Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

umeleta historia nzuri kwa vizazi vya sasa....wazee wetu walifedheeka sana na kuuwawa kwa viwanda hizi kwa ukosefu wa uzalendo na ubinafsi wa walielimishwa na kuamniwa na taifa hili
Kweli kabisa !!
 
Hakuna sababu yeyote ya maana iliyokuwepo wakati ule !! Ndio maana yeye mwenyewe Mkapa alikiri kwamba kosa kubwa analolijutia zaidi katika utawala wake ni kuvibinafsisha viwanda hivyo !!
 
upo sahihi sana, ilifikia rasimali za viwanda kama magari, matrekta etc yanatumika kijamii zaidi yaani kulima kwenye masham,ba ya wafanyakazi, magari ya umma na dereva kuhudumia familia za mabosi muda wa kazi, viongozi wa mashirika walijilimbikizia mali kifisadi toka hayo SU, ajira za kindugu bila tija wala professional. u-god father ulitawala
 
Mwadui kulikuwa na lami na mabasi yalikuwa yanazunguka bila abiria kulipa nauli.
Kwa walioishi mgodini enzi hizo mgodi wa Mwadui ukiwa Mwadui kweli wanasema maisha yalikuwa kama Ulaya.

Hadi maziwa walikuwa wanaletewa kwenye chupa mlangoni kila siku kama London.
 
Mwendazake wakati anazindua soko Morogoro alimuumbua Abood,alimwambia umepewa viwanda lakini umekaa navyo kwa miaka 24 na hujafanya lolote,si bora uvirudishe kama umeshindwa.
 
Nasikis kwenye NBC,Mwakyembe alikuwa mmojawapo ya wanabodi,alipinga sana Bank isiuzwe,wakaamua kumtoa nje na kumfukuza
 
Vinaweza kurejea, iwapo watu wenye mitaji (matajiri) watakaa meza moja na wapanga sera.
 
umeleta historia nzuri kwa vizazi vya sasa....wazee wetu walifedheeka sana na kuuwawa kwa viwanda hizi kwa ukosefu wa uzalendo na ubinafsi wa walielimishwa na kuamniwa na taifa hili

..siasa za ujamaa.

..Urasimu wa serikali.

..uzembe wa wafanyakazi waliokuwa wakilindwa na viongozi wa Ccm viwandani na kwenye mashirika.
 
Shinyanga vilikuwepo viwanda vya kusindika pamba na kukamua mafuta vya SHIRECU ! Shinyanga region cooperative union !!

..vilishindwa kuzalisha ndio maana kulikuwa na uhaba wa bidhaa muhimu nchi nzima.

..watu walikuwa wanapanga foleni kwa ajili ya sukari, mafuta, mkate, sembe, mchele, ngano, etc halafu mnasema tulikuwa na viwanda?!

..Na iliwachukua miaka mingi kuuza viwanda na mashirika. Viwanda vingi viliuzwa miaka kadhaa baada ya kusimama uzalishaji au kufungwa.
 
Hizi ni sababu za kuhalalisha hayo Angejenga discipline na uwajibikaji visingesimama?
 
Hapo ndipo kuna makosa makubwa kimtazamo wa sababu ya kuviuza, haikuwa eti ni kumnufaisha mnunuzi tu. Ni ili mnunuzi ahakikishe anavirekebisha viweze kuanza kuzalisha kwa manufaa ya Taifa, haswa kiteknologia. Sasa unapouza kiwanda cha serikali halafu hakuna kipengele kama hicho cha kuhakikisha kinabakia kuwa na manufaa kwa Taifa, then huo ni ubadhirifu wa mali ya umma.
Kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba serikali yake ilitakiwa ijenge vipya vilivyo bora zaidi ndipo waviuze hivyo vilivyoundwa na Mwalimu, ili aonyeshe umahiri wake. Kama baba yako amejenga nyumba kwenye kiwanja cha familia ukaona si nzuri kipindi cha utu uzima wako, unatakiwa ujenge ya kwako iliyo bora zaidi na siyo kuibomoa aliyojenga Baba yako.
Leo hii ukiuliza fedha iliyopatikana kwa kuuza hivyo viwanda vyoote zimelinufaisha je Taifa kiuchumi haielezeki hata kidogo. Nina wasiwasi Mwalimu Nyerere alipata msongo wa mawazo kutokana na maamuzi haya ambao huenda ndiyo uliosababisha kifo chake. Hotuba ya Mwalimu Nyerere wakati wa kumteua inatosha kuthibisha hilo, it is beyond any reasonable doubt kwamba hili lilisababisha maumivu kwa Baba wa Taifa.
Ilikuwa ni muhimu maamuzi haya kujadiliwa kwa kina hata na Bunge. Vyuo vikuu tulikuwa navyo vilitakiwa vishirikishwe kufanya research ya nini kifanyike, vyuo kama UDSM, DIT, Arusha Tech, Sokoine University, Mzumbe, Chuo Cha Biashara DSM nk. walitakiwa wataalamu wapitie mkakati huo na kutoa ushauri. Unapokuwa kiongozi usiependa kushauriwa na unaishia kufanya maamuzi ya kubomoa uchumi wa nchi kiasi hicho, basi uwe tayari kushitakiwa kwa kosa la ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Kuna mtu amesema eti Baraza la Mawaziri halihusiki moja kwa moja kutokana na mfumo wetu. Kwanini basi hakuna hata mmoja wao aliyejiuzulu ili kujitoa kwenye huo ubadhirifu? Ina maana maadili ya uongozi hakuna.
Kitendo hicho kililirudisha Taifa miaka 40 nyuma kiuchumi.
 

..serikali ya Raisi Mkapa ilikuwa haina fedha za kutoa huduma muhimu za jamii kama elimu, afya, etc sembuse kujenga viwanda vipya.

..Kulikuwa na ukata mkubwa wa fedha uliotokana na makusanyo madogo ya mapato ya serikali, pamoja na mzigo mkubwa wa madeni ya ndani na nje.

..Zaidi ya matatizo niliyoyaeleza hapo juu kulikuwa na tatizo la mzigo wa gharama za kuhudumia viwanda na mashirika ya umma ambayo yalikuwa hayawezi kujiendesha.

..Katika mazingira kama hayo nadhani sio sahihi kuilaumu serikali ya Raisi Mkapa kwa kutokujenga viwanda vipya, au kuvifufua vile vilivyokufa wakati wa awamu ya 1 na ya 2.
 
Hiyo siyo sababu ya kuua na kuuza viwanda vyoote hivyo. Wapi uliona upembuzi yakinifu uliotumika kufikia uamuzi huo? Huwezi kuamua kuua viwanda na mashirika mengi namna hiyo. Kwanini asitembee kutafuta ushauri wa kitaalam hata nchi za nje? Kwa nchi ni afadhali ku-negotiate mikopo yenye masharti nafuu kuliko kuzima uchumi wa nchi nzima. Unatetea nini Mkuu wakati yeye mwenyewe alifika mahali akakiri hadhani kuwa alifanya makosa? Ila inakubidi ukumbuke kuwa wakati anakiri hilo alikwisha kuwaita waliopinga maamuzi yake jina baya "Makanjanja" . Hakuna kitu kibaya kama ulevi wa madaraka.
 
Ni kweli kabisa. Mwalimu alijitahidi sana.. hata kama viwanda alivyopewa/uziwa vilikuwa tayari vimepitwa na wakati. Laiti kama Mwalimu angelijuwa kuwa alikuwa anaongoza watu wa aina gani, angeamua tu kula bata kama Mobutu

Mosi.. watz wa nyakati zile, kama walivyo wa sasa hawakuwa watu wa kupiga kazi.. walijaa uvivu tuuu, kulalamika na uzembe. Ili viwanda visonge mbele na kuzalisha faida, ilitakiwa mali ghafi. Katika sekta ya uzalishaji mali ghafi, mambo yaliharibika pindi mkoloni alipoondoka hususa baada ya Azimio la Arusha, 1967. Watz wakiwa na jembe la mkono huko mashambani na wengine wakiwa na elimu duni katika masuala mazima ya uchumi ea viwanda, hakuna cha maana ambacho kingefanýika. Ni uvivu kwa kwenda mbelee..
Baadaye ghafla chama kikashika hatam.. balaa la uharibifu likapanuka.. meneja wa kiwana cha Bucop anapewa amri ya kutoa milioni 30 kugharamia safari ya Kawawa mkoani Kagera, bila vielelezo wala nyaraka stahiki.. naye meneja anajiongezea zake milioni 5.. na kila mahala ilikuwa hivyo..
Kwa muktadha huo, uongozi wa wakati ule unapswa kulaumiwa sehemu kwa kushindwa kufuata miiko ya kiviwanda..
Ikawaje Waasia na waarabu wakavigeuza magodown? Ni uozo tu katika nchi.. Mh Ben (RIP) anarithi mahame/mapango wananchi waliopigika kisawa sawa.. wenye kaunafuu ni wahindi kwa vile wana uwezo wa kupata vijimikopo kutoka India.. ndo ikawa hivyo..

Kazi sana kuendeleza nchi ambako watu wake hawapendi kazi.. wanapenda kula kuliko kazi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…