Baada ya kuweka koma kwenye orodha ya kwanza ya Mawaziri, Rais Samia asema atatangaza orodha mpya karibuni

Baada ya kuweka koma kwenye orodha ya kwanza ya Mawaziri, Rais Samia asema atatangaza orodha mpya karibuni

Una uhakika gani atakao wachagua siyo wanafika
 
Nikuombe Mheshimiwa Rais kwa upande wa mawaziri na manaibu naomba usimpe Yeyote hata aliyewahi shika akatolewa na Magufuli


Fumua wote kasoro wanne tu nao ni Ummy Mwalimu, Lukuvi, Profesa Mbarawa Na Stagomena Tax


Wengine wanafiki tu wachumia tumbo Mioyo yao kigeugeu na wapo kuvizia fursa tu
Alaa!!, Leo unawakana sukuma gang wenzio!? Bado mtanyooshwa sana
 
Naunga mkono hoja ila kwa upande wangu nataka afanye hivyo ili akose wa kumtupia lawama.
Kweli Kama yule katibu wa wizara ya fedha mteule wake,aliyeidhinisha mamilioni ya posho.PM alikwenda amefura alifikiri Hangaya ni JPM.
Mpaka Sasa kimia.
 
Hilo la kuvunja baraza la mawaziri wa Magufuli tulisema toka alivyokalia hicho kiti cha zali la mental. Nyie ndio mnaamka sasa wakati wahuni wameanza kumpa ukweli wake!? Nadhani sasa mtajiona mlivyo na akili zilizosinzia.
 
Nashauri avunje serikali nzima aweke wapya kabisa.

Angevunja toka mwanzo kama tulivyosema angepata haiba nzuri. Ila sasa anaonekana anavunja kwa jazba baada ya kuambiwa ukweli.
 
Nikuombe Mheshimiwa Rais kwa upande wa mawaziri na manaibu naomba usimpe Yeyote hata aliyewahi shika akatolewa na Magufuli


Fumua wote kasoro wanne tu nao ni Ummy Mwalimu, Lukuvi, Profesa Mbarawa Na Stagomena Tax


Wengine wanafiki tu wachumia tumbo Mioyo yao kigeugeu na wapo kuvizia fursa tu
Lukuvi naye aondolewe tu. Wizara ya ardhi ipelekewe damu changa yenye kujua changamoto za sekta husika. Ninaamini wapo akiwatafuta atawapata
 
Kabudi,dotto,waitara,katambi out bashe anakuwa waziri kamili kigwangala anapewa wizara dr.samizi analamba uteuzi ndalichako anabadilishwa wizara
Kigwangala atakuwa anahangaika sana huku na huku kusaka nazi
 
Wakuu heri ya mwaka mpya...

Kama tulivyo msikia Mama akisema kuwa hivi karibuni atafanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri
Je kwa mtazamo wako wakiutendaji kwa mawaziri hao
Je ni nani anafaa kubaki kwenye baraza ilo na ni nani anafaa kuondolewa kwenye baraza hilo

Aya twende kazi..
Wa kwanza kuondolewa ni kassim majaliwa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Spika hata kama atabaki hatakaa apikike chungu kimoja tena na bi mkubwa.. Itakuwa ni mwendo wa kuwindana..
PM unaweza kumeza machungu lakini inategemea kama naye alikuwa na zake za chinichini atapigwa pini kimyakimya na kutakuwa pia kuna kuwindana kusikoisha..
In fact serikali ya CCM kuanzia sasa mpaka 2025 itakuwa ya burudani tupu.. Kama ikifanikiwa kufika lakini...

Mkeka wowote ujao hautaleta unafuu wowote bali utazidisha mkanganyiko chuki, makundi na kutafutana
Kama kuna kipindi walikuwa hawaaminiani kwenye maji sasa itakuwa mpaka kwenye salamu
Yajayo yana furahisha
 
Back
Top Bottom