Baba yangu hakuniachia urithi lakini ndugu zangu wengine wamepewa wote, je nikijitenga na ile familia nakosea?

Mama yako yupo?Kama yupo,kaa naye umuulize hayo maswali/masuala yanayokutatiza.Anayo majibu yake.
 
Kuna haya mawili matatu:

Kwanza yawezekana aliandika wosia kabla hujazaliwa kwani hata wewe Umesema uligundua hilo ukiwa mdogo sana. Hivyo mzee wako hana nia mbaya na wewe.

Pili kama wewe ni Mchagga basi huwa kitindamimba wa kiume huwa ni mrithi wa nyumbani na hurithi nyumba na shamba la asili la nyumbani hivyo angalia hilo.

Tatu usijitenge na familia utakuwa umepiteza kitu kikubwa zaidi kuliko shamba.

Nne angalia kama kuna wosia mwingine pengine umeachiwa acount ya benk yenye thamani mara 5 ya hayo mashamba.
 
We b..o..y..a una tatizo fulani la kisaikolojia kichwani , nikiunganisha dots na ule uzi wako wa kushinda bet ukajenga nyumba namna unavomchukia mama yako!!! Hebu fanya haraka nenda hospitali kwa wataalamu wa saikolojia.
 
Ebu acha sasa, labda siyo baba yako ndiyo maana mzee hakutaka urithi. Ndoa zina mengi ujue oooh.
 
Weee
We b..o..y..a una tatizo fulani la kisaikolojia kichwani , nikiunganisha dots na ule uzi wako wa kushinda bet ukajenga nyumba namna unavomchukia mama yako!!! Hebu fanya haraka nenda hospitali kwa wataalamu wa saikolojia.
Wewe ni mtu katili sana, mimi nitendwe vibaya bado ugongelee msumari asee wewe hapana sio binadamu
 
Umezungumza jambo kubwa sana
 
Labda mzee aliandika wosia kabla haujazaliwa akasahau kuedit baadae hata ivyo una uhakika kama uyo ni baba yako kabisa? Si ajabu mzee alibambikiwa mtoto akatumia busara tu kukaa kimya
 
Kwani baba
 
Kwani Baba yako alipate hizo mali?
Je,unauhakika Mama yako alimwambia nini Baba yako kuhusu uzao wako?
Je,tabia zako zikoje maana hata tukupost mambo ya Baba yako ni ishara kwamba kimaadili kuna walakini na inaweza kuwa sababu ya kuachwa solemba.
Inakuwaje wale watoto wanne walipopewa walichopewa bado nao hawana huruma nawe ili wakusaidie?
Ukoo mzima haukupendi? Tafakari
 
Hiyo hujuma alinifanyia baba yangu nikiwa na miak miwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…