Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Sasa unachobisha ni nini???
Familia nyingi za afrika watoto ndio wanapambana kama vibarua.
Kibarua huwa analipwa kitu gani ? Shares za Kampuni ? Ni kwamba wewe mzazi wako hata kama hana mali ni wajibu wake na ni lazima sababu amekuzaa ahakikishe unapata basic needs zote hata kama atakesha au kuwa omba omba..., lakini unapokuwa mtu mzima sio wajibu wake kuhakikisha kwamba alizalisha ili kuweza kuwaachia nyie. Elimu, Chakula na Shelter aliyowapa kwa miaka yote hio (tena kwa bongo mpaka mtu anauza shamba ili uende Chuo na huenda mpaka in your 30's bado anakupa hifadhi);

Baada ya hapo unachopata shukuru sio kulazimisha kama vile ni mali yenu... (Kama aliachiwa na Babu yenu that's completely difference thing i.e mali ya Ukoo). In short ni Utashi wake mwenye mali kuamua.
 
We nawe mjinga tu, kama hukumpangia baba yako kukuleta duniani basi agharamikie ujinga wake, kama huna mpango wa kuboresha maisha ya kiumbe utakachokileta duniani borq usikilete kabisa, urithi ni haki ya mtoto, issue ni urithi wa aina gani, iwe wa hali(Elimu, koneksheni, waangalizi nk) au wa mali mf nyumba, shamba, biashara nk, kuzaa mtoto kisha umwambie apambane na hali yake ni upumbavu, ni roho ya kishetani kabisa, umezaa mtoto ili uje kumuangalia akiteseka? Mbona mtoto akifanikiwa kupata mali mwenyewe wazazi wanaona ni haki yao kufaidi matunda ya mtoto wao? Ujinga kabisa.
Your too naive. Maneno ya vitabu takatifu vinasema HAKUNA MWANADAMU AKIOMBWA MKATE NA MWANAE YEYE ATAMPA NYOKA..IKIWA HATA WAOVU HUWAPA WAWAPENDAO YALIYO MEMA.

NB. UNDER THIS SCENERIO KUTAKUA NA KUTO ELEWANA BAINA YA MZEE NA WATOTO HAO

Eg. Una mtoto wako una mdukua kapeleka mwanamke hapo kariakoo kwenye kutongoza anasema nangojea mzee afariki then Tuuze tule bata na kufanya harusi. Matoto majinga majinga ya sampuli hiyo kwangu Mimi ni Bora 100.1% nitoe mali KANISA ama MSIKITINI.
 
Hata watoto kuhudumia wazazi wao ni hisani tu, sio lazima au wajibu.
Kwa binadamu (Social animals) hata kama mtu sio mzazi wangu nikiona anashida au anahitaji msaada nitatoa msaada kadri ya uwezo wangu (ni Ubinadamu) ila sio kwamba mzazi unampangia mtoto hadi bajeti kwamba vipi mwezi huu mpesa haijasoma wakati huenda mtoto na yeye maisha ya kuunga unga (alafu tukiwa na kizazi cha wala rushwa na mafisadi tunashangaa kumbe huenda ni hizi extended families)

Kwahio hapa wa kulaumiwa ni Serikali / Watunga Sera sababu kesho yetu itakuwa hatari zaidi...

 
Hiko kizee baadaye unaweza kukuta kinalaani tena watoto hawakihudumii/ hawakitunzi/wamekisahau/wamekitelekeza.
Angekuwa anategemea kusubiri kuhudumiwa na watoto wake asingejiwekea vitegauchumi kama hivyo ambavyo anavitoa sadaka kwa hiari yake na watoto haohao unaosema mzee atawalaani kwa kushindwa kumsaidia ndio wanaotoa milio. Mwambaa, tafuta zako hujaletwa duniani kuwa tegemezi asee, dunia ni uwanja wa mapambano na ndo maana tulishaambiwa tutakula kwa jasho na sio ubweteke usubiri wazaz watafute halafu ukeshe ukiomba wafe ili urithi mali zao, maana kama n mwenye kubweteka hata kama ukirithi hizo mali hutozifanyia chochote utazifuja na zitaisha zote maana huna uchungu nazo
 
Mwenye mali kaamua. Watoto na ndugu watafute mali zao.

Yeye mwenyewe huyo mzee hapo kariakoo hajanunua hilo eneo. Bali alirithi kutoka kwa wazazi wake. Kwa nini na yeye hataki generation yake irithi tena kama yeye alivyorithi
 
Akifa huo wakfu utapingwa mahakamani kuwa uliandaliwa na mtu ambaye hakuwa timamu kichwani.

Wosia wenyewe unapingwa na watu wanashinda itakuwa wakfu?

Ukitazama video hao waislamu wanaopokea hiyo zawadi wapo makini sana.. kwenye video wanasema wanaenda na mzee kwa afisa ardhi kupata hati kabisa kuonesha ardhi hiyo ni mali ya msikiti
 
Hapo kuna shidd mzazi bora ni yule anayemuachia urithi mtoto wake, hapo napingana na huyo mzee, unaacha watoto waanze moja thats very wrong

Mit 19:14​

Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
 
Kwahiyo wanae wakarithi kisenvule ndani ndani ili wakalime na mihogo kariakoo kwenye big asset wapate mashekee
Yeah.Hatujui pia alivyoipata hiyo property ya kariakoo.na hizo za huko kinsemvule unakosema.utajiri una siri nyingi mkuu.huenda watoto wasingepaweza hapo kariakoo
 
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee mwenye umri wa miaka 97 akiitoa nyumba yake ya kuishi yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto wake walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo


imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

Pia inashangaza familia kuruhusu mzee wa miaka 97 kufanya maamuzi makubwa kama hayo huku inajulikana akili ya mzee ni sawa na mtoto mdogo kwenye kufikiria


View attachment 3379922
Job true true
 
Back
Top Bottom