Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Hofu yao kuu zaidi ni Zanzibar mkuu.

Si vizuri kuwaachia CCM Zanzibar.
Hilo ndilo hitimisho la hoja hii, CCM inamwogopa Maalimu Seif na wanajua kuwa katika chaguzi zote za Zanzibar toka 1995 Nyerere alipoenda kubadilisha matokeo kwa nguvu, hawajawahi kumshinda Seif na wanaona bado anaushawishi mkubwa hivyo kumweka pabaya mgombea wa CCM.
 
Wanataka eti chadema wasimsimamishe Lissu badala yake wamsaport Membe this is unacceptable.
Kwa hiyo unachotaka wewe Act wamsapoti Lisu! Lisu hawezi kumbea uraisi maana atakua amewekwa ndani. kama unabisha subiri uone.
 
Kuna watu nnya zao zinapwita wakisikia vyama vya upinzani walivyojipanga kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2020.
 
Jana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe alitangaza rasmi kujiunga na chama cha ACT Wazalendo

Mchakato wa Membe ulianza zaidi ya miezi minne iliyopita huku serikali ikifuatilia kwa karibu

Baada ya hivi karibuni kujiridhisha kwamba atajiunga na kuna uwezekano vyama pinzani vikamsimamisha kuwa mgombea wao,serikali kupitia ofisi ya msajili ikaibuka na kituko cha mwaka kwa kuwaandikia ACT barua ya kuwajulisha nia ya kuwaadhibu...
Soma vizuri malezo ya msajili, acha kupindisha ukweli. wanachotakiwa ACT Wazalendo ni kukaa na ofisi ya msajili kumaliza hili kwa amani. ushahidi umetolewa na msajili namna ambavyo sheria imevunjwa.

Wakati mwingine weledi kwenye namna ya kufanya siasa bila kuvunja sheria ni muhimu sana.
 
Naona michezo ya kikachero imeanza,Hio ni Zuga tu ili ionekane ACT nao wanapitia Magumu kama ya Chadema.

HAKUNA HATUA ZOZOTE ZITACHUKULIWA DHIDI YA ACT.
Huu ni ubinafsi uliopitiliza! watu kama nyinyi hamueleweki mna malengo gani.
 
CCM mmepoteza miaka 5 mkipambana na upinzani, mkipewa tena nchi mtaendeleza huo uozo. Tatizo sio CCM ila ni mgombea mliyomsimamisha
 
Busara inahitajika katika usimamizi wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine. Tumeiona Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikishindwa kuisimamia sheria ya vyama vya siasa kikammilifu na sasa inachagua baadhi ya vifungu katika sheria ambavyo inaona vinaweza kuviumiza vyama vya upinzani.

Mbona kwa miaka mitano imeshindwa kukemea kusimamishwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasi ambapo ni ukiukaji wa sheria? Vyama vilihitaji kwenda kwa wananch ili kujinadi ili kupata wanachama wapya.

Watanzania ni binadamu kama binadamu wengine katika dunia hii. Mwal, Nyerere aliwahi kuonya kuwa Watanzania tusijidanganye kuwa sisi si sawa na Somalia, Kenya nk na akasema tunapaswa kama tuna amani kuilinda kama mti kwa kuumwagilia maji ili uweze kendelea kuwepo. Ubabe unaweza kutuondolea amani yetu.
 
Basi tena lissu sio tishio dadeeki CCM inawaimbisha viiitikio tofauti!
Nadhani kwa ushetani huu ni dhahiri kuwa mmewachoka Watanzania na hasa uvumilivu wao.
Nchi hii ni yetu sote, tunakaribia kuja kuwakumbusha hilo.

We shall overcome. Amen
 
Akifutie kwa kosa gani hasa?
Kosa hakuna na halipo lakini CCM wamemwamuru Msajiliccm aunde abuni atengeneze kosa feki awabambikie ACT wapate kuwakomoa kwa kuwafuta tu, CCM ya sasa ni waonevu watupu
 
Kosa hakuna na halipo lakini CCM wamemwamuru Msajiliccm aunde abuni atengeneze kosa feki awabambikie ACT wapate kuwakomoa kwa kuwafuta tu, CCM ya sasa ni waonevu watupu
Hawana ubavu wa kupambana kwenye uwanja SAWA.
 
Back
Top Bottom