Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Kunywa maji ya kutosha mkuu
Huwezi kunipangia mifumo ya maisha au siwezi amino unachokiishi kukuamini kunywa. Maji kwangu zambi lakin kugegeda wake za watu baridi tu
 
Sio lazima mtumie kondomu,unaweza kufunga uzazi kwa operasheni.
That is the last stupid thing you do before you die.

Madaktari siku hizi wanashauri mtu afanyiwe operation pale tu ambapo hakuna njia mbadala, sasa wewe mtu na afya yako unakwenda kufanyiwa operation uwe hanisi. Ssasa mwanaume ukisha fanyiwa hiyo operation halafu mbegu zitoke butu au zisitoke kabisa utakua mtu wa namna gani.

Mwanamke akikushauri ufanyiwe huo upuuzi achana nae.
 
Hiyo ya three children a maximum ni kanuni yako uliyojitungia, hata ukisoma maandiko yote ya family planning hawajaweka limit ya idadi ya watoto.

Katika family planning unaelekezwa kuzaa watoto kwa utaratibu wa angalau kila baada ya miaka 2 au 3 ili mama apate muda mzuri wa kumtunza mtoto na yeye mwenyewe Afya yake iwe katika hali nzuri kabla ya kubeba ujauzito mwingine.

Pia inatoa fursa ya kujitathimini kiuchumi Kama unaweza kuongeza mtoto mwingine. Kwa hiyo Kama mtu atafuata utaratibu huo anaweza kuzaa hata watoto Saba.

Tatizo lako inawezekana hali yako ya kiuchumi inakulazimu uishie kuzaa watoto watatu, kwa hiyo unataka kugeneralize, au umekalili tu kuwa ukifuata uzazi wa mpango basi hutakiwi kuzidi watoto watatu.
 
Mi mtoto was sister analingana na pengine nimkubwa kidogo na mdogo wangu wa mwisho sijui bana watajua wenyewe
 
Huu ndio ukweli. Katika uhalisia, wadada huolewa beteeen 14------18 years, 15 years later, mwanaye anaanza kuzaa huku mama akiwa 30 years na bado ana mayai ya kutosha. Nimeshuhudia mama aliyezaa watoto 14, hapa lazima watoto walingane na wazazi wao
 
Mleta mada yamemkuta haya mambo, sasa anajisikia vibaya inakuwaje yeye ana miaka 25 halafu mjombaake ndo kwanza kazaliwa mkesha wa mwaka mpya, na kwa mila za kwao ni lazima AMUAMKIE kwa kupiga goti! [emoji23][emoji23]
 
Halafu huyu jamaa, haya maneno USTAARABU, MAADILI na STAHA anayatumia tu lkn hajui hata maana zake! [emoji23]
 
Kwa hiyo kwa sababu wewe ni muafrika ndio uzae kama sungura? Akili za wapi hizi!
hata sijazungumzia kuzaa watoto wengi km sungura, kinachozungumzwa hapa ni sawa au si sawa kuzaa pamoja na mtoto wako. kwangu mimi nimesema sioni tatizo lolote km mazingira, hususani ya uhitaji na usalama, yanaruhusu. ndicho nilichosema mkuu!!
 
Kama Kigezo ni kipato cha kuwapa elimu watoto na future nzuri, basi hapo moja kwa moja jidharau wewe na umasikini wako, au panua wigo wa kipato, kama we ni mwajiriwa na kipato chako kiko fixed huna budi kufanya hayo mafamily planning yako.

Kuna watu wana pesa mpaka zinamwagika, na investments za kutosha hawa nao uwapangie uzazi. By the way kila mtu ajaye hapa duniani mwenyezi mungu kampangia destiny yake.

BRAIN WASHED.
 
Mleta mada yamemkuta haya mambo, sasa anajisikia vibaya inakuwaje yeye ana miaka 25 halafu mjombaake ndo kwanza kazaliwa mkesha wa mwaka mpya, na kwa mila za kwao ni lazima AMUAMKIE kwa kupiga goti! [emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwa mtu kama wewe na hii mentality yako basi nadhani ulistahiki kuandika hivi,lakini kwa mtu ambae anamentity ya kumkuza mtoto wake kwa kujitegemea na kuwa mpiganaji basi hawezi kuona shida kuzaa.

Wangapi wametoboa leo bila hata ya sapoti ya shule na kutafutiwa ajira na baba zao, wapo kibao.

Lakini kazi kubwa ya mzazi ilikuwa ni kulea na wengine hata hhawakulelewa na wazazi lakini wametoboa fresh.

Kikubwa riziki haiko fixed,we ukija leo duniani utapambana na utapata riziki yako
 
Hapana sio maneno ya mwenye kushiba, hata kidogo!

Nimefikiria tu binti yangu awe na umri wa miaka 18 which means soon ataleta wajukuu kwanini nisiendelee kuwajengea wao misingi imara badala ya kuhangaika na vitanda vya leba?...
sawa, lkn bado hilo naona si salama sana kwako kwani sio wako hao....furaha ya kweli na ya kudumu ipo katika chako; isitoshe km uwezo upo bado unaweza tu kulea na hao wajukuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…