Wakuu kwema, Hii stori inamuhusu mtu wa karibu na mimi naileta kwa niaba yake, kanitumia anahitaji ushauri, nimeandika kwa kutumia uhusika wangu.
Nimekua na mahusiano na mchumba wangu kwa muda wa maika 6, na sasa nikaona imefika wakati wa kumuoa, nikaamua kwenda kumtambulisha nyumbani kwetu kijijini.
Ila tangu nimtambulishe kwetu najuta kwani sikutegemea baada ya tukio hilo haya yafuate.
Tuliporudi mjini baba alinipigia simu kuuliza iwapo mkwewe yaani mchumba wangu yuko salama nikamjibu yuko salama, akaomba kumsalimia nikampatia kwa kuwa tulikuwa pamoja akaongea naye kumuuliza hali na kumwambia kuwa yeye amefurahi sana kumuona na kwamba anakaribishwa sana kwenye familia yetu na kumtia moyo kuwa awe na amani atahakikisha mimi simtendei chochote kibaya. Kwa kweli ilinishangaza kusikia hayo ila nilipotezea.
Baada ya hapo baba akawa ananitumia ujumbe anataka namba ya simu ya mchumba wangu, nilijiuliza yeye ya nini nikawa namzungusha, nilipomshirikisha mama akanambia sasa baba yako anataka namba ya mchumba wako ya kazi gani kwa sasa na bado hamjaoana? Usimpe. Ila baba aliendelea kulazimisha mpaka nikampatia.
Baada ya kumpatia namba imegeuka kero kuu, anapiga simu kila siku kwa mchumba wangu hadi mara kumi au zaidi iwapo asipopokea, asubuhi anatuma ujumbe wa kumtakia siku njema, mchana anamjulia hali na usiku anapiga kumuaga.
Nikimuuliza baba kwa nini anafanya hivyo anasema anajenga ukaribu na mkwewe kwani huyo sasa ni binti yake, na anakua mkali sana iwapo nikiuliza ananifokea kuwa nina mawazo mabaya kwa kuwa jambo analofanya si baya. Na ikitokea asipopokea ananipigia mimi kuniuliza kwa nini kapiga simu mchumba wangunhajapokea.
Mchumba wangu kafikia hatua ya kuchoka anawaza kumblock baba yangu, ila anaona kama atakua kamvunjia heshima, nami nimewaza kufanya hivyo pia. Pia ni kama hali hii imeanza kumtia mashaka kukubali kuolewa na mimi akidai huenda baba yangu ana ajenda ya siri labd hata anamtaka.
Wakuu, mnamshauri afanyaje? Akimblock atakuwa saawa?