KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,893
- 3,145
1 DINI=Siku ya malipo (Kiroho)Tupe tafsiri YAKO.
Wapi Mungu kaumba dini
مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ
(AL-FAATIH'A - 4)
Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ
(AL - MAAU'N - 1)
Je! Umemwona anaye kadhibisha siku ya Malipo?
2 DINI =MILA (Kimwili)
ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ
(AN NAH'L - 123)
Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا
(AN-NISAAI - 125)
Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usalimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.
Hivyo,Kiislamu Dini ni mfumo wa maisha ya mwanadamu unaofuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu aliuelekeza kwa wanadamu kupitia mitume na manabii wake.
NA MAANA YA JUMLA YA DINI,
Ni mfumo wowote wa maisha anaoufuata mwanadamu katika kuendesha maisha yake ya kibinafsi na kijamii katika Nyanja zote za maisha.
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app