Lakini hata kesi ya Zombe na wenzake baada ya tume kuundwa na kutoa majibu kuhusu ukweli, tatizo likaja kwenye uandishi wa mashitaka!
Mtu wa taaluma hiyo alipokwisha kulambishwa mlungula akajifanya mamuma wa taaluma, akaandika kesi miguu juu kichwa chini, hali iliyofanya Zombe akaonekana ni muungwana, afisa mpole na hajashiriki kabisa kwenye mauaji hayo na kuachiwa huru kula pensheni na hewa tulivu ya uraiani!
Na hata sasa nasikia harufu ya mambo hayo kujirudia ingawa Makamo kafoka sana hadi povu limemtoka kumshurutisha Igp aingilie kadhia ya mauaji yanayoendelea kote nchini, lakini mwisho wa jambo hili tusitarajie lolote la maana.