushi vyeti au cheti?, umewahi kusikia sehemu mbowe alitumia cheti cha mtu cha primary, au sekondary? Kama alifeli hata kama ni kwa kupata zero na kakomaa na zero yake hiyo mpaka sasa au kajiendeleza kwa mifumo mingine rasmi hiyo haituhusu, hata makonda kufeli kwake siyo hoja haoja kubwa hapa ni kutumia cheti cha mtu kinyume cha sheria. Kwa issue ya kufeli mbona olesendeka hashambuliwi na ana zero mbona kibajaji hashambuiliwi? Hapa hoja ni kutimia cheti cha mtu siyo kufeli kwani yeye kawa wakwanza kufeli?
Hao wote wana ushahidi katika cv je umeiona cv ya makonda inayoonyesha kafoji au kwa mujibu wa gwajima?
 
Back
Top Bottom