Mimi ni mzaliwa wa mwisho kati ya watoto tisa, wanaume watano na wanawake wanne
Wakati mzee wetu anaandika urithi aliandikia wanaume wanne tu akaagiza shamba ligawe mara nne tu wakati mimi ni watano wala hakunijumuisha
Mimi sikujua chochote kipindi hicho mana nilikuwa mdogo, baada ya kukua ndipo nikajaikuta karatasi ya wosia wake ndani ya sanduku lake
Nilisoma huku nabubujika machozi kiasi gani baba yangu alikuwa fedhuli na kuacha kunijumuisha kama mtoto wake kwenye mirathi yake wakati amenizaa na mama yangu na mimi sio mtoto wa nje
Nimebeba hayo maumivu mpaka sasa sikutaka kabisa kuwa na roho mbaya nianze kudai mirathi nilichojisemea ni kuwa kama alinyima ni sawa yote ni maisha
Lakini nimeona haitoshi nisiishie hapo tu nimeamua kujiondoa kwenye ile familia ambayo sikuhesabiwa na wala sitadai chochote
Je mimi kujitenga niko sawa au nakosea
Mimi binafsi sioni kama nakosea kwasababu sitaki kujipendekeza familia niliyotupiliwa nje
Baba yako akuzae ,akuchagulie Mama,akuchagulie ndugu wako wa karibu ,akusomeshe ,akupe jina unalotumia hadi sasa.
Hata huu uwezo ulikuja hapa kuandika ,kumdhalilisha humu ,umekupa yeye,akili amekugaia
Bado huoni ni urithi tosha ,
Acha malalamiko ,Dunia iko wazi sana ikufanye nawewe utafute zakoo.
Ni aibu Sanaa na unataibisha wanaume
Umetukosea Sanaa, unamdhalilisha sana baba yakoo.
Nakuambia utateseka Sanaa, njia pekee rudi kamuombe radhi baba yako kwa hichi ulichokufanya hapo njia zako zitafunguka .
Ushauri tuuu Mkuu ,najua utachukulia kichanyaa.