Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Hizo ndio athari za umaskin..inaharib Hadi saikolojia ya mtu...unakua unawaza upumbavu tu..na hii Iko mahala pengi sana hapa bongo ..familia Ina assets ila watoto wako mitaani eti wanajitafutia..mwisho wa siku mtoto anakuja kufanikiwa anamsahau mzazi ana deal na mkewe na watoto wake mnaanza kulalamika hamjal mzazi sjui ujinga gan, where the fuk were you
 
Kama baba yao aliweza kutafuta kwann na wao wasitafute waje wanunue ardhi kariakoo
 
Hiyo ni roho mbaya inayotusumbua waafrika ndio maana generational wealth inakuwa ngumu kwetu kwa roho kama zako, unaacha watoto wako wanadhalilika kama hawakuwa na mzazi, umaskini ni mbaya sana
Nimemuelewa mdau anasema wakiwa mafala mana yake wakiwa wajinga labda Wana tabia mbovu walevi wazinzi hawana akili ya kuamua mambo ya msingi ndio hatowapa., ila wakiwa tofaut na hapo atawapa...na ndivyo inavyopaswa kua ..unamuacha mtoto wako Hana shida yoyote na amesoma vizuri au hata kama hajasoma Hadi madigirii ila ni mtu ana akili ya maisha, unamuacha anateseka mtaani wewe unagawa mali kama karanga kwa watu Baki..ni upumbavu.
 
Mzee huyo ana busara sana
1, ameepusha ugomvi kwa watoto wake katika kugombea mali zake
2, anataka thawabu ili imsaidie huko atakapoenda baada ya maisha ya duniani
Funzo kwa watoto wote wajinga
Urithi pekee kutoka kwa wazazi wako ni elimu na sio mali (tangible)
Kila mtoto apambane kupata mali zake na kamwe usitegemee urithi
Mzazi wako alipambana ndo akapata hizo mali je wewe ukitegemea urithi utawaachia nn watoto wako
 
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee mwenye umri wa miaka 97 akiitoa nyumba yake ya kuishi yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto wake walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo


imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

Pia inashangaza familia kuruhusu mzee wa miaka 97 kufanya maamuzi makubwa kama hayo huku inajulikana akili ya mzee ni sawa na mtoto mdogo kwenye kufikiria


View attachment 3379922
Waende mahakamami, wakadeclare mental incapacitation ya baba yao, hana uwezo wa kuamua sababu ya kudorora kwa afya ya akili
 
Waende mahakamami, wakadeclare mental incapacitation ya baba yao, hana uwezo wa kuamua sababu ya kudorora kwa afya ya akili
Watoto wanaonea aibu msikiti uliopewa zawadi hiyo utawachukia na kuwaona hawapendi dini yao. Pia baba yao atawachukia kuona hawampendi Allah bali wanapenda mali
 
Baada ya kusikiliza video sasa nimeelewa. Huyo mtoto kimbembele hapo anataka kuwatapeli wenzake, maana hiyo Al-Nuur ipo chini ya milki yake yeye.., hivyo akioewa hiyo ardhi, anaweza baadae kusema msikiti umeamua kuuza ardhi yake.., na pesa akachukua yeye
 
Sasa kama ameona wanae wenyewe vilaza, mzee yupo sahihi. Ni mali yake.
 
Back
Top Bottom