Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Walikuwa wanapima upepo tu na hili tulilisema humu.

Mitandao ina nguvu sana!

Dr.Slaa sasa atapongeza uamuzi huu
Angekuwa fulani angesema tunapoteza muda wa kulima kwenye mitandao hivyo tutwangwe haswaaa na angeungwa mkono. Haya mzee Slaa tayari tangazo lingine limetoka wahi ukapongeze. Yani ukimaliza huu mwezi ukiwa balozi nenda katambike!

Hii ya Dr Slaa ilinipita, vipi ali support kupanda kwa gharama za bando za data?
 
Airtel hawajasitisha mpaka sasa vifurushi vipo juu
 
Kuna watu wanajiita magu2016 na countrywide sjui hapa watashangilia.

Kuwa kijana wa aina ya hawa watu inahitaji uwe ni mjinga na psychopathy wa hali ya juu sana.
Hao ni mazuzu tu na inaonekana ni kula kulala tu kwa shemeji zao.
Maana mtu anayetafuta fedha hawezi kufurahia upandishwaji wa ghalama za maisha.
 
Kila sababu ya kuipongeza serikali ipo hakika Kama itakua upande huu ndio itakua tafsiri halisi ya kuwajali wanyonge Kama wanavyojipambanua.

Huu ulikua ni aina nyingine ya kudidimiza kaki zetu Kama raia za kupata mawasiliano kwa garama rafiki.

Mungu amlaze kwema magufuli maana alikokua anatupeleka Ni kibra.
 
Tena mapeeemaaaaa
Wa kulaumiwa ni Dr Ndugulile ,hawa wanasiasa ndio wanaifanya serikali ilaumiwe, wanadhani wanaongoza wananchi wa stone ages 1890 wakati sasa hizi ni kidigital, ndio maana tulisisitiza mawaziri wawe wataalam wa eneo husika kama lengo lao ni kumuwakilisha Rais, how come Ndugulile atudanganye? Mama Samia ilitakiwa amfukuze haraka.
 
Katika hili.
Ndungulile's days at the ministry are numbered.
Hivi ndungulile Ni daktari wa falsafa PhD au wa COVID?
Maana baadhi ya PhD za bongo flavour Ni nzuri sana.
Yule ni Dr sio Dk
Medical doctor
 
Kwanza nakupongeza Rais Samia kwa kuwa muumini wa mitandao ya kijamii. Bila shaka malalamiko haya umeyapata huko.

Ombi langu (letu) usiishie kusitisha bei mpya bali pia wachukulie hatua za kisheria waliohusika ikiwa ni pamoja na Waziri husika na wafanyakazi wa TCRA
 
Mtetezi halisi wa wanyonge anaonekana sio yule mkandamizaji wa wanyonge aliyekuwa anajiita mtetezi wa wanyonge.Huko aliko sijui atakuwa mtetezi wa nani
Yaani kwake mnyonge alikuwa anatumika kama kitendea maovu
 
Watu wachache sana wanaelewa hili, lakini ipo siku watakuja kujua. Hakukuwa na haja yeyote ya serikali kusimamia sekta kama mawasiliano kwa kiasi hiki, let the market decide
Duniani kote juhudi kubwa zinafanyika kuwawezesha wananchi kutumia mitandao kwa bei nafuu na ziko sehemu ambako jitihada zinafanyika kuwezesha huduma ya mitandao kwa bei karibu sawa na bure. Hapa Tanzania tunacho chombo (TCRA) kisichozalisha kitu lakini watu wanalipwa mishahara mikubwa eti kwa kubuni njia za kuongeza gharama katika matumizi ya mitandao...ili kubana uhuru wa kujieleza? Ujinga mtupu.
 
Usitishaji huu onevu uendane na kutumbuliwa kwa waziri wake na manaibu.. itakuwa haijirudii rudii huu ni upuuzi wa Jiwe unaendelezwa na wajinga wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…