Hapo ndipo kuna makosa makubwa kimtazamo wa sababu ya kuviuza, haikuwa eti ni kumnufaisha mnunuzi tu. Ni ili mnunuzi ahakikishe anavirekebisha viweze kuanza kuzalisha kwa manufaa ya Taifa, haswa kiteknologia. Sasa unapouza kiwanda cha serikali halafu hakuna kipengele kama hicho cha kuhakikisha kinabakia kuwa na manufaa kwa Taifa, then huo ni ubadhirifu wa mali ya umma.
Kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba serikali yake ilitakiwa ijenge vipya vilivyo bora zaidi ndipo waviuze hivyo vilivyoundwa na Mwalimu, ili aonyeshe umahiri wake. Kama baba yako amejenga nyumba kwenye kiwanja cha familia ukaona si nzuri kipindi cha utu uzima wako, unatakiwa ujenge ya kwako iliyo bora zaidi na siyo kuibomoa aliyojenga Baba yako.
Leo hii ukiuliza fedha iliyopatikana kwa kuuza hivyo viwanda vyoote zimelinufaisha je Taifa kiuchumi haielezeki hata kidogo. Nina wasiwasi Mwalimu Nyerere alipata msongo wa mawazo kutokana na maamuzi haya ambao huenda ndiyo uliosababisha kifo chake. Hotuba ya Mwalimu Nyerere wakati wa kumteua inatosha kuthibisha hilo, it is beyond any reasonable doubt kwamba hili lilisababisha maumivu kwa Baba wa Taifa.
Ilikuwa ni muhimu maamuzi haya kujadiliwa kwa kina hata na Bunge. Vyuo vikuu tulikuwa navyo vilitakiwa vishirikishwe kufanya research ya nini kifanyike, vyuo kama UDSM, DIT, Arusha Tech, Sokoine University, Mzumbe, Chuo Cha Biashara DSM nk. walitakiwa wataalamu wapitie mkakati huo na kutoa ushauri. Unapokuwa kiongozi usiependa kushauriwa na unaishia kufanya maamuzi ya kubomoa uchumi wa nchi kiasi hicho, basi uwe tayari kushitakiwa kwa kosa la ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
Kuna mtu amesema eti Baraza la Mawaziri halihusiki moja kwa moja kutokana na mfumo wetu. Kwanini basi hakuna hata mmoja wao aliyejiuzulu ili kujitoa kwenye huo ubadhirifu? Ina maana maadili ya uongozi hakuna.
Kitendo hicho kililirudisha Taifa miaka 40 nyuma kiuchumi.