Baba yangu alilazimisha sana nimpe namba ya simu ya mchumba wangu, sasa anampigia simu hadi mara 10 kwa siku kumjulia hali

Msiwe na mawazo potofu

Sio Wazazi wote ni mabazazi wasio jielewa

Inaonekana Mzee wako yupo kwenye zoezi la kumchunguza mchumba/mkeo mtarajiwa

Kupitia kuongea naye mara kwa mara, kuna vitu atavijua kumhusu huyo bibie ambavyo wewe hujavijua
Sasa mzee amchunguze mkwe ili iweje? Kwani ana muoa yeye? Kazi ipo.
 
Hakuwahi kuvuta bangi ujanani?Bangi affection!
 
Msiwe na mawazo potofu

Sio Wazazi wote ni mabazazi wasio jielewa

Inaonekana Mzee wako yupo kwenye zoezi la kumchunguza mchumba/mkeo mtarajiwa

Kupitia kuongea naye mara kwa mara, kuna vitu atavijua kumhusu huyo bibie ambavyo wewe hujavijua
Pia mzee kama yupo kijijini hii hutokea sis watu wa kijijni huwa tunawashobokea watu wa mjini.
Hata hivo amuache tu mzee apige simu maana hatoweza kupiga kila siku mfululizo kwa miaka 2.
Ashauriane tu mzee wake kuwa sio kila saa ni wa kupiga simu kuna muda wa kaz na faragha.
 
Mmh! Mkuu hivyo kumchunguza mtu ni kumtakia asubuhi njema, mchana mwema na jioni njema zisokwisha?
Kwani kuna shida ipi Baba kumsalimia mkwewe? Anaonesha anajali na kumpenda mkwewe.

Kwa familia nyingine angeshamkataa, na kumwambia Kijana wake atafute mchumba mwingine
Wewe umewahi kufanya hivyo kwa mkweo?Mana nasikiaga wanakuita babu. 😀
Mimi nimewahi, sio mara moja ni zaidi ya mara tatu maana vijana wangu wote wameoa

Sisi kikwetu, hairuhusiwi kulala na mke wa mwanao/mke wa kaka/mdogo wako

Ikitokea binti akaonesha hizo dalili za kutengeneza mazingira alalwe na shemeji/mkwe basi ndiyo mwisho wa ndoa yake

NB; ni kweli nimekula chumvi nyingi mjukuu 🤭
 
Ni kweli Mkuu

Unajua changamoto ya vijana wengi wa miaka hii, ni kudhani uhuni wanaofanya wao basi na Wazee wao wanaweza kuufanya

Siku hizi ni kawaida kaka kutaka kulala na mke wa mdogo wake (Wanasema hainaga ushemeji 🙌)

Jambo ambalo, sisi wa zamani tulikuwa hatufanyi na kulikuwa na mipaka kikubwa dhidi ya shemeji zetu
 
Sasa mzee amchunguze mkwe ili iweje? Kwani ana muoa yeye? Kazi ipo.
Kupitia mke ambaye Kijana wangu ataoa, ndipo jina la ukoo na familia yangu kwa ujumla itapata kuongezeka.

Kwahiyo Kijana wako akioa mke asiye na maadili, ni dhahiri kwamba anakwenda kuniletea wajukuu wasio na maadili

Ndiyo maana zamani, tuliwachagulia vijana wetu wake na waume wa kuolewa nao

Lengo ni kupata familia zitakazokuwa na ustawi
 
Hivi Gran Pah, wewe kichwani kwako unawaza kizazi kuendeleza tu? Huna kingine? Hope siku ikiwa tofauti unapotea mazima.
Unakua km mjima, Lol.
 
Hili suala mbona jepesi sana dingi ni mwanaume mwenzangu
ningemchana makavu live face to face!
 
Hivi Gran Pah, wewe kichwani kwako unawaza kizazi kuendeleza tu? Huna kingine? Hope siku ikiwa tofauti unapotea mazima.
Unakua km mjima, Lol.
Bila kuwa na mtazamo huu, unadhani wewe ungezaliwa mjukuu?

Kila siku watu wanakufa na kuzaliwa wengine, bila kuzaliana, Dunia si itafikia mwisho?

Pambana na yule mkwe uliyenaye, mtuletee wajukuu sawa

Mimi na bibienu, hatuwezi kukaa nyumba yote hii kubwa bila mjukuu 🤭
 
Hivi mfano ukute mwanao hana uwezo wa kuzalisha (siombei) utafanyaje? Maana wee akili yako unawaza kizazi kuendelezwa, au yeye huyo akiwa hataki watoto??
 
Halafu jamaa anataka kutenga mke na wakwe zake, atakuja kukumbuka kumekucha.
 
Wacha amlombe....wewe inakuhusu nini ? Maisha yenyewe mafupi, dunia imevaa bukta
 
Katika amrii kumi za Mungu,
kuna moja inasema,
"Waheshimu baba na mama ili upate miaka mingi na heri duniani". Vijana wengi leo hii kwa kiburi wanakosa heri za wazazi wao na ku r.i.p wakiwa wadogo sana.

Gentleman,
kukataa ukaribu wa mawasiliono na baba yako mzazi, dhidi yako na mchumba wako ni kukaataa baraka za kuishi miaka mingi, furaha na kheri duniani. Tena unazikataa kwa ukali huku ukimuwazia baba yako mzazi mabaya, huko ni kuchuma laana na mikosi wazi wazi kabisa.

In fact,
mkufunga ndoa na kuzaa watoto, hutaona ukaribu wa Baba yako dhidi yako au mchumba wako ispokua wajukuu wake 🐒
 
Hivi mfano ukute mwanao hana uwezo wa kuzalisha (siombei) utafanyaje? Maana wee akili yako unawaza kizazi kuendelezwa, au yeye huyo akiwa hataki watoto??
Ikitokea imetokea, najua majirani wanaweza kumsaidia kumjaza mimba mkewe

Nasisi kama kawaida ya Wazee, tutasema kitanda hakizai haramu. Muhimu nitakuwa na mjukuu

Hata hivyo, ni ndoto ya kila Mwanaume kuwa na familia yake

Mimi Baba yake nilikuwa na ndoto hiyo, ndiyo maana tumewapata wao, ni maoni yangu kwamba hata wao (watoto wangu) watapenda kuwa na watoto wao

✓Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
✓Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hatoiacha hata atakapokuwa Mzee
 
Wakuu, mnamshauri afanyaje? Akimblock atakuwa saawa?
Siyo sawa kum block.

Mnaweza kufanya moja ya mambo mawili:

1. Futa namba ya mkeo kwenye simu ya baba ako - hili lifanywe kupitia mama ako au ndugu kijijini huko. Ukute ikifutwa hatoikumbuka.
2. Mchumba wako asitishe kutumia namba ya sasa. Asajili mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…