Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo

imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

View attachment 3379922
Mali yake anaamua aifanyie nini.

Si kila mtu anaamini katika generational wealth. Wengine wanaamini kila mtu ajitafutie mwenyewe.

Kwa nini unalazimisha kila mtu aamini katika generational wealth?

Hao watoto wake wewe ndiye unawajua kuliko yeye?

Unaelewa kuwa kuna watu wanaona generational wealth inaleta tatizo la inequality walio nacho wanazidi kuwa nacho na wasio nacho wanazidi kutokuwa nacho, na njia ya kumaliza tatizo hilo ni kuondoa habari za urithi wa mali?
 
Wewe una mtoto kwanza? Nisije nikawa najadiri jambo na mtoto ambae hata hajui mtoto mpaka kufika duniani ana gharama gani, km huna hata mtoto mmoja emu tuishie hapa maana huijui gharama ya mtoto
Fool & idiot.

Nimefunga mjadala na wewe ngumbaruu mwitu.

Nikijibishana na wewe Tena nikamatwe nipelekwe MILEMBE MENTAL HOSPITAL

Bull shit!
 
Slogan yangu ni kuwawezesha wanangu kuwa shape waweze kuyatawala mazingira yao kwanza nawapa elimu Bora.

Mtoto wangu siwalei kuanza kuangalia mali zangu ili arithi hapana kwanza Mimi nalea mtoto wangu asiwaze kurithi chochote kwangu ili akija kurithi asije kua Kama haya matoto yanayo ona mali za mzee wake ni wajibu kugawiwa.

Mzee tafuta vya kwako wafundishe wanao watafute vyao

WAHENGA HUSEMA MAREHEMU HUFA NA VYAKE PIGANA UTAFUTE VYAKO.
At least umenikosha sasa.
 
Hua nashangaanamjadili mtu na mali zake,hata angeamua kuuza sawa tu.
Mali zake,
Na watoto pia ni mali yake,
Kwa kifupi mali haiwezi kuidai mali.
 
Hakuwasomesha na kuwapa chakula mpaka pale mlipoweza kujitegemea ? Kwani yeye Babu yake alimuachia nini tuanzie hapo kwanza ?

Tutofautisha Obligation (wajibu) na uamuzi / maamuzi ; By the way kitendo cha hawa kumpeleka mahakamani inaonyesha ni jinsi gani they don't deserve hata sumni ya huyu mzee...
Mzazi wa mo dewji angekuw na fikra za aina hii, sidhani metl group ingekuwapo leo
 
Mali yake anaamua aifanyie nini.

Si kila mtu anaamini katika generational wealth. Wengine wanaamini kila mtu ajitafutie mwenyewe.

Kwa nini unalazimisha kila mtu aamini katika generational wealth?

Hao watoto wake wewe ndiye unawajua kuliko yeye?

Unaelewa kuwa kuna watu wanaona generational wealth inaleta tatizo la inequality walio nacho wanazidi kuwa nacho na wasio nacho wanazidi kutokuwa nacho, na njia ya kumaliza tatizo hilo ni kuondoa habari za urithi wa mali?
Cc. stow away
 
Mzee ana elimu ya duniya ya darasa la 7 anajua nini. Muone na kobazi lake
 
Bill Gates anagawa mali zake zote. Hamuachii mtoto yeyote urithi. Anataka watumie privilege walizopata kusimama wenyewe.

Ni mtazamo tu wa mtu na mtu. Mzee ameona kujenga taasisi kuna faida zaidi. Anaweza kuwa sahihi kwa namna nyingi tu. Hiyo taasisi inaweza kuwa chanzo cha ajira na elimu kwa watu wengi sana pamoja na watoto na wajukuu wake. Imagine mtu aliyejitolea ardhi yake kujenga Muhimbili Hospital. Wote tunanufaika sasa hivi.

Kwahiyo mzee sio mbinafsi. Wabinafsi ni wale wanaotaka wapewe wao mali.
 
Yeye kama hakupewa chochote basi baba yake anamakosa. Kama hataki kuwapa urithi watoto kwani aliwazaa? Nani alimwambia ajamiiane kwa raha zake na kuwazaa watoto ambao hataki kuwahudumia?

Umalaya uachwe kama ni hivyo?
Wapi imeandikwa ikiwa na watoto lazima uwape urithi?
 
Bill Gates anagawa mali zake zote. Hamuachii mtoto yeyote urithi. Anataka watumie privilege walizopata kusimama wenyewe.

Ni mtazamo tu wa mtu na mtu. Mzee ameona kujenga taasisi kuna faida zaidi. Anaweza kuwa sahihi kwa namna nyingi tu. Hiyo taasisi inaweza kuwa chanzo cha ajira na elimu kwa watu wengi sana pamoja na watoto na wajukuu wake. Imagine mtu aliyejitolea ardhi yake kujenga Muhimbili Hospital. Wote tunanufaika sasa hivi.

Kwahiyo mzee sio mbinafsi. Wabinafsi ni wale wanaotaka wapewe wao mali.
Sorry hapo kwa billgate i beg to differ, yes kuna kiasi atamuachia mwanae na si kweli eti everything atagawa ,check your facts kwanza
 
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo

imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

View attachment 3379922
Kwani kachuma yeye au watoto? Kafanya jambo la maana kwa akhera yake
 
Back
Top Bottom