Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Binafsi mimi nisingezaa tena! Ningesubiri wajukuu!

Hao ningewafanya wanangu na pia kwa mzazi kupata Mjukuu ukiwa bado na nguvu basi ni kama baraka!

It’s like getting a second chance to create a whole human being again, kwa kutumia ujuzi na makosa ya zamani kufanya bora zaidi!
Safi sana mkuu
 
Na huu ndio mzizi wa umaskini katika familia zetu nyingi!

Mtu tangu kabaleghe yeye anafanya kazi ya kuzalisha na kulisha kiasi kwamba hata muda wa kulea na kuwekeza zaidi hautoshi na rasilimali ni ndogo kuja kushtuka yuko na 50 years!..
Sisi waafrika bado tuna safari ndefu sana ya mafanikio
 
coach, maneno ya mwenye kushiba hayo!! mtoto ana raha yake asikwambie mtu; isitoshe kuna wimbi la wazazi wasiotaka au kupenda watoto wao kulelewa na mabibi siku hizi......ungelipata tabu na majuto.

Hapana sio maneno ya mwenye kushiba, hata kidogo!

Nimefikiria tu binti yangu awe na umri wa miaka 18 which means soon ataleta wajukuu kwanini nisiendelee kuwajengea wao misingi imara badala ya kuhangaika na vitanda vya leba?

Kuna busara sana katika mzazi wako kusimamia wanao ambae ni wajukuu zake na ndivyo familia na koo bora zinavyojengwa!

Vinginevyo utajikuta katika umri wa miaka 54 mwanao mdogo Ana miaka 3 na babake Ana miaka 60 huko, matokeo yake mkiondoka mzigo mnauacha kwa watoto wakubwa ambao pia hata misingi imara mlikosa nafasi ya kutosha kuwaandalia! Ni mzunguko mbaya sana sana!
 
Naona Sasa umeanza kujifananisha na samaki[emoji23][emoji23]
Ila usisahau huna asili ya samaki. Acha samaki aitwe samaki.

Kutoa mfano ni sawa na kujifananisha??

Nimekuuliza mbona nature imekupa uwezo wa kutoa sperms zenye uhai zaidi ya elfu lakini mara nyingi atazaliwa mtoto mmoja, mapacha ama triplets na quadruplets in few cases, kwanini hawatoki wote kwa maelfu kwa wakati mmoja??
 
Watoto kumi unataka kufungua timu ya mpira?!


Nimetolea mfano tu chief! Ila binafsi nikijaaliwa 5 si haba!

Ila kumi kama pesa ipo na umri unaruhusu why not? Mimi napenda mtoto wangu wa mwisho akiwa na 15 years basi niwe na angalau 40 ama 46 angalau nipate nafasi ya kutosha kuwafahamu hao binaadam ambao tumewatengeneza na kushirikiana nao katika kuwaandalia kizazi chao (wajukuu zetu) mazingira muhimu!
 
Ukiamua kuzaa uwe na mpango thabiti wa kutunza pia, ni jambo la ajabu kuzaa ukitegemea utatunziwa na wengine.
najua ni mbaya lakini hakuna mwenye guarantee ya kuishi cha msingi ni kumuandalia mazingira mazuri yaani hata usipokuwapo kazi iwe katika usimamizi tu na si matunzo kiujumla
 
Sio jambo zuri kuzaa ikiwa mtoto ako tayar kaisha pevuka, ila kuna mda inabid iwe hvyo
Mfano:- mtu nimezaa nikiwa na miaka 18 (ilikuwa bahata mbaya na sikutaka abortion) baada ya hapo nikasema sasa naitaji kurekebisha makosa, nikaamua kutulia kuanza kuandaa life langu kwanza ( nikarudi school) ndio nije nizae tena hapo nakuja kusema sasa naitaji mtoto wa pili nina miaka 35 mtoto wa kwanza kaisha vunja ungo tayari. Unazania nn kitatokea kwa kizazi hiki
u are correct
 
Rafiki yangu ana Baba wadogo (wakubwa) wenye miaka 3, ila sina uhakika na jina rasmi labda mnisaidie. Ni hivi, kaka wa Babu yake aliongeza mke wa 3 akazaa mtoto. Je huyo mtoto anamuitaje?
 
Back
Top Bottom