Baba yangu hakuniachia urithi lakini ndugu zangu wengine wamepewa wote, je nikijitenga na ile familia nakosea?

Baba yangu hakuniachia urithi lakini ndugu zangu wengine wamepewa wote, je nikijitenga na ile familia nakosea?

Mimi ni mzaliwa wa mwisho kati ya watoto tisa, wanaume watano na wanawake wanne
Wakati mzee wetu anaandika urithi aliandikia wanaume wanne tu akaagiza shamba ligawe mara nne tu wakati mimi ni watano wala hakunijumuisha

Mimi sikujua chochote kipindi hicho mana nilikuwa mdogo, baada ya kukua ndipo nikajaikuta karatasi ya wosia wake ndani ya sanduku lake
Nilisoma huku nabubujika machozi kiasi gani baba yangu alikuwa fedhuli na kuacha kunijumuisha kama mtoto wake kwenye mirathi yake wakati amenizaa na mama yangu na mimi sio mtoto wa nje

Nimebeba hayo maumivu mpaka sasa sikutaka kabisa kuwa na roho mbaya nianze kudai mirathi nilichojisemea ni kuwa kama alinyima ni sawa yote ni maisha

Lakini nimeona haitoshi nisiishie hapo tu nimeamua kujiondoa kwenye ile familia ambayo sikuhesabiwa na wala sitadai chochote
Je mimi kujitenga niko sawa au nakosea

Mimi binafsi sioni kama nakosea kwasababu sitaki kujipendekeza familia niliyotupiliwa nje
Kuvuja kwa pakacha?

Jitenge tu… who cares?
 
Kama hakutoa sababu za kwanini hakukupa urithi wakati wewe ni mrithi halali unaweza kupinga wosia huo
Ile familia hakuna mali zao ninazozitaka hata wakinipa sitapokea kinachonitesa kwanini baba yangu mzazi anifanyie hivi inamaana mimi ni mbwa wale ndio watoto
 
Kwanza huyo mzee aliye acha wosia amekosea na ikiwa ndugu wapo hai inabidi muwatafute wanaojua kugawa urithi ili mumuokoe baba yenu huko alipo maana hata kama alikuwa anatenda mema basi kwa kosa hilo alofanya ALLAH(S.W) anamuadhibu.
 
Kwani walimtenga?
Baba yangu mzazi amenitupa na kunisaliti wala hakunihesabia kama mtoto wake na amenizaa yeye
Baba mwenye tabia ya kupendelea na kibagua watoto
 
B
Pambana kutafuta vyako usiku na muchana mpaka siku moja wajutie kukutenga
Brother Mshua naamin kakuachia mwanga wa kupambana yawezekana miongn mw watto wake aliemuona anauwezo wa kupambana na kusaidia familia yake kifikira hapo badae
 
Nduguzo wao wanasema kwann hukujumuishwa? Umewahi kuwauliza swali hilo? Je mama nae amekwambia sababu n nini?
 
Mimi ni mzaliwa wa mwisho kati ya watoto tisa, wanaume watano na wanawake wanne
Wakati mzee wetu anaandika urithi aliandikia wanaume wanne tu akaagiza shamba ligawe mara nne tu wakati mimi ni watano wala hakunijumuisha

Mimi sikujua chochote kipindi hicho mana nilikuwa mdogo, baada ya kukua ndipo nikajaikuta karatasi ya wosia wake ndani ya sanduku lake
Nilisoma huku nabubujika machozi kiasi gani baba yangu alikuwa fedhuli na kuacha kunijumuisha kama mtoto wake kwenye mirathi yake wakati amenizaa na mama yangu na mimi sio mtoto wa nje

Nimebeba hayo maumivu mpaka sasa sikutaka kabisa kuwa na roho mbaya nianze kudai mirathi nilichojisemea ni kuwa kama alinyima ni sawa yote ni maisha

Lakini nimeona haitoshi nisiishie hapo tu nimeamua kujiondoa kwenye ile familia ambayo sikuhesabiwa na wala sitadai chochote
Je mimi kujitenga niko sawa au nakosea

Mimi binafsi sioni kama nakosea kwasababu sitaki kujipendekeza familia niliyotupiliwa nje
Kwa mtazamo wangu Mimi, Mzee wako anasababu ya kutokukupa urithi, ongea vizuri na mama yako utajua kwa nini
Pili hadithi za urithi hazina ishu sana, kama umezaliwa na viungo vyote salama, pambana upate vyako na ww uje kurithisha, unadhani Mzee wako alirithi hizo mali? alizitafuta kwa jasho, kwahiyo na ww pambana kwa jasho upate zako
Tatu kujitenga na familia haibadilishi chochote zaidi yakukuongezea chuki na maumivu moyoni mwako. Maisha Yana mapito mengi kumbuka alie kubagua ni Mzee wako sio hao wanafamilia wengine
 
Utakuwa sio mwanae kuna siri anajua peleleza kuna jamaa yangu alifanyiwa hv na baba yake baadae akaja kugundua sio mtoto wa yule mzee ila akakausha tu maisha yaendelee maana kashafika miaka 57 akasema ataenda wapi umri umemkimbia.
 
Nduguzo wao wanasema kwann hukujumuishwa? Umewahi kuwauliza swali hilo? Je mama nae amekwambia sababu n nini?
Ndugu zangu wanafurahia kupewa thamani mimi wananichukulia mbwa wao
Nimeamua kutoshiriki jambo lolote ni majuzi wamenipigia simu za kunitaka nihudhurie vikao vyao kutokana na hasira niliyonayo nikavunja ile laini mpaka sasa nina laini mpya sitaki kuwakumbuka kwasababu kila napofanya hivyo hasira inapanda sana, wanathubutuje kunifata fata wakati wao ndio watoto mimi ndiye mbwa
Mtu unaweza kuzaliwa mwema lakini badae ukaamua kuwa nyoka kwakusababishiwa
 
Pole sana kwa yote , kwa vyovyote hapo wanapoishi Wazazi wako ndiyo urithi wako pia pambana ili upate vya kwako.
 
Aah unakosea kujitenga hiyo ni familia yako endelea kuwanao..ilichopaswa ukijue n kwann hukujumuishwa kwny mirath? alfu isitoshe hyo isikufnye ujione hiyo sio familia yako, Cha msingi Pambana tafuta chako.
 
sasa unataka ujiondoe kwenye hiyo familia ili iweje?kwan wao ndio walio kutenga kwenye mirathi au ni baba yako?binafsi sizan kama ni uamizi sahihi hio itakua ni roho mbaya unafanya kwa sababu ndugu unao taka kujitenga nao ...hawahusiki katika kugawa hiyi mirathi, hapo mtu wa kumchukia ni huyu marehemu baba yako na sio hao ndugu zako ambao na wenyewe waligawiwa tu hiyo mirathi na mzee kama watoto pia...
 
Kikubwa uzima upo mikono na miguu unayo macho unayo nitume Fanya kazi kwabidii usijitenge na familia waatabaki kuwa Ndugu na familia Yako hata kama ukijitenga haitabadili chochote wewe tafuta vya kwako heshimu familia unachotakiwa kufanya nikufanya kazi kwabidii zilizohalali ardhi haipiganiwi heshimu unachopata ili uwe na maendeleo asilimia kubwa familia nyingi watu wanauwana wanalogana kwasababu ya mali za urithi baba kutokukupa urithi usimlaumu mshukuru kwasababu kakuepusha na mengi ipende familia Yako na Ndugu zako tengeneza maisha Yako na umshukuru kwa unachopata
 
Mwanangu wewe pambania vyako, mimi nilizaliwa peke yangu kwa baba yangu na alifariki ni kiwa na mwaka 1 tu,.

Mzee alikuwa mfanyabiashara Malawi, Tz,na huko inasemekana alikuwa na vijimali ila alikuwa kivyake vyake Sana,.

Alienda malawi, akarudi Home mgonjwa haongei chcochote, haikueleweka nini alikiwa anaumwa mpaka unsure unamkuta.

Aliacha nyumba,ile nyumba sikuwahi kupewa maelezo yakutosha ,hakuna mtu alikuwa anaifuatilia, wapangaji walikuwa wanaishi Lamar bure tu maana dingi mkubwa ambaye ndiye msimamizi alikuwa busy na mambo yake.

Ile nyumba ilipigwa mnada mimi nikanunuliwa mitumba ya buku 10 tu, fresh, nashukuru Muumba mimi nahesabia zone pesa za nyumba ndio zilinisomesha japo najua waliuza Kwa ajili gani,tangia shule ya msingi nilishaapia sitamfuatilia masuala ya Marathi nitatafuta vyangu.

Pambana upate vyako mkuu.
 
Kwa kauli zako dhidi ya baba yako ni wazi kuwa wewe ndio tatizo na baba yako aliliona hilo katika hisia zake kabla ya wewe kujitambua. Kwa hizo kauli dhidi ya marehemu baba yako histahili kulithi hata kijiko.
 
Back
Top Bottom