Baba Mzazi wa Daktari aliyepotea na Mwili kupatikana Coco Beach asema wamejulishwa mwili umeshazikwa

Baba Mzazi wa Daktari aliyepotea na Mwili kupatikana Coco Beach asema wamejulishwa mwili umeshazikwa

Dokta Hashimu Titho Kilosa alikua ni mwanafunzi wa udaktari bingwa katika Chuo cha Muhimbili na pia ni mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini (Mtwara).

Juhudi za kumtafuta Dk.Hashimu zilianza mwanzoni mwa mwezi wa tano baada ya kutopatikana kwa takribani wiki moja, ambapo baba yake, mzee Titho Kilosa ilimbidi kufika Dar es Salaam kufuatilia kilichojiri.

Siku ya Juni 04, 2025, iliweza kuthibitika kuwa mwili wa Dr. Hashim kuwa uliokotwa mnamo Aprili 24, 2025, maeneo ya Coco Beach, na taarifa hiyo kutolewa na Polisi siku hiyo hiyo.

Dk.Hashimu ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita wa Mzee Titho Kilosa ambaye makazi yake yapo mkoani Morogoro.

Chanzo: The Chanzo
sasa huyu naye alifanya kosa gani jamani?
 
Naona made
sa ya.mejichanganya! Mtu anaokotwa coco alafu maiti inahifadhiwa polisi kurasini🤔🤔😭
 
Inna lillahi wainna ilaihi rajioun.....

Poleni Wana familia.

Navyomfahamu huyo Brother na mambo ya siasa vilikua vitu viwili tofauti ....very calm person......kidogo sana mpira.
Kama ni kweli taarifa zinasema alipigwa siku ya usikilizwaji wa kesi ya Lissu ..kwa Sasa mkuu unaweza usiwe mtu wa siasa lakini ukawa moved kwenda tu kusikiliza kesi na naamin watu wengi tu ambao.sio watu wa siasa kutokana tu na uzalendo wao walifuatilia kwa kias kikubwa hili jambo la Lissu huko mahakamani
 
sasa huyu naye alifanya kosa gani jamani?

Nchi hii mbaya ukiwa kijana na safari zako ukawa sehemu isiyo sahihi kwa wakati usio sahihi kwa mujibu wa jeshi unaweza kupokea kipigo, ukatekwa, kutupwa majoring, kuuawa bila kosa lolote.
 
huyu alipigwa siku ya kesi ya Lisu na kupelekwa Mwananyamala, walipokuta kuna viongozi wa chadema wakakikmbia na marehemu ....ndiyo kapatikana sasa.......tetesi zinasema hivyo
Polisi walitoa taarifa wapi/kwa nani siku mwili ulipo okotwa April?
Ni wazi huyu ni mhanga wa matukio haya anayo yatekeleza Samia.
 
Nakumbuka hii ishu, machadema walitaka kutembelea nyota ya marehemu walidai eti ni mfuasi wao kapigwa!!! Kumbe maskini wa mungu ni mtumishi wa serikali tena DAKTARI.
Kwa hiyo kwakuwa tu alikuwa mtumishi ndio inaondoa ufuasi wake kwa Chadema?
Kwa hiyo km alipigiwa eneo walilokuwepo Chadema haikuwapasa kumtetea?

Kwa hiyo kwakuwa alikuwa mtumishi wa serikali alisitahili kuawa kama ni kweli alipigwa na hao asikari ama wengineo?
 
..marehemu alipookotwa Coco Beach alionekana amefungwa pop mkononi.

..kwanza inabidi kuchunguza kama alikuwa ameumia na alipewa matibabu ya mkono kabla hajapotea.
Kuna vitu inawezekana sijavielewa au taarifa nisizo zielewa
1. Dr angeumia angewataarifu wenzake. Kwanini simu ilikuwa off. POP angesisitiza lifungwe Muhimbili anakojua Madaktari wenzake. Polisi wameshindwa kujua mnara wa mwisho wa mawasiliano ya simu.
2. Kilwa Road ni Hospitali ya Polisi, hivi siku hizi inahifadhi miili ya Raia?
3. Hivi Jeshi la Polisi haliwezi kuchora ''sketch diagram'' inayoweza kutoa 'clue' kwa public. Kipanya anaweza
4. Maiti coco beach, taarifa Oysterbay polisi, hifadhi Kilwa road!!
 
Nakumbuka hii ishu, machadema walitaka kutembelea nyota ya marehemu walidai eti ni mfuasi wao kapigwa!!! Kumbe maskini wa mungu ni mtumishi wa serikali tena DAKTARI.
Ni dhahiri kabisa wewe ni mtu mjinga kwelikweli.
Kwa hiyo kwa fikra zako unategemea watumishi wa serikali wawe ni watu wanaoiunga mkono CCM?
 
Nakumbuka hii ishu, machadema walitaka kutembelea nyota ya marehemu walidai eti ni mfuasi wao kapigwa!!! Kumbe maskini wa mungu ni mtumishi wa serikali tena DAKTARI.
Kwahiyo chadema haina wanachama ambao ni watumishi wa serikali?

Akili zenu zipo kwenye VINYEO ama?
 
Unapoteza maisha ya binadamu kisa nini wakati duniani wote tunapita wangejua bidamu dunia tuna pita Dunia ingestarabika
 
acha uropokaji na upotoshaji gentleman 🐒
Labda nikwambie kuna dhambi utahukumiwa mbinguni,lakini kuna dhambi itabidi uhukumiwe duniani na mbinguni,ni pamoja na kumwaga damu za watu wasiokuwa na hatia
 
Back
Top Bottom