Baada ya TPA kutangaza tenda kuhusu uwekezaji Terminal 2, Bado mnaamini Bandari zote zimeuzwa?

Usilete mambo ya kijinga kwenye jukwaa tukufu. Hilo tangazo mlilotoa mnafikiri Watanzania ni wajinga? Hiyo kampuni ya Adan Group mliyoipa mktaba kinyemela walikuwa vibarua kusafisha gati?

Mmeuona mziki wa Watanganyika wasiopenda masihala ulivyowachezesha dansi mkaona hili likija kugundulika tutakatwa shingo ndio mnajifanya kutangaza tenda?

Lazima serikali itamke hadharani na kwa maandishi kwamba mkataba na DP World umefutwa ndio Watanganyika wataamini kinyume na hapo hakuna wa kudanganywa tena.
 
Umeishia darasa la ngapi? Kama unasubiri mkataba wq DP ufutwe mwambie Mungu akuchukue tu maana nakuhakikoshia haufitwi
 
Mngeendelea kuishupazia shingo TEC na ilivyojipanga ni zaidi ya ccm ya lowasa

Tundulisu mkatolic yule ,pangeiva
 
TPA wanatangaza kumtafuta mwekezaji wakati tayari kuna makubaliano na DPW? Kama makubaliano hayajavunjika, basi wenye dhamana katika nchi hii wanafanya issues muhimu za kitaifa katika kiwango kidogo sana cha kufikiri. Tangazo la kutafuta mbia na yale makubaliano ya IGA yanapikika chungu kimoja?
 
Wewe ni mmoja wa wale waliopotoshwa. Mmemuogopa DP World bila ya sababu zozote za msingi. Eneo lake ndani ya JMT ni gati namba tano mpaka namba saba, ambayo ni asilimia nane tu ya eneo lote la bandari la Tanzania.
 
Mantiki ya huu uzi ni kuwapa elimu kuwa hakuna bandari iliyouzwa wala kugawiwa.

Makubaliana ya Tanzania na Dubai yanahusu uwekezaji katika Terminal 1 hasa gati 0-7. Hii ni sehemu ndogo sana ya Bandari ya DSM.

Ndo mana TPA amekaribisha uwekezaji mwingine katika Terminal 2

Waliowaambia sijui hakuna national sovereignty sijui bandari za maziwa na bahari zimegawiwa walikuwa wanawaokota na kuwadanganya vilaza nyie alafu mnapayuka tu
 
Wamesanda kwa wa-TEC.DP WORLD byebye.
 
Inabidi uje na uthibitisho wa kuthibitisha hizo kelele zako kwamba wanaopinga vipengele vya mikataba wamehongwa au wana maslahi binafsi, hilo halibadilishi ukweli kwamba bibi yenu anataka kugawa mali zetu kipumbavu kabisa
 
Wamesanda kwa wa-TEC.DP WORLD byebye.
DP World bye bye kivipi?

Kwa ujinga wenu huo hata hamjui kusoma na kuelewa vitu ndo mana hao wanasiasa na maaskofu wanawapelekesha kama makaratasi
 
Kwa kweli nilijua unashusha vitu, kumbe umeandika kwa mapenzi yako.
Watanzania wameelimika miaka hii.
 
Kasome part II ya IGA, kama huna nikupatie, huwa unapoteza muda kuandika ujinga!

Bunge limeshakataa kupokea muswada wa mabadiliko ya sheria ya Maliasili na Ile ya mikataba ya Maliasili, ambayo ililenga kuaccommodate IGA,

Huoni kwamba sauti zimesikika kwamba Kuna uhovyo ulikua unafanyika?
Bado unaamini Rais ameuza bandari zote na bahari, mito na maziwa?
 
Part 2 ya iga inahusu Terminal 1. Muswada wa Sheria ya Maliasilia hauhusiani na uwekezaji wa Bandari. Shida yako nini?
 
DP World bye bye kivipi?

Kwa ujinga wenu huo hata hamjui kusoma na kuelewa vitu ndo mana hao wanasiasa na maaskofu wanawapelekesha kama makaratasi
Kwahiyo DP world atafanya kazi nchini kinyume Cha sheria zetu? Kwa mujibu wa sheria yetu ya mikataba ya 2017 disputes zitaamuliwa na mahakama zetu, Kwa Mujibu wa IGA, zitaamuliwa Kwa sheria za Uingereza na center of abitration ni SA. Bunge limegoma kupokea mabadiliko ya Sheria ili kuweza kusuit mkataba na DP world. Ama Hilo hujui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…